Mwenyekiti wa kamati ya madaktari atishiwa usalama wake

Kutishiwa ni kawaida jamani.
Ukiona matishio yanakuja ujue ndo mwanzo wa ushindi.
Swala la mgomo wa ma dr linatisha lkn naona serekali inaona mzaha.

Nashindwa kuelewa maamuzi ya posho za wabunge yalikuwa ni chap chap lkn madai ya msingi ya ma dr yanahitaji muda kujadili
 
Huyu jamaa tangu 2005/2006 alipoongoza mgomo ule..alifuatiliwa sana, nyumbani kwao river side wazazi wake walipata taabu kweli kweli..but alikaza buti, I know him well ana moyo wa 'Kikurya'. Mambo yatanyooka tu. Kila lakheri kaka Mboka..!
 
Vitisho ndiyo vinaonyesha kuwa ujumbe wa mgomo umefika!tofauti na hapo ningeona kuwa bado somo halijaeleweka kwa serikali,baada ya hili linaanza na la kima cha chini kuwa laki 5,ningeomba mchumi wa serikali atupigie hesabu jinsi mtu anavyoweza kumaliza mwezi na sh 200000 za sasa,hata hiyo laki tano haitoshi!!!

Kitu kingine kinachonishangaza ni watu kukurupuka na kusema kuwa madaktari wanataka sh mil 3.5 na posho ya laki 2 nadhani hawa ni wale walio kwenye kampeni ili madaktari waonekana wabaya,lakini nashindwa kuelewa kama kweli hawa watu wapo tanzania kwani wanatumia mbinu ya zamani kweli,wananchi wameshawaelewa sana kilichobaki bado ni ile kauli kuwa ccm eti ndiyo inaleta amani bila ccm hakuna amani,bado hapa uelewa unasuasua.

Kwa mujibu wa taarifa ilivyoandikwa kwenya gazeti,kauli ya mil 3.5 na laki 2 ilitolewa na kigwangala ambapo ilipingwa na madaktari kusema wanataka elfu 40 tu na mshahara watakaa na serikali kukokotoa,huu umbea unaozidi kuenea wa mil 3.5 sijui unatoka wapi!!!!
 
Huu mgomo unaorganaiziwa na vyama vya upinzani! Majibu mepesi ya akina Nnape
 
Wasikubali kuwa kama akina Mgaya wa TUCTA na Mkoba wa Walimu..walipotishiwa na JK wakafyata mkia...alunta continua!!

Hawa jamaa walinikera sana wala sitaki kuwasikia majuzi mgaya alienda kwa madaktari kuwaomba warudi kazini wakamgomea na kesho yake akaibuka na singo ya laki 5 wakati ya laki 3 bado haijauzika!!!!
 
Hawa viongozi wetu kufanya kitendo kama hicho ni kawaida sana. Kipindi flani kukiwa na mgomo chuoni walimtishia aliyekuwa rais wetu asitishe mgomo.
 
Source ni Dkt Stephen Ulimboka mwenyewe ambaye pia alisema kuwa hivi ni baadhi ya vitisho tu ambavyo anavipata kwani pia amekuwa akipata simu za vitisho kupitia namba za ajabu ambazo hata ukijaribu kuzipi hazipatikani hewani .

lakini pia alitoa rai kwa madaktari wenzake kuwa yeye yupo tayari kufa kwa ajili ya kutetea masuala haya ambayo anaamini kuwa ni ya msingi na ya haki kwa watanzania na hata kama yeye hatakuwapo siku jumatatu ya tarehe 30/01/2012 ambayo ni siku ya kikao kingine ambacho kitahusisha wajumbe toka mikoani anaamini madaktaari hawatachoka kuendelea na haya mapambano ambayo yameanza kwani kama yatashindwa itachukua miaka mingi hadi kuweza kuboresha sekta ya afya tena

Hapo kwenye red; hebu hili suala lihojiwe kwa ukaribu na umakini zaidi. Pamoja na kuwepo kwa chombo kinachodhibiti mawasiliano nchini (TCRA) bado upuuzi huu unaendelea. Nakumbuka "namba za ajabu" zilitumika sana wakati wa uchaguzi mkuu 2010 kwa maslahi ya kisiasa hasa maslahi yaliyo kinyume na sheria, taratibu, na hata maadili ya uchaguzi lakini hatujasikia hatua zozote zikichukuliwa!

Hizi namba za ajabu zinatoka wapi wakati line zote za simu nchini zimesajiliwa na wamiliki wake wanafahamika? Kama TCRA imeshindwa kazi ni wakati muafaka sasa kwa uongozi kuwajibika badala ya kung'ang'ania ofisi na ikizingatiwa ni miongoni mwa taasisi za umma zisizo na rekodi nzuri ya matumizi ya resources za umma ikiwemo ufisadi.

Waziri Kivuli wa Mawasiliano, tunahitaji kuona Waziri husika akitoa maelezo yaliyojitosheleza kuhusiana na "namba za ajabu". Otherwise, TCRA kwa kushirikiana na NEC na UWT ndio wavurugaji namba moja wa mustakabali wa taifa letu. Sijui tutakapoanza kupiga kura kupitia mtandao ilhali hawa jamaa (TCRA) ndio wadhibiti wakuu wa mawasiliano na kwa mtindo sijui itakuwaje? Ni wakati muafaka sasa kuanza kuisafisha hii nyumba iitwayo TCRA!
 
Hapo kwenye red; hebu hili suala lihojiwe kwa ukaribu na umakini zaidi. Pamoja na kuwepo kwa chombo kinachodhibiti mawasiliano nchini (TCRA) bado upuuzi huu unaendelea. Nakumbuka "namba za ajabu" zilitumika sana wakati wa uchaguzi mkuu 2010 kwa maslahi ya kisiasa hasa maslahi yaliyo kinyume na sheria, taratibu, na hata maadili ya uchaguzi lakini hatujasikia hatua zozote zikichukuliwa!

Hizi namba za ajabu zinatoka wapi wakati line zote za simu nchini zimesajiliwa na wamiliki wake wanafahamika? Kama TCRA imeshindwa kazi ni wakati muafaka sasa kwa uongozi kuwajibika badala ya kung'ang'ania ofisi na ikizingatiwa ni miongoni mwa taasisi za umma zisizo na rekodi nzuri ya matumizi ya resources za umma ikiwemo ufisadi.

Waziri Kivuli wa Mawasiliano, tunahitaji kuona Waziri husika akitoa maelezo yaliyojitosheleza kuhusiana na "namba za ajabu". Otherwise, TCRA kwa kushirikiana na NEC na UWT ndio wavurugaji namba moja wa mustakabali wa taifa letu. Sijui tutakapoanza kupiga kura kupitia mtandao ilhali hawa jamaa (TCRA) ndio wadhibiti wakuu wa mawasiliano na kwa mtindo sijui itakuwaje? Ni wakati muafaka sasa kuanza kuisafisha hii nyumba iitwayo TCRA!

Mkuu Nakuunga mkono, mimi ninavyojua hizi namba za ajabuajabu zinaweza kuwa traced kupitia mitandao yetu ya hapa ndani . Nahofia TTCL kunaweza kukawa na hii service ya kubadilisha source address na kuionyesha kwa receiver ikiwa tofauti na original. Nakumbuka TCRA ilitoagizo mitandao yote iondoe ufichaji wa calling line identification na mitandao yote ilitekeleza lakini sijui TTCL maana ni wa serikali Lazima wawe na hizi service kwa ajili ya UWT na kazi yake ndo kama hii kutishia watu. Nadhani wameona maji ni marefu ndo maana wanatishia kwa msg. Kimsingi UWT kama kweli wanaona wako sahihi hawana haja ya kumtaarifu mharifu wao badala ya kutekeleza tu maamuzi yao kimyakimya.

Ngoja tusubili tuone nasikia pia katibu wa ccm huko Tanga naye kapiga simu kutishia. Huyu si watapambana naye madaktari wa huko tanga?
 
huu mgomo wa ma-Daktari unanidhiirishia kuwa Tanzania hatuna sheria madhubuti. Sheria ya Kazi(Ajira na Mahusiano Kazini No.6 ya 2004) inawatambua Ma-daktari kama wafanyakazi wa kazi muhimu(essential service) hivyo awatakiwi kugoma na hata ikitokea kuna mazingira ya kugoma basi si wote watakao goma, baadhi wataendelea na kazi huku wenzio wakifatalia mambo yao kwa ujumla wao( Ref. Kanuni-Code of good practice and conduct ,2007).

Kwa maana nyingine Serikali inabidi iwatambue ma-Daktari kwamba inapotokea ishu inayo husu maslai yao kwa haraka sana inabidi itatuliwe bila hata kupoteza siku, vinginevyo Tanzania tutaendelea kuwa na sheria zisizo na meno.

Hii ishu ya Ma-daktari jinsi ilivyo si ya kutatuliwa kisiasa bali ni ya kitaalamu na kisheria zaidi. tunayo Tume ya Usuluhishi na Uamuzi-CMA maalumu kwa ajiri ya kushughulikia migogoro ya kazi, kwanini aishirikishwi katika swala hili muhimu badala yake wanasiasa wanachezea haki za watu.

Kama pengine wenye mamlaka hawajui utaratibu wa kui-handle ni bora ku-declear ili wanazuoni wajitokeze wawasaidie kuliko kuanza kutoa Vitisho baada ya kuona wamelemewa, Tanzania siyo Iraqi wala Iran.
 
hii serikali ya chama cha magamba-ccm hakika ni serikali ya wendawazimu,vichaa na majuha!

Hivi hawa jamaa bado wanafikiri watu bado wako karne za ujima za kutishana na ndiyo mzee!!!????
Badala ya ku-address serious issues kama hii ya mgomo wa madaktari wanaanza kutoa vitisho kweli? Nimeshasema several times kwenye ukumbi huu kuwa rais kiwete hana waziri mkuu na hana baraza la mawaziri. Inasikitisha kwamba hata rais mwenyewe anaonekana hajui maana ya kuongoza.
Ni aibu tena ni fedheha kwa mkuu wa nchi kukimbilia ughaibuni(davos-uswiss) kwenye mkutano wa wef huku akiacha mgomo unafukuta na watanzania wanakufa!!!! Yaonyesha tu kuwa kiwete hathamini uhai na utu wa watanzania. Ameondoka na shazi la watu 14 kwa gharama ya 300m tshs fedha ya kitanzania kwenda kutalii na kutumbua fedha ya walipa kodi hela ambayo kwa rais makini angeliweza kuahirisha na kuwapoza madaktari kama kianzio kwa madai yao ambayo ni halali kabisa!

Hii inadhihirisha tu kuwa tanzania kwa sasa haina rais,haina pm,haina mawaziri na haina chama kinachoongoza. Pengine mimi niseme tu kwamba hii ni indicator nzuri sana ya kuwaonyesha watanzania kuwa ccm na serikali yake
wamechoka na wanatakiwa waondoke ikulu haraka sana ili chama kingine makini chenye kujali maslahi ya watanzania kichukue madaraka. Chama hicho si kingine isipokuwa chadema,the peoples poweeeeeeeeeeeeeeeeer!

madaktari na wataalamu wenzangu muwe makini sana hasa mtakapokutana na pm. Pm ni mzuri sana waku-sympathise na watu na anaweza kabisa akafanya mabadiliko ktk stahiki zenu. Tabu niionayo baada ya mkutano wenu ni;
1. Unaweza mkakuta wengi wenu ama baadhi yenu mkaambiwa taaluma zenu hazitambuliki kwani zina utata katika matokeo yenu. Kama si hilo
2. Kama mmeajiliwa serikalini mtapokea barua za kuachishwa kazi yenye tarehe ya tangu mgomo/haraati/extended meeting ilipoanza.
Nasema hivi kwani kuna mahala aliitwa katka taasisi mpya ya elimu na kubwa kwa maana ya wingi wa wanachuo na akafanikisha baadhi ya mambo muhimi. Lingine ambalo ni mzizi wa matatizo hayo alisema atashauriana na rais hadi leo mzizi huo upo matokeo yake sasa watu wanafukuzwa kazi katika matatizo ambayo msingi wako ni manuva au kupika tatizo la mfanyakazi huyo. Wengine wamefukuzwa kazi kabla ya kikao chakuidhinisha kufukuzwa ama kutofukuzwa kazi na tarehe ya barua inaonesha hivyo.
3. Kama mlivyokwisha azimia kuwa baadhi ya maafsa wa wizara ya afya ndo tatizo na kuwa waondoshwe komalieni mkiwa nae pm atamke hapo mbele yenu na mbele ya maafsa hao kuwa wanaenda wizara gani ama watapangiwa kazi nyingne, mkikosea kwa kuridhika na majibu ya pm mkasahau msingi wa matatizo juhudi zenu hizi na extended meeting yenu itakuwa karibu na sifuri
 
Wakati tunasubiria kwa hamu mkutano wa madaktari wagomaji na Waziri Mkuu Pinda baadae leo, ningependa wale wote mnaounga mkono mgomo huu wa madaktari mzingatie haya

masaburi at work,mambo ulizungumzi huu ni upotoshaji wa mambo ya msingi kuhusu haki za madktari
 
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa naye anahusika vipi na masuala ya madaktari kama si dharau.
 
Back
Top Bottom