Mwenyekiti wa kijiji (CDM) Kigarama anaharibu hadhi ya Chama...Kashfa kibao wananchi hawana mbadala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenyekiti wa kijiji (CDM) Kigarama anaharibu hadhi ya Chama...Kashfa kibao wananchi hawana mbadala

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ta Muganyizi, Jun 26, 2012.

 1. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #1
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Wanakijiji cha Kigarama kata ya Kanyigo wilaya ya Missenyi mkoa wa Kagera Bw. Ijumba ni mtu ambaye anawakatisha wananchi waliomchagua kwa kuwa na vituko vingi vya ajabu kiasi cha kukatisha tamaa wananchi wake. Baada ya kuwahoji ni kuwa kwa sasa akigombea tena hapati kura hata moja. Wakasema walimchagua pamoja na mapungufu yake wakitarajia atajirekebisha maana hawaipendi CCm kiasi kwamba hata angesimama chizi kwa tiketi ya CDM angeshinda mana hawaipendi CCM. Lakini mwenyekiti huyu anawakatisha tamaa wananchi na kufikia hatua ya kutaka kujua kama kuna utaratibu wa kumuondoa na kufanya uchaguzi mpya.

  Mwenyekiti huyu amesharipotiwa mara mbili na redio Karagwe kwa kosa moja la aibu ambalo kulitaja naona aibu. Chanzo kikubwa cha kurukwa na akili ilikuwa ni pombe lakini baada ya kelele nyingi kutoka kwa viongozi wa kijiji wakiwemo madiwani...........akaaacha pombe na akatangza kuokoka............lakini kwa sasa kuanzia asubuhi..........ameweka Viroba na Nkonyagi ya asili ya Kagera.

  Basi akinywa ni matatizo matupu. Wadau wengi wa maendeleo wanapoenda kijijini kwake hataki kutoa ushirikiano mpaka apewe posho. Akinyimwa anaondoka. Mfano Shirika moja mkoani hapo lilikwenda kutoa huduma ya watu kupima virusi kwa hiari lakini alisema ili aweze kushiriki kikamilifu inabidi apewe posho. Hii iliniudhi sana na matokeo yake mashirika yataanza kuiruka kata hiyo katika suala la maendeleo sababu ya kiongozi huyu.

  Wana CDM pamoja na kuwa tuko kwenye mapambano ya Ukombozi..........tusikae kimya kwa wale ambao wanaanza kukichafua chama na kuwa na mifano ya ajabu. Inapofikia wanakijiji wanasema hawana jinsi na wanashindwa wafanyeje ili wapate kiongozi mwingine. Wana CCM wanatumia nafasi hiyo kwa kuwaambia wanakijiji kuwa Upinzani ni ngumu kuwa na kiongozi mwadilifu. Hii inaniudhi sana. Wakikanusha kauli hiyo wanaambiwa "muoneni mwenyekiti wenu" hii inakuwa mbaya sana.

  Pendekezo langu : Viongozi wa CDM wilaya au mkoa waingilie kati hali hii. Wakawasilikilize wananchi wa kjiji hiki maana wao wanasema wana kura za CDM mkononi kuanzia Kijiji, Udiwani, Ubunge na Urais ...lakini wanakatishwa tamaa na baadhi ya viongozi hawa. Ni aibu.........CDM jitahidini hadhi ya chama isiendelee kushuka.
   
 2. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #2
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Kuna baadhi ya wana CDM tunapokuwa tunaweka wazi matatizo yaliyoko vijijini kwetu kuhusu viongozi wetu kwa tiketi ya chama chetu CDM na kuwaomba viongozi wetu ngazi ya wilaya yetu au mkoa wetu wao wanaconclude kuwa " Magamba at work" ili issue ionekane ni mzaha isitiliwe maanani. Nimegundua ni magamba wenyewe ndo wenye comment hizo.
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Huyo mwenyekiti kama kweli hiyo ndiyo tabia yake, anafaa sana kuwa kiongozi wa Chama Cha Mapenzi (CCM)
   
 4. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  tuwe wavumilivu, wenyeviti wengi wa vijiji kupitia CHADEMA ni watu waliojivua gamba, hivyo sumu bado haijaisha.
   
 5. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Wanaoharibu ni wengi maana wengine walichaguliwa kwa kura za hasira dhidi ya CCM mfano tosha ni DIWANI WA KATA YA KIRANYI
   
 6. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #6
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Kaka huyu kazidi kidogo nitoe machozi niko tayari kutoa namba za baadhi ya wananchi muwahoji
   
 7. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  Asante, hiyo ni taarifa mbivu kwa ajili ya hatua stahiki kuchukuliwa. Ni udhaifu kwa chama na ni wajibu wa CDM kutopuuza hili.
   
 8. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Kwani nguvu ya UMA mwisho wake ni kuiondoa CCM tu, waambie hao wananchi wamtilie timu na kumshurutisha kuacha pombe na kumpatia list ya items za kuzifanyia kazi. wote waandamane kwenda kwake asubuhi kabla hajanywa hayo mapombe yake.

  Kama ameshindwa kuwaongoza wamuongoze wao hii ndio DHANA YA NGUVU YA UMA, Wakibweteka na mtu kujiita mwana chadema watachemsha, CHADEMA WAUONGO WAMEKWISHA KUWA WENGI SANA.
   
 9. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Naungana nawe, nami nimekutana na wenyeviti 2, wenye matatizo; na mbaya zaidi wanapinga kila kitu bila msingi. Mmoja wa huku Kigoma ilibidi niongee na Katibu wa chama. Mwingine ilibidi nikiuke masharti ya kazi, nimuite pembeni na kumuonesha kadi yangu ya chama ili at least anielewe.
  Mimi naona tunahitaji kuwajenga sana ili wailewe vision ya chama na mipango.

  Magamba wanafurahia sana wanapoharibu. Imagine mwenyekiti anawaambia watu wavue vitoto vya samaki na makokoro.
   
 10. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #10
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Inabidi Viongozi wa wilaya watie timu kule..........kiongozi na kama kachanganyikiwa wakati wavijiji wanazidi.......kujiunga na CDM. Leo kulikuwa na Uchaguzi wa wenyeviti wa wazazai wa CCM ngazi ya kata wilaya ya BUkoba Vijijini maeneo ya Bugabo, Kaagya, Lubafu...........lakini ilikuwa ni aibu watu ni wachahce na wanajitokeza baadhi ya wazee tu. Hii ni aibu. Kata ya Lubafu nzima kulikuwa na wajumbe 12 tu. hakuna hata kijana mmoja aliyeonekana pale.
   
 11. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #11
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Mkuu kiranyi Iko wapi ili hawa viongozi wa CDM wachukue list ya hayo maeneo na Katika movement zinazoendelea awepo kiongozi mmojawapo wa kupita anarekebisha hii badala ya kuacha uozo uendeleeee. Tukiacha ujinga kama huu kuendelea na kushindwa kudhibiti uzembe ngazi ya kijiji ni ngumu wananchi kutuamini na kutupa dhamana kubwa kama halmashauri na nchi kwa ujumla. Tukiwa serious chini........tutajenga kuta imara za kusimamishia ghorofa zaidi ya hapo tutazoeleka na kuonekana hatuna tofauti na magamba. Tusiwe Lazier affair es kama CCM'
   
 12. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #12
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  NADHANI TUSIANZE DHARAU KAMA ZA ccm
   
 13. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #13
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,742
  Trophy Points: 280
  Hilo litafanyiwa kazi,vizuri ni kwamba viongozi wetu hupita humu wataliona.
   
 14. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #14
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Mpigie simu Lwakatale aiseee
   
Loading...