Mwenyekiti wa Kijiji ampa raia adhabu kwa saa mbili hadi ujauzito kuharibika

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,141
2,000
Asha Rajabu(28) mkazi wa kijiji cha Samanga Marangu wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, amesimulia namna alivyorukishwa kichurachura na mwenyekiti wa kijiji hicho, kwa madai ya kuchelewa kufunga baa na kusababisha ujauzito wake wa miezi miwili kuharibika.

Mwenyekiti huyo, Wilfredy Minja kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo, kwa tuhuma ya kumsababishia Asha mateso na kupoteza ujauzito.

Akizungumza na gazeti hili, Asha alieleza kuwa kwa zaidi ya miaka mitano, amekuwa akisumbuka kutafuta ujauzito bila mafanikio mpaka hapo alipobahatika kuupata ujauzito huo, lakini baada ya kupata masaibu hayo, furaha yake imemtumbukia nyongo.

Chanzo: Mwananchi
 

njofu

Member
Jul 29, 2012
65
95
Nipe pole Sana mhusika. Nashauri huyu Dada apelekwe kwa wataalam WA uzazi waangalie vizurimasaibu aliyoipata

2. Mwenyekiti huyo nimesikia amekomesha uvunjifu wa Amani toka alipochaguliwa hivyo wasiompenda Wana tumia mwanya huo.
3. Kwa kuwa vyombo vya usalama vipo tuvipe muda hatimaye sheria itachukua mkondo wake.
4. Taarifa hizi zimekwenda karibu vyombo vyote vya habari vilivyoko kilimanjaro Arusha n.k.
 

Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
40,312
2,000
Mwenyekiti wa CCM, serikali za mitaa ni CCM, diwani wa CCM, mbunge wa CCM, polisi wa CCM. wanamtesa raia hakikaa itoke mitano hadi saba au hata mia moja.
 

McMahoon

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
1,316
2,000
Kuna sheria gani inayosema, mtu akichelewa kufunga bar arukishwe kichura? Awamu hii kila mwenye cheo anataka ajioneshe na yy ni nani.
Ujinga sana. Sheria zipo na zinaeleweka. Balozi au mwenyekiti anirukishe kichura? Atajuta siku hiyo. Watu hawajui sheria ndiyo maana wanafanyiwa vyovyote vile.
Nipe pole Sana mhusika. Nashauri huyu Dada apelekwe kwa wataalam WA uzazi waangalie vizurimasaibu aliyoipata
2.mwenyekiti huyo nimesikia amekomesha uvunjifu wa Amani toka alipochaguliwa hivyo wasiompenda Wana tumia mwanya huo.
3.kwa kuwa vyombo vya usalama vipo tuvipe muda hatimaye sheria itachukua mkondo wake.
4.taarifa hizi zimekwenda karibu vyombo vyote vya habari vilivyoko kilimanjaro Arusha n.k.
 

Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
11,402
2,000
Hawa wenyeviti wa mitaa wa CCM wakulazimisha ni shida sana kwa wananchi.
 

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
17,182
2,000
Nipe pole Sana mhusika. Nashauri huyu Dada apelekwe kwa wataalam WA uzazi waangalie vizurimasaibu aliyoipata
2.mwenyekiti huyo nimesikia amekomesha uvunjifu wa Amani toka alipochaguliwa hivyo wasiompenda Wana tumia mwanya huo.
3.kwa kuwa vyombo vya usalama vipo tuvipe muda hatimaye sheria itachukua mkondo wake.
4.taarifa hizi zimekwenda karibu vyombo vyote vya habari vilivyoko kilimanjaro Arusha n.k.
Umeandika kijingaaa sana na kujaribu kutengeneza mazingira ya KiCCM CCM.

Huenda huyu mama alikua na Cervical incompetence ,nahivo mazoezi au kazi yoyote yanayozalisha Presha kwa tumbo lazima itapelekea ujauzito kuchoropoka.

Swali ni je, Mama alimwambia mwenyekiti kua anaujauzito??? Mwenyekiti akafanya nn??? .

Kivyovyote vile, MWENYEKITI LAZIMA AWAJIBIKE KWA KWA MATESO NA MUMIVU,NA KUHARIBIKA KWA MIMBA ALOMSABABISHIA HUYU MAMA.

HAYA NI MATOKEO YA SERIKALI YA CCM INAYOONGOZWA NA JOHN POMBE MAGUFULI MSUKUMA AMBAYO KILA KIONGOZI ANAWEZA TOA ADHABU,NA VIPIGO KWA RAIA.
 

njofu

Member
Jul 29, 2012
65
95
Kitu mhimu huyo mama apelekwe kwa wataalam wa uzazi isije kwenda hospital ya kilema ikawa kisingizio. Tusihukumu bila kujua chanzo. Je m/kilikuwa mwenyewe au Kuna ushabiki wa Aina fulani
 

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
17,182
2,000
ipimwe kwanza na hicho kipimo kithibitishe kuwa ilitoka kwa kuruka chura haikutoka yenyewe au hakuitoa
Unaona sasa, hizi ndo akili za CCM

Mnakazi sana

Ndo mnazitumia kuendesha familia na changamoto zake??? Au hizi hiwa zinaishia humuhum???
 

njaakalihatari

JF-Expert Member
Feb 12, 2019
1,213
2,000
wanaiga yanayofanyika juu kupiga watu vibao kudhalilisha kwa lugha z a matusi,kuchapa watu viboko ni vurugu kil akona
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom