Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu mkoa wa Mbeya atumbuliwa

lusaka city

Senior Member
Mar 17, 2015
145
225
CHAMA CHA MAPINDUZI
SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU MKOA WA MBEYA.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi.

Leo tarehe 19. 12. 2016 umefanyika mkutano mkuu wa dharula wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya juu mkoa wa Mbeya.

Madhumuni ya mkutano huo ulikuwa ni kujadili waraka uliotolewa na Ndugu Alex Kinyamagoha tarehe 15. 12. 2016 ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa Shirikisho la vyuo vya Elimu ya juu mkoa wa Mbeya.

Ndugu Alex Kinyamagoha pamoja na mambo mengine amekwenda kinyume na katiba ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2012. Aidha, amevunja kanuni za shirikisho la vyuo vya elimu juu Tanzania.

Mkutano mkuu wa shirikisho la vyuo vya elimu ya juu mkoa wa Mbeya kwa mamlaka ulionayo umemvua NduguAlex Kinyamagoha madaraka yake ya mwenyekiti wa shirikisho kuanzia leo tarehe 19. 12. 2016.

Nafasi ya mwenyekiti wa shirikisho la vyuo vya Elimu ya juu mkoa wa Mbeya itakaimiwa na Ndugu Michael Rutundwe Malegesi ambaye ni Katibu mtendaji wa shirikisho la vyuo vya Elimu ya juu mkoa wa Mbeya mpaka uchauzi wa kuziba nafasi utakapofanyika.

Tuendelee kuwa wamoja na tuendelee kuwa na mshikamano ili tuendelee kukiimarisha chama chetu.

Kidumu Chama cha Mapinduzi.

Oddo Aidan Ndunguru,
Katibu wa Siasa na Uenezi,
Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu,
MKOA WA MBEYA
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom