Mwenyekiti wa Mtaa wa Ziwa Kata ya Butimba Mwanza kupitia CHADEMA ajiuzulu na kuhamia CCM

Kinachonishangaza sio kuhama bali why wote waende ccm tu wakati kuna vyama vingi tu vya kisiasa!
Kingine ni cha mwenyekiti wa mtaa nae kuita vyombo vya habari!!
 
Ahame tu kwa maamuzi yake. Wengine wanamhusu nini? Siku wakiamua kuhama kila mmoja na uamuzi wake.
 
Hana madhara kama ni mwenyekiti ni kama nyoya ling'oke kwenye mwili wa kuku
 
Nilipata shaka aina ya uletaji wako wa hii taarifa, ambayo ilionyesha dhahiri umejaza maneno yako binafsi! Kipande hicho hapo juu, ndio kimenithibitishia shaka yangu!
kama una mashaka na taarifa hiyo..wasiliana na uongozi wa cdm nyamagana au kata ya butimba au diwani wake
 
Pamoja ni kwamba ni takwa la kikatiba (kujiunga na chama cha siasa) kwa kisingizio cha DEMOKRASIA, ila tunahitaji kutafakari zaidi hii hali.
Je ni kweli unahitaji kuhama chama na kujivua nafasi za uwakilishi ili kuunga mkono juhudi za Rais? Juhudi za Rais ni zipi? Kwa kadri ya uelewa wangu, juhudi za Rais ni kutekeleza kwa vitendo mipango /sera za maendeleo bila kujali upo chama gani. Fedha za maendeleo siyo pesa za hisani za Rais ni bajeti ya kitaifa inayopaswa kuelekezwa katika maeneo bila kujali nani ni Mbunge /Diwani/Mwenyekiti wa eneo husika.

Njia pekee ya kumuunga mkono Rais ni kuja na ubunifu wa mipango ya maendeleo dhidi ya wananchi masikini na wanyonge. Ninachokiona katika hii hama hama ni HOFU YA UBAGUZI! Labda Serikali ya CCM inabagua uelekezaji wa maendeleo katika maeneo yaliyo chini ya UPINZANI! Labda wapinzani wanapata hofu ya kutoenekana wamefanya lolote na kukosa cha kuwaambia wapiga kura! Hofu hiyo inawafanya wanyooshe mikono na kuelekea CCM ili kupata UPENDELEO wa kimaendeleo (maendeleo ambayo hata majimbo yaliyo chini ya CCM ni mtihani).

Katika tafakari yangu, wote wanahama kwa hofu ya MADARAKA comes 2020. Wanatafuta upande ambao watahakikishiwa ushindi bila wao kuvuja damu, jasho na machozi. Huwezi kuunga juhudi za Rais kwa kuingiza nchi kwenye gharama za uchaguzi kwa kimvuli cha NDIYO DEMOKRASIA!

Canimito
 
Abeid Ahmed Mussa Mwenyekiti wa Mtaa wa Ziwa Kata ya Butimba kwa tiketi ya chadema amejiuzulu Uenyekiti wa Mtaa na kukihama Chama hicho na kuomba kujiunga na Chama Cha Mapinduzi.

Akiongea na Vyombo vya Habari Leo Tarehe 10.10.2018 Amesema chadema kwa sasa imekosa Dira wala hakuna zaidi ya ubishi ubishi tu lakini hawana nia Ya kushika Dola zaidi ni chama cha watu wachache wenye lengo la kujenga Maisha yao Binafsi tu.
Ameongeza zaidi kuwa Hata Diwani wa Kata ya Butimba Bwana John Pambalu atafuata muda si mrefu na viongozi wengine wa wilaya na kata na kujiunga na ccm.
Pia Amesema Kuna Taarifa za Mnyika na Wabunge wengine wa kutoka kanda ya ziwa wako mbioni kabla ya Desemba.
Ameongeza kuwa Amejivua uanachama wa chadema na kuomba kujiunga na ccm ili kujenga Taifa kwa chama chenye sera na falsafa za kweli na dira.

Source: Katibu wa ccm Kata ya Butimba Bwana Marwa
In politics, there are no permanent friends or enemy.
 
Back
Top Bottom