Mwenyekiti wa MAT atakiwa kuripoti polisi

Hivi ni kweli mahakama haikujua ni nani aliyeitisha mgomo na ni kweli imekosea kutoa maamuzi ya kumkamata mtu asiyehusika? Je ni kweli serikali ipo makini na ina nia ya dhati ya kutatua mgogoro wa madaktari na serikali ambao unaotuumiza zaidi sisi makabwela walipa kodi? Hivi ni kweli watawala wetu pamoja na mihimili yote mitatu vimeshindwa kulitafutia ufumbuzi wa haraka mgogoro huu?
 
kwa kuwa mahakama ''imeshatoa'' uamuzi naona sasa ni ruksa kuliongelea suala hili mjengoni.

Si mjengoni tu, mbona Rais Kikwete yeye ameshaanza kuliongelea suala ambalo lipo mahakamani kabla ya mahakama kutoa uamuzi.

MAhakama ndio walitakiwa waseme kama Madr wana kesi ya kujibu na kuwasimamisha ajira zao, lakini Kiwete akatoa uamuzi yeye, hivyo sheria haituzuii kuongelea jambo lilipo mahakamani.

RUKSAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Hivi kweli hii serikali ina washauri! Kweli it is a sinking ship. Mbona naona kama hapa wana-fuel zaidi tatizo badala ya kulitafutia ufumbuzi? Kwani Ma-Dr wamegoma chini ya MAT! Na Ma-Dr waliogoma ni wangapi ni wanachama wa MAT? Hii serikali inafanya maamuzi utadhani hawana vichwa.
 
Dr.Mkopi Simama imara kama Yesu mbele ya Pilato na Mafarisayo, na kama ni kichwa chako kubali kichukuliwe kama mtume Stefano na Yohana Mbatizaji kwa kukataa dhuluma na unafiki wowote.Watanzania weledi na wajuzi wa mambo ya Tanzania wapo na wewe daima.Wala USIOGOPE hata siku moja.
 
We POLISI lazima uwe updated. Muda wote wa sakata hili hujui nani kaitisha mgomo!? Au mpaka ulishwe mdomoni. MAT si chama cha wafanyakazi na walioitisha mgomo ni wafanyakazi wa hospitali za Umma! Haya meza hiyo, nimeshakutafunia!
Mbona unaanza kumtetea? Hayo unayoyaongea atakwenda kuyaeleza huko mahakamani. Wewe kazi yako ilikuwa kutuhabarisha kwamba mahakama imetoa amri akamatwe, finito.
 
MAT haijawahi itisha mgomo.
na sii kila daktari ni member wa MAT.
sasa uyu mwenyekiti akawashike lukosi madaktari warudishe kazini?
na ivi kumbe kesi ipo mahakamani?mbona rais na MPs walishalitolea tamko?maamuzi ya mahakama ni batili

labda wanasheria mje hapa mtoe ufafanuzi....yani hii nchi ina matahira kwelikweli
 
Ndugu wan JF,
Kuna wakati nafikia hatua ya kuamini kuwa hata mtoto wangu wa darasa la sita anaweza kuwa
raisi wa Tanzania.Manake badala ya wao kuzima moto kwa maji wanakazana kuweka petrol.
Siku ipo tena yaja ambayo hawataamini wanachokiona.Leo wamekalia kiti kinachobonyea na kuzunguka
lakini iko siku watakalia misumari.Take my word!
 
Hivi ni kweli mahakama haikujua ni nani aliyeitisha mgomo na ni kweli imekosea kutoa maamuzi ya kumkamata mtu asiyehusika? Je ni kweli serikali ipo makini na ina nia ya dhati ya kutatua mgogoro wa madaktari na serikali ambao unaotuumiza zaidi sisi makabwela walipa kodi? Hivi ni kweli watawala wetu pamoja na mihimili yote mitatu vimeshindwa kulitafutia ufumbuzi wa haraka mgogoro huu?
Wanafikiri wanauelewa zaidi na wanajificha ndani ya kivuli kinachoingiza jua!
 
Mkopi utashinda katika vita hii,kuna upotoshwaji mkubwa umegubikwa kwenye madai yenu ili ionekane kuwa mnachopigania ninyi ni mshahara mzuri peke yake yale madai yenye maslahi ya watanzania walio wenge kama vile kuboresha mazingira ya kazi na vifaa(vitendea kazi)hayazunguzwi na serikali!

Aluta Continua,mapambano yanaendelea!
 
kwa mujibu wa kiongozi wa MAT, Dr Namala Mkopi anahitajika central police kwa kosa la kukiuka amri ya mahakama.
haya hapa chini ni sehemu ya maneno yake...


my Take;MAT ni chama cha kitaaluma na hakijawahi kuitisha wala kuratibu mgomo.

Chonde chonde asiende peke yake, na asikubali kuhojiwa mahala penye kificho, siwaamini sana polisi.
 
Kuwatisha madaktari na kukamata viongozi wao haisaidii na hata kama wakirejea kazini haitarudisha hali ya utendaji kazi wa madaktari. Ni mbaya na nihatari sana Daktari kufanya kazi kwa kulazimishwa. Serikali ingeangalia ni jinsi gani wangeweza kurudisha mori wa utendaji kazi wa madaktari na kwa upande wangu wakubali kurudi kwenye meza ya mazungumzo ili kufikia muafaka na si vinginevyo.
 
Nchi ya wasomi chakulaa cha wanasiasa; hiyo salam ya mahakama kwa walim
 
Awe makini asikubali kula kitu chochote pale polisi. Mapambano yanaendelea bana
 
We POLISI lazima uwe updated. Muda wote wa sakata hili hujui nani kaitisha mgomo!? Au mpaka ulishwe mdomoni. MAT si chama cha wafanyakazi na walioitisha mgomo ni wafanyakazi wa hospitali za Umma! Haya meza hiyo, nimeshakutafunia!

Sawa. Aende akaileze hivyo mahakama. Nadhani hiyo ndo njia nzuri ya kupata ukweli
 
Inaonyesha udhaifu wao ni mkubwa kiasi cha kushindwa kuelewa mbinu iliyotumika kuitisha mgomo? MAT has nevr been into the game, how comes wanalazimishwa kuamuru mgomo uishe?
 
Siku rais kikwete atakapokabidhi ikulu kwa Rais mwingine wa awamu ya tano (hata kama siyo CHADEMA) nitafurahi sana. Nitamshukuru Mungu sana, nitatoa sadaka ya shukrani kanisani. Naona kama sumaye amekuwa nabii wa Kweli vile!!!!!.
 
Back
Top Bottom