Mwenyekiti wa NEC Jaji Kaijage atoa somo kwa Vyama vya Siasa na Wagombea Udiwani

Mwakaboko King

JF-Expert Member
Apr 22, 2015
1,099
207


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistolces Kaijage amevitaka vyama vya siasa kufanya kampeni kwa kuzingatia maadili ya Uchaguzi.

Jaji Kaijage ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa NEC na vyama vya siasa uliofanyika jijini Dar es Salaam kuelekea Uchaguzi mdogo wa madiwani.


Alisema iwapo ukiukwaji au uvunjaji wa Maadili hayo utatokea, Chama au Mgombea awasilishe malalamiko hayo mbele ya Kamati husika ili ishughulikiwe kisheria.

Aliwakumbusha kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 53 cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 Tume inayo mamlaka ya kuruhusu kuwepo kwa Kampeni za Uchaguzi katika maeneo ya Uchaguzi na siyo Mikutano ya Vyama vya Siasa.

Hivyo, kampeni hizo zifanyike kwenye Kata husika na inategemewa kuwa Mikutano ya Kampeni italenga kuwashawishi, kwa namna ya kistaarabu, wananchi wa Kata husika ili wamchague Mgombea anayefanyiwa kampeni.

” Kwa mujibu wa kipengele cha 2.1. (C) cha Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 tunategemea kila Chama cha Siasa kiendelee kufanya Kampeni kwa mujibu wa ratiba. Kampeni zote zinatakiwa kuanza saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni” alisema Jaji Kaijage.

Aliongeza kuwa kwa kuzingatia Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015, Tume imekwisha kutoa ushauri kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya ili katika kipindi hiki cha Uchaguzi wahakikishe wanazingatia wajibu wao na ukomo wa madaraka yao katika shughuli za Uchaguzi kuanzia kipindi cha Kampeni hadi kutangazwa kwa Matokeo.

Naye Mkurugenzi wa Uchaguzi kailima Ramadhani aliaviomba Vyama vya Siasa kuwahimiza wanachama na wapenzi wao walioandikishwa kuwa Wapiga Kura wajitokeze Siku ya Uchaguzi kwenda Kupiga Kura zao bila hofu yoyote kuhusu usalama wao.

“Ni imani ya Tume kuwa Viongozi wa Vyama vya Siasa mtakuwa chachu ya kuwaongoza na kuwaelekeza wanachama, wafuasi na mashabiki wenu katika kushiriki uchaguzi kwa amani na utulivu’ alisema Kailima.

Uchaguzi Mdogo wa madiwani katika kata 43 za Tanzania Bara, unatarajiwa kufanyika tarehe 26 Novemba, 2017 ambapo wapiga kura 333,309 wanategemewa kupiga kura siku ya uchaguzi

CHANZO: NEC ONLINE TV - TANZANIA
 
Tume imeshaanda maneno yanayopaswa kutumika kwenye kampeni

ifanye haraka kuyagawa kwa vyama vinavyohusika
 
Kila lakheri wagombea udiwani wote
mpige kampeni za kistaarabu cause
kuna maisha baada ya uchaguzi
 
Tume imeshaanda maneno yanayopaswa kutumika kwenye kampeni

ifanye haraka kuyagawa kwa vyama vinavyohusika

Sio kazi ya NEC kunadi au kutengeneza Ilani za vyama! Inaelekea hata mikutano ya kampeni hauendi, Mi nachojua kila mgombea atapimwa na wananchi wake anaotaka wampigie Kura tarehe 26 issue unayoisema haiwezekani na kama ulifikiri hivyo kalagabaho.
 
Sio kazi ya NEC kunadi au kutengeneza Ilani za vyama! Inaelekea hata mikutano ya kampeni hauendi, Mi nachojua kila mgombea atapimwa na wananchi wake anaotaka wampigie Kura tarehe 26 issue unayoisema haiwezekani na kama ulifikiri hivyo kalagabaho.
Tume inataka kuwachagulia watu maneno ya kuongea...ingekuwa vizuri zaidi kama ingeyaandika ikawapa watu
 
haya endelea kurudia,.sina muda wa kupoteza na slow learners

Kijana jibu ni rahisi tu ukisoma Katiba ya nchi yetu Ibara ya 74 (1) utaona kuanzishwa kwa tume na Ibara ya 74 (6) utaona majukumu ya NEC hakuna sehemu imepewa jukumu la kuviandalia vyama hayo maneno unayosema Katiba iko wazi kaisome na uielewe kati ya mimi na wewe itajulikana nani ni slowlearners.No research No right to speak!
 
Vyama vya siasa vyilivyosimamisha wagombea katika siku zilizobaki vinadi sera hakuna namna wananchi wanataka maendeleo.
 
Jamaa alisema atatupa 50m kila kijiji, alinadi maneno hayo akapiga na pushapu, huo ulikuwa ni ushawishi, nitajie kijiji kimepewa huo mpunga!
Vyama vya siasa vyilivyosimamisha wagombea katika siku zilizobaki vinadi sera hakuna namna wananchi wanataka maendeleo.
 
Jamaa alisema atatupa 50m kila kijiji, alinadi maneno hayo akapiga na pushapu, huo ulikuwa ni ushawishi, nitajie kijiji kimepewa huo mpunga!

Kwani utawala wake ni wa muda gani? Na je muda wake umeisha? Kama bado muda wake wa miaka 5 haujaisha tulia utapewa tu na uendelee kushiriki kuchagua viongozi wako.
 
Back
Top Bottom