Mwenyekiti wa Halmashauri Singida Vijijini, Mbunge, DED wapinga maamuzi ya Waziri kuwapelekea Hospitali

mchangamadini

Member
Jun 1, 2017
59
28
Hili ni ajabu la kumi duniani.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Singida Vijijini ambaye pia ni kibaraka mkubwa wa Lazaro Nyalandu, mbunge Monko, DED Rashid Mandoa, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri, Omari Ng'ombe pamoja na Diwani Munyawi Hinga wa Ikhanoda na wa Merya Idd wameondoka leo hapa Singida kuelekea Dodoma kuonana na Waziri Mkuu na Waziri wa Tamisemi kwenda kupinga hatua ya Serikali kutenga fedha kwa ajili ya kujenga hospitali ya Wilaya katika mji wa Ilongero.

Wanafanya hivi kwa sababu ya chuki zao binafsi za mgogoro waliouunda wa wapi ijengwe makao makuu ya wilaya

Wanakula utumbo wao kwa kuwanyima wananchi haki ya kupata huduma za afya. Watu wa aina hii ni wa kulaaniwa na kuogopwa kama ukoma, mnakataaje hospitali na nyie ni viongozi?

Mnampingaje waziri na Rais aliyeamua kuwasaidia wananchi? Mbunge Monko ameapa bora akose ubunge lakini atahakikisha makao makuu yanajengwa kwao.

My take. Hii ni hujuma kwa wananchi.
 
Tatizo Ilongero imedumaa ,haikui na haifai kuwa makao makuu ya Wilaya. Mmejaa uswahili na ushirikina tu

Mbona Merya ni karibu tu?

Wenzenu wa Ikungi hatukuona tija ya kugombea location ya makao makuu na tunasonga mbele

Nakushauri uache huo ujinga.
Hao uliowataja woote hawawezi kuakisi hoja yako ila wanakubalika zaidi kimantiki
 
Swala wanagombana mbele ya chui mwenye njaa, waache wagombane ili chui apate mlo kwa urahisi
 
Hii ni taarifa Au utungo wa kipande cha nyimbo yako mpya ya Taarab??
 
Cool down! Don't attack personalities.
Hiyo Singida siijui vizuri, achilia mbali Ilongero.
Kwa jinsi ulivyoshibdwa kujenga hoja, (discordination ya tittle na content) nawatakia hao viongozi kila la heri.
 
Hili ni ajabu la kumi duniani. Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Singida vijijini ambaye pia ni kibaraka mkubwa wa lazaro Nyalandu, mbunge Monko, DED Rashid Mandoa, makam mwenyekiti halmashauri omari ng'ombe pamoja na diwani mlevi sana munyawi hinga wa ikhanoda na wa merya idd wameondoka leo hapa singida kuelekea dodoma kuonana na waziri mkuu na waziri wa tamisemi kwenda kupinga hatua ya serikali kutenga fedha kwa ajili ya kujenga hospitali ya wilaya katika mji wa ilongero. Wanafanya hivi kwa sababu ya chuki zao binafsi za mgogoro waliouunda wa wapi ijengwe makao makuu ya wilaya...wanakula utumbo wao kwa kuwanyima wananchi haki ya kupata huduma za afya. Watu wa aina hii ni wa kulaaniwa na kuogopwa kama ukoma, mnakataaje hospitali na nyie ni viongozi? Mnampingaje waziri na Rais aliyeamua kuwasaidia wananchi? Mbunge Monko ameapa bora akose ubunge lakini atahakikisha makao makuu yanajengwa kwao.
My take. Hii ni hujuma kwa wananchi.
Mmmh.... nafikili hoja ni mabishano wa sehemu gani hiyo hospital ijengwe na sio hao watu kukataa kujengewa hospital. ( kama kwl hawataki hospital basi ni watu wa ajabu sana) .

Nadhani wana sababu zao za kukataa na ww una zako za kutaka hospital ijengwe hapo unapopenda, hilo sasa ni lenu hatutaki kujua kwa maana ''nyie ni wafu acha mzikane wenyewe kwa wenyewe".

My take: siku nyingine ukiwa na lengo la kutuletea thread yako jaribu kutulia, ndipo uandike sio ukurupuke kama hivi.
 
1.5 Trillion zingetosha kumaliza huo mgogoro na kuwajengea hospital sehemu zote mbili
 
Mnaokejeli taarifa hii pingeni kwa vielelezo. Singida watu tunateseka kwa kukosa huduma mbalimbali leo tumeletewa hospitali Eti Elia digha na mkurugenzi wanashirikiana wanatumia kodi zetu kwenda kuloga kwa serikali sisi tusipate huduma bora za afya kwa maslahi ya matumbo yao
 
Tatizo Ilongero imedumaa ,haikui na haifai kuwa makao makuu ya Wilaya. Mmejaa uswahili na ushirikina tu

Mbona Merya ni karibu tu?

Wenzenu wa Ikungi hatukuona tija ya kugombea location ya makao makuu na tunasonga mbele

Nakushauri uache huo ujinga.
Hao uliowataja woote hawawezi kuakisi hoja yako ila wanakubalika zaidi kimantiki
Imedumaa? Basi wewe una matege ya macho km sio ya ubongo, kwa hiyo unakubaliana na hawa wanaopinga tuletewe hospitali?
 
Mmmh.... nafikili hoja ni mabishano wa sehemu gani hiyo hospital ijengwe na sio hao watu kukataa kujengewa hospital. ( kama kwl hawataki hospital basi ni watu wa ajabu sana) .

Nadhani wana sababu zao za kukataa na ww una zako za kutaka hospital ijengwe hapo unapopenda, hilo sasa ni lenu hatutaki kujua kwa maana ''nyie ni wafu acha mzikane wenyewe kwa wenyewe".

My take: siku nyingine ukiwa na lengo la kutuletea thread yako jaribu kutulia, ndipo uandike sio ukurupuke kama hivi.
Na wewe ni kibaraka wao unapinga wilaya kupata hospitali ya kisasa
 
Back
Top Bottom