Mwenyekiti wa Chama Chetu akisoma hotuba zinakuwa na hoja, akitoa kichwani analeta taharuki kwa lugha inayodhaniwa kuwakera akina mama

Mikono yenye Sugu

Senior Member
Jul 1, 2020
133
215
Nashauri wasaidizi wa Mwenyekiti ambaye pia ni Mgombea wetu katika kipindi hiki cha kampeni wamshauri hotuba zake azisome tu. Wapinzani wetu wanafuatilia kila neno litokalo kinywani mwake na wanatumia baadhi ya maneno, ambayo wakati mwingine ni ya utani, kutuchapia viboko huku mtaani.

Bahati mbaya Mwenyekiti wetu akiweka maneno ya kuchomeka huishia kuponyokwa na maneno ambayo yanakirihisha hasa anapotoa utani kulenga akina mama. Wengine hutafsiri kuwa anadharau wanawake au hata kumtuhumu kuwa hana maadili.

Naomba chondechonde wasaidizi au washauri wake wamshauri kujikita kwenye hotuba iliyoandikwa kwani mpinzani wetu ana kipaji cha kupangilia maneno pasipo kusoma kwani taaluma yake ni pamoja na mabishano. Tukimuiga tutaingia mtaroni, tarehe 28 sio mbali.

Ni ushauri tu kwa chama changu!
 
Wakenya wanamtambua kama mtu MKAIDI! Huwa hasikii na pia hashauriki! Hivyo hata haya uliyo yaandika yataishia humu humu.
 
Back
Top Bottom