Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Nachingwea ajiunga na CCM

Kumbe makamu wa rais kwenye ziara ya kiserikali kazi yake kuwapa kadi wanachama wapya? Kama ndio hivyo tutaendelea kuwa maskini kwa muda mrefu kama hatutachukua hatua ya kubadilisha hali hii/mfumo huu yaani kukiua ccm.
 
Hivi mtu awe anaishi Nachingwea halafu ahaidiwe au apewe cash money kwa ajili ya kuama chama unadhani anaweza kuziacha hizo pesa? kama hamfahamu wastani wa wakazi wa mikoa ya Mtwara na Lindi ni kura nyama kilo moja kwa mwaka mzima, sasa hapo mnaweza mkapata picha ya yaliojiri.
 
Kumbe makamu wa rais kwenye ziara ya kiserikali kazi yake kuwapa kadi wanachama wapya? Kama ndio hivyo tutaendelea kuwa maskini kwa muda mrefu kama hatutachukua hatua ya kubadilisha hali hii/mfumo huu yaani kukiua ccm.
Hapo napingana na wewe mimi naona huo ndio utaratibu wetu, kwani hata Maalim Seif Juzi juzi tu alikuwa na ziara za kichama mikoa ya Mwanza, Lindi na Dar es salaam lakini alikuwa anatumia resource za serikali. naomba nisiwe mnafki kwenye hili.
 
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, hongera sana kwani naona unajiongezea CV katika mbio zako za kuusaka Uraisi 2015! Ingawa hiyo ni ndoto tu lakini ni haki yako asiyoweza kukunyang'anya mtu, lakini unaonaje kama ungetumia ziara yako kumsaidia bosi wako kutekeleza japo moja katika ahadi lukuki alizotoa 2010 ? Najua muda mwingi huna la kufanya lakini hii ya kutumia rasilimali ya taifa kupokea kadi moja ya Chadema, aarrghh !

Naona hapo jirani yako upande wa kulia ni Mkuu mpya wa Mkoa wa Lindi, Mwananzila, aliyeikimbia Mkoa wa Shinyanga kinyemela kwa kushindwa kuwajibika kwa wananchi. Unaonaje kama badala ya kupokea kadi ya mlalahoi Hassan Mkope, ungekuwa unapokea ripoti kutoka kwa huyo RC, kuhusu mpango wa namna ya kuboresha maisha ya wana Lindi, moja ya mikoa inayotia huruma kwa umasikini, ujinga na maradhi ?

Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, unaonaje siku nyingine ukifanya ziara maalumu ya kisiasa mkoani Lindi kabla ya uchaguzi ndani ya CCM lakini safari hii uambatane na katibu wa oganaizesheni, Nape Nnauye. Siku hiyo bila shaka mpango kabambe utafanyika kuhakikisha uongozi mzima wa Chadema mkoani Lindi unajisalimisha kwako na kukabidhi kadi kama alivyofanya Waziri Ngeleja huko Sengerema, hiyo itakuwa ni CV ya kufa mtu na saizi yako!
 
nakumbuka pia niliwahi kutabiri kuwa kabla ya mwaka 2013 chadema itakuwa imekufa sio kilimanjaro tu,hata katika mikoa ambayo inaonekana walau ina ahueni ya wanachama,mwaka 2012 umeanza vinaya kwa chaga development manifesto,( matukio mnayo,sengerema & na hawa wa nachingwea) kuna tetesi kuwa hapa mwanza mjini na hata wilaya ya geita viongozi wa cdm watavua magwanda,kisa? Yana joto sana

Sengerema tulishatoa feedback magamba walichukua wachovu 30 waliokwisha fukuzwa cdm, I mean wanachama wafu tukalamba 55 walio hai tena damu changaaa. Hivi unafikiri mukimchukua mzee kama huyo wa miaka 60+chadema watashtuka?unaelewa wazi kuwa ngome kubwa ya cdm ni vijana na tegemeo kubwa la vijana ni cdm. Tunahitaji wazee sawa lakini sio wale mizigo wanaofuata harufu ya pilau.tisheti na kanga tunataka wazee wachache wenye fikra hai zinazoweza kuishi miaka kadhaa ijayo. Hivyo huyo mchukueni akakae na kingunge warioba mwinyi nk
 
Mzee huyo namfahamu vizuri alkuwa CCM akaja Nachigwea Lipumba akajiunga na CUF, alipokuja Dr Slaa akajiunga na CHADEMA na amekuja Dr Bilal karudi CCM, Subilini aende Mrema mtamsikia TLP na akizuka huko Mbatia mtamsikia NCCR......
Halafu mimi nkienda kule mtaskia kajiunga na JF!!!!!
Ha ha ha ha!!!!!!
 
Niliwahi kuwaambia humu JF baada ya Bunge tutaona vigogo wa Magwanda wakiondoka, wakanishutumu, wakanikejeli, sasa naona hawataki hata kuikumbusha ile nyuzi, maana mimi nilifikiri watakuwa wawili watatu, lakini sasa naona ni makundi kwa makundi. Maaaweeee!

Kwani awali walitengewa shilingi ngapi ili kuwanasa wawili watatu na hatimaye zimeongezwa sh. ngapi hadi wanakuwa makundi???
 
Mi naona hawa ni wale wanaotumikia matumbo tu &nbsp;sasa walienda CDM wakizani watapata kitu kidogo kumbe CDM ni wazalendo na wapambanaji wanahitajika &nbsp;sasa kamuona huyo mzenji &nbsp;kaona hamkabithi kadi bila shaka kapewa chochote si bure.<br><br>ILA KUNA JAMBO SIILEWI LABDA WANA JAMVI MNISAIDIE HUKO KUSINI BILALI ANAFANYA &nbsp;ZIARA YA KICHAMA AU YA KITAIFA MI SIELEWI THIS IS WASTAGE OF RESOURCES (UPOTEZAJI WA RASILIMALI ZETU) nadhani yule mzee anaitwa msajili wa vyama vya siasa atusaidie hizi gharama wanazotumia kina ngeleja na bilali ni halali kufanya shughuli za kichama
 
Mizigo inazidi kujiengua CDM. Angechelewa kidogo angefukuzwa na chama. Heri amesepa mapema.

kwanini tunapenda sana chama kufukuza wanachama wake.hakuna namna bora ya kuwakosoa na kuwakanya wakajirekebisha mle mle kwenye chama?nadhani uongozi wa juu wa chama ulitafakari hili.
 
Niliwahi kuwaambia humu JF baada ya Bunge tutaona vigogo wa Magwanda wakiondoka, wakanishutumu, wakanikejeli, sasa naona hawataki hata kuikumbusha ile nyuzi, maana mimi nilifikiri watakuwa wawili watatu, lakini sasa naona ni makundi kwa makundi. Maaaweeee!
Nilipoona jina tu sikushangaa kwa nini karudisha kadi.... unafiki ni sehemu ya maisha ............
 
Niliwahi kuwaambia humu JF baada ya Bunge tutaona vigogo wa Magwanda wakiondoka, wakanishutumu, wakanikejeli, sasa naona hawataki hata kuikumbusha ile nyuzi, maana mimi nilifikiri watakuwa wawili watatu, lakini sasa naona ni makundi kwa makundi. Maaaweeee!
Huyo naye kigogo unanchekesha mnauziwa mbuzi kwenye gunia na nyie mnakubali muulizeni Ngeleja atawaambia.
 
Huyo naye kigogo unanchekesha mnauziwa mbuzi kwenye gunia na nyie mnakubali muulizeni Ngeleja atawaambia.
Ngeleja hana hamu na hii kitu,
Bora hata angeuziwa mbuzi kwenye gunia, hiyo inaitwa kuuziwa mlio,
Pamoja na kuishi kote Dsm jamaa walimuingiza mjini.
Yaani mtu anajibanza uchochoroni na kufanya "meeeeeeee", halafu huku wewe unalipia hela kwa mwingine ukidanganywa ni mbuzi.
 
wanaotoka cdm kurudi ccm ni wanafiki/mamluki lakini wanaotoka ccm kwenda cdm ni mashujaa,kazi kweli kweli.
 
Amekabidhiwa kadi ya ccm na makam wa rais Mohamed Ghalib Bilal.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha kadi ya CHADEMA baada ya kukabidhiwa na Hassan Mkope (kulia) aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wa Wilaya ya Nachingwea, aliyeamua kujiengua na kujiunga na CCM. Makamu ameanza ziara yake katika Mkoa wa Lindi jana januari 20.

source:mjengwa na michuzi blogs

Kaona vijana wanakuja chukua nafasi hiyo,akaamua bora arudi kwa vilazi wenzie c.c.m
 
Nothing so special ni jambo la kawaida sana. na linatokea kila siku kila upande na kila chama ndio siasa zenyewe hizo hakuna haja ya kuanza kurushiana madongo.
 
Amekabidhiwa kadi ya ccm na makam wa rais Mohamed Ghalib Bilal.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha kadi ya CHADEMA baada ya kukabidhiwa na Hassan Mkope (kulia) aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wa Wilaya ya Nachingwea, aliyeamua kujiengua na kujiunga na CCM. Makamu ameanza ziara yake katika Mkoa wa Lindi jana januari 20.

source:mjengwa na michuzi blogs

Hata hivyo naona ni kikongwe, asingeweza kuhimili kazi ya ki-kamanda, bora akae na magamba
 
Niliwahi kuwaambia humu JF baada ya Bunge tutaona vigogo wa Magwanda wakiondoka, wakanishutumu, wakanikejeli, sasa naona hawataki hata kuikumbusha ile nyuzi, maana mimi nilifikiri watakuwa wawili watatu, lakini sasa naona ni makundi kwa makundi. Maaaweeee!

wakumbushie, wasimike msumari wa moto kumoyo... thubutu hiyo ni kuumia kimyakimya2....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom