Mwenyekiti wa Hai ni Mama shupavu, awasomesha Polisi lakini wamembeba

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,720
2,000
Ona mwenyekliti halmashauri ya Hai, Helga Mchomvu alivyowajibu polisi. Inaonekana Mkuu wa Wilaya ya Hai alitaka kuwatumia Polisi kumnyamazisha huyu Diwani wa CHADEMA. aliwajibu sawa sawa na Vitendo vyao kwamba "Kama mumekuja kunikamata kwa makosa nliyoyafanya huko mtaani sina tatizo, lakini kama Mukekuja kuninyamazisha ili tusilaani kitendo cha Mkuu wa Wilaya kuharibu shamba la muwekezaji wa ndani kisa tu ni Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, Kamwambieni hataweza kuninyamazisha"

Polisi wakamsihi aache kuongea kwa sauti, akawajibu acha niongee umma usikie matendo yenu. Nyie Polisi siwalaumu sababu nyie ni nyuma geuka, mbele tembea.

"Sio kawaida kwa utaratibu wa kuja kusimamiwa na askari wakati naendesha baraza, baraza hili ni l ahalmashauri ya Wilaya ya hai kwa manufaa ya watu wa Hai. Mnanitoa kwenye Pozi la kuendelea kusimamia na kutafuta jinsi gani tuendelea kupata mapato ya Halmashauri hii".


MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA HAI ASHIKILIWA NA POLISI KWA SAA TANO BAADA YA KUMALIZA KIKAO CHA BARAZA.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai, Helga Mchomvu (kulia) akiingia katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Hai kwa ajili kuongoza kikao cha baraza hilo.Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Yahana Sintoo.


Mwenyekiti wa Baraza la Halmashauri ya wilaya ya Hai,Helga Mchomvu akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai ,Yahana Sintoo wakati wa kikao cha baraza la Madiwani.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akizungumza wakati wa kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo.

Baadhi ya Madiwani wanaounda baraza la Halmashauri ya wilaya ya Hai.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai, Helga Mchomvu akizungumza wakati wa kikao cha baraza hilo.

Baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hai wakiwa katika kikao cha baraza hilo.

Diwani Harry Masakia akisoma kanuni za kudumu za Halmashauri wakati wa kikao cha baraza hilo.

Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hai.Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Helga Mchomvu akitoka nje ya ukumbi wa mikutno mara baada a kuhairisha kikao cha baraza hilo.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,akizungumza na askari Polisi waliokuwa nje ya ukumbi wakimsubiri kwa ajili ya kumfikisha kituo cha Polisi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai, Helga Mchomvu akiongozana na askari Polisi wakati akilekea ofsiini kwake.

Askari Polisi wakiomngojea Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Helga Mchomvu nje ya ofisi yake .


Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai ,Helga Mchomvu akieleka kito cha Polisi huku akisindikizwa ana askari Polisi.


Mwenyekiti wa Halmahauri ya wilaya ya Hai ,Helga Mchomvu akiingia kituo cha Polisi Bomang'ombe.
 

INGENJA

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
4,995
2,000
Tanzania tunajivunia amani na upendo unaotumiwa na wenye madaraka kunyanyasa walio chini...!
 

dmketo

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
541
1,000
Kwa mujibu wa Thomas Hobes, asili ya binadamu ni ubinafsi, kusolve tatizo hilo akashauri tuwe na mfumo wa serikali (Leviathan) kudhibiti machafuko (State of nature) kati ya mtu na mtu katika kukidhi mahitaji binafsi.

Wanafalsafa wengi walipendekeza miundo mbali mbali ya serikali. Lakini watu wa Magharibi walionelea mfumo wa Demokrasia (Serikali ya watu, kwa ajiri ya watu na iliyoundwa/kuchaguliwa na watu) ni mzuri. Nasi waafrika wakati huo tulikuwa na aina zetu za Serikali kulingana na tamaduni, hulka na utengamano wa jamii zetu.

Miaka ya 90, kupitia msukumo wa nchi za magharibi nchi nyingi za Afrika kwa shingo upande zilianza kufuata mfumo wa Serikali za kidemokrasia ya kimagharibi (Vyama vingi/Mageuzi)

Kwa mtazamo wangu matatizo mengi yanayoendelea nchi nyingi za Afrika yalianzia hapo, nafikiri wengi tulijikuta tukiingia kwenye mfumo wa kidemokrasia ambayo haikuendana na hulka yetu, tamaduni zetu na hata huwezo wetu wa kuyachanganua mambo. Nafikiri ili Afrika iwe salama ni lazima tuanze kufikiria upya aina ya demokrasia inayoweza kuendana na matakwa yetu. Nafikiri hivi kutokana na ukweli kwamba maeneo mengi ya Afrika kumekuwa na chaguzi za hovyo ambazo waliopo madarakani hawapo tayari kuachia dora, maeneo mengine waliopo madarakani kutaka kuhodhi nchi kuwa mali zao binafsi na hata maeneo mengine walio nje ya mfumo wa madaraka kuonekana si lolote bali takataka.

Nakaribisha mawazo huru ili kuelimishana Zaidi. Huu ni mtizamo wangu juu ya ili na mengine mengi yanayoendelea Afrika
 

leiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
621
1,000
Kama sio kuogopa kuitwa mchochezi, ningeshauri maoni ya Nasari aliyoyasema enzi za balehe yake kisiasa yafanyiwe kazi.
Yaani KASKAZINI waanze kutafuta uhuru wao. Na sisi wa Rorya na Tarime tutaomba hifadhi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom