Zanzibar 2020 Mwenyekiti wa Chama cha ADC, Hamad Rashid Mohammed achukua fomu ya kugombea Urais Zanzibar

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,763
4,327
Mwenyekiti wa Chama cha ADC ambaye pia ni Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohammed, amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia chama hicho.

 
Nahisi kwenye kampeni atasema ataendeleza yale yaliyofanywa na CCM. Wakati huo CCM watasema wataendeleza waliyofanya na kubuni mapya. Sasa akili kumukichwa. Atakuwa anawapigia CCM kampeni au atakuwa anajipigia yeye mwenyewe?
 
Katika watia nia wote Urais, muungano na visiwani, nitajieni ambaye hajawahi kuwa mwana CCM.
 
Na uwaziri hatoupata tena maana kwa vyovyote vile chama chake hakitoki cha pili na kujumuishwa kwenye serikali ya kitaifa.
 
Ni Hali yake na kila mtu anahaki ya kufanya hivyo, wenye uwezo huo hata uliyepo hapa, nenda kajipime
 
Safari hii atafute tu kazi nyingine ya kufanya. Awamu hii, wenye Visiwa vyao (Team Maalim Seif) kupitia ACT Wazalendo, hawatokubali tena kuwaachia mamluki kuitafuna keki ya Visiwa vyao.
 
Hii ndio kazi ya mwisho aliyoandaliwa kuifanya baada ya hapo arudi akachunge mabata.Kazi yenyewe ni kumtukana maalim Seif jukwaani kuisadia CCM
 
Safari hii atafute tu kazi nyingine ya kufanya. Awamu hii, wenye Visiwa vyao (Team Maalim Seif) kupitia ACT Wazalendo, hawatokubali tena kuwaachia mamluki kuitafuna keki ya Visiwa vyao.
Seif mwaka wa 20 na huu anagombea yeye tu na anashindwa 😃
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom