Mwenyekiti wa kamati ya madaktari atishiwa usalama wake

Mungu akusaidie kwa ajili ya ustawi wa watanzania wote. Walala hoi wote wenye mawazo chanya wako nawe. Leo makanisani tutakuombea Mungu akuponye dhidi ya vitisho hivyo.
 
Katika jambo kama hili vitisho lazima mvitegemee.Cha msingi jipangeni vizuri..

Hivyo ni vitisho tu kwani hali ilivyofika sasa hawawezi kumfanya chochote labda baadae wajekupiga chini kama walivyofanya kwa mkurugenzi wa TBC
 
Nilichangia kwenye thread nyingine kuwa hili lingetokea kwa kuwa ni serikali legelege. Ni sawa kabisa kupigana na mtu mwoga, atakutisha kwa kila hali na wewe utadhani anamaanisha kweli kumbe ukimstua tu atakimbia na kujamba hovyo.

Dr Ulimboka wewe ni jemadari mkuu tuongoze baba uasiwmwoga. Kumbuka hata Idd Amin alitisha sana hata,Gadaffi au Sadam Husein kiasi kwamba hawakufanya resistance yoyote.

Safari hii wametumia sms kesho watakuja na kila aina ya silaha we subiri tu uone, lakini hawana lolote. Lakini kaeni sawa mwoga anaweza akakuangushia pigo akakutoa roho.

Nani duniani ameona serikali kama hii?

Ndo itakuwa serikali ya kwanza duniani na haitokaa itokee tena
 
Hawa mafisadi Mi nawachukia mpk hata ardhi ninayoikanyaga ni shahidi!

Hila na njama zao zitakwama tu!

Wapuuzi wakubwa kabisa!

Ukizingatia hawa ndo serikali yetu iliwasomesha mpaka chuo bure badala yake wakuwa siyo wazalendo kwakuendekeza ufisadi, sasa wanategemea kizazi cha sasa kinachojisomesha kitakuwa je pindi kitakapokuja kushilia dola?
 
Hivi jk angehairisha hiyo safari na kutoa hiyo hela alotumia kwenda kwa madaktari tatizo lingekuwa lishaisha
 
Back
Top Bottom