Mwenyekiti wa halmashauri Geita ajiuzuru

Mulangila Mukuru

JF-Expert Member
Feb 24, 2010
1,945
724
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Geita Nd.Msukuma leo ametangaza kujiuzuru uenyekiti wa Halmashauri pamoja na udiwani kwa tiketi ya CCM baada ya kuwa kwenye mgogoro na madiwani wenzake wa magamba kwa muda sasa.

Source: ni habari toka ukumbi wa halmashauri.

======
Ukweli ni kuwa ameng'olewa na Madiwani wa chama chake kutokana na kuwa na Mgogoro wa muda mrefu, kambi mbili zilikuwa zikishindana.

Toka alipoingia kushinda udiwani alikuwa akipambana na wenzake na leo wamefanikiwa kumg'oa. Japo alitamka kuachia na UDIWANI taarifa za sasa usiku nimeambiwa kuwa amekanusha kuachia na udiwani.
 
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Geita Nd.Msukuma leo ametangaza kujiuzuru uenyekiti wa Halmashauri pamoja na udiwani kwa tiketi ya CCM baada ya kuwa kwenye mgogoro na madiwani wenzake wa magamba kwa muda sasa.

source,ni habari toka ukumbi wa halmashauri.

Itakuwa walimshtukia ana mahusiano na magwanda.
 
CCM na wapenda haki ni mbali mbali. Tunamkaribisha kwenye mapambano ya kudai ukombozi wa kweli wa nchi hii. Kabla ya kujiunga akafanyiwe assessment kujua kwamba siyo Shibuda style.
 
Mafilili karibu uwanjani, natamani mwita25 aokoe jahazi. Sikubaliani kabisa na kujiuzulu kwake, mchozi unanitoka na kububujika, hapana nasema hapana!
 
Mnamkaribisha kwenu, kwani munajua chanzo cha mgogoro? Hebu shughulisheni akili kidogo kugundua tatizo nini kabla ya kumkaribisha? Mbona Mh. Rostamu hamjamkaribisha au yeye alijivua gamba na huyu mwenyekiti amejivua shati?
 
Kuna makapi mengine unaweza kuambulia hata punje moja lakini type ya RA mhhhh.
 
Halafu wakati wa kampeni atapanda jukwaani pamoja na mgombea wa CCM
 
Habari za kutoka Geita zinadai kuwa mwenyekiti alikuwa anahoji matumizi ya pesa ambazo zinatolewa GGM (Mgodi wa geita) kusaidia maendeleo ya wilaya ya geita.

Pamoja na fedha lukuki zitolewazo hakuna maendeleo ambayo mtu anaweza kuonyesha wapi hizo fedha zimefanya kazi. Maana nasikia alienda kuonana na uongozi wa mgodi kuhoji nivipi wanasaidia maendeleo ya wilaya wakampa takwimu zote za fweza, ndo alitaka kujua pesa ziliko enda. Basi wale wanao tafuna na wanasomeshea watoto wao ulaya wakaona huyo si mwenzao, kwa kutumia pesa zao wamewahonga madiwani na leo wakapiga kura ya kutokuwa na imani naye na kikao kilihudhuliwa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza " KANDORO"

CCM hawawataki kabisa watu ambao wapo kwa maendeleo ya UMMA
 
Asante kwa taarifa na maoni yako.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom