Mungi
JF Gold Member
- Sep 23, 2010
- 16,975
- 9,566
Mwenyekiti serikali ya mtaa wa sanawari Arusha amekamatwa na polisi baada ya kuvunja tawi la chadema.
Awali uongozi wa chadema kata ya Sekei baada ya kupata taarifa ulikwenda kituo cha polisi Sekei kutoa taarifa. OCS wa kituo alisema japo walikuwa wana taarifa kuwa tawi litavunjwa na Godfrey, hawatatoa) ya kumkamata. Ikabidi uongozi wa chadema uende Kituo Kikuu cha Arusha na kuandika maelezo na kupewa RB.
Hata hivyo leo asubuhi kuliibuka taharuki kubwa nyumbani kwa mwenyekiti huyo wa mtaa aliyetokana na ccm, baada ya polisi kushindwa kumkamata jana, vijana wenye hasira walikusanyika nyumbani kwa mwenyekiti wa mtaa wakitaka kumchomea nyumba. Vijana walilalamika inakuwaje watumie fedha zao kujenga tawi halafu ccm wanakuja kuvunja bila sababu! Uongozi wa chadema kata ya Sekei ilibidi wawasihi vijana waliokusanyika kwa wingi wasifanye uharibifu wowote, wasubiri polisi wafanye kazi yao. Polisi walifika pale wakiongozwa na Inspector Daudi.
Hivi sasa huyo Mwenyekiti huyo yupo selo akisubiri dhamana