Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Monduli asimamishwa uongozi mara moja

Crashwise

Crashwise

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Messages
22,173
Points
2,000
Crashwise

Crashwise

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2007
22,173 2,000
TAARIFA KWA UMMA


KUKOMA KUWA KIONGOZI KWA MWENYEKITI WA WILAYA YA MONDULI MCHUNGAJI AMANI SILANGA MOLLEL

Kwa niaba ya baraza la uongozi la mkoa wa Arusha, napenda kuujulisha umma wote kwa ujumla kuwa mwenyekiti wa wilaya ya monduli Mchungaji Amani Silanga Mollel amekoma/amesimamishwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya monduli kuanzia tarehe 29 Novemba 2013 kufuatia tuhuma nzito za uvunjifu wa kanuni za maadili ya chama.

Hatua hii imefikiwa baada ya kuthibitika na yeyé mwenyewe kukiri mbele ya kikao cha kamati tendaji ya wilaya ya monduli kilichoketi tarehe 29 Novemba 2913 saa NNE asubuhi kuwa alitoa tamko batili akitumia wadhifa wa mwenyekiti wa wilaya bila ridhaa ya kamati tendaji na huku akidanganya kuwa ni tamko kwa niaba ya wilaya ya Monduli.

Katika tamko lake ametoa tuhuma dhidi ya wajumbe wa kamati kuu na viongozi wakuu wa kitaifa kwa maamuzi halali ya kikao cha kamati kuu huku akijua kuwa anavunja kanuni za chama kwa mujibu wa katiba ya chama toleo la mwaka 2006 ya Kanuni za uendeshaji kazi za chama, sura ya KUMI, ibara ya 10 (X) "Kiongozi asitoe tuhuma zozote juu ya viongozi wenzake pasipo kupitia vikao halali na kuzingatia taratibu na ngazi zilizoelezwa kwenye kanuni za chama".

Sambamba na hilo, Mchungaji Amani Silanga ametoa tuhuma za uzushi, uongo na upotoshaji na kutaka kuaminisha jamii kuwa chadema ina makundi ya CHADEMA Asili na CHADEMA Family kitu ambacho ni upotoshaji mkubwa na wa hatari kwa ustawi na umoja wa chama na kinyume na kanuni za uendeshaji kazi za chama, sura ya KUMI, ibara ya 10 (VII), "Kiongozi anatakiwa kuwa mkweli na muwazi wakati wote hususani katika vikao halali na aachane na vikundi vya majungu, wadanganyifu (Rumour Mongers). Ni mwiko kwa kiongozi kujihusisha na upotoshaji wa maamuzi wa vikao halali".

Kamati tendaji ya wilaya ilipomtaka aonyeshe CHADEMA asili ni kina nani na CHADEMA family ni kina nani alishindwa kutoa maelezo yoyote ya maana na kufikia hatua ya kutaka kuvuruga kikao kwa kuleta vijana wahuni wapatao 17 ndani ya kikao ambao wengi walijulikana kuwa sio WANACHADEMA. Katika utambulisho wake wa majigambo Mchungaji Amani SIlanga kwa kiburi na kejeli amejitambulisha na kukiri kuwa yeye yupo kambi ya Zito Kabwe na hakuna wa kumfanya kitu maana ni mjumbe wa baraza kuu la chama. Maneno yake yalidhihirisha kuwa Mchungaji Amani Silanga anashiriki mpango wa kuunda makundi yasiyo na tija ndani ya chama na hivyo kuwa kinyume na sura hiyo hiyo ya kumi ya kanuni za uendeshaji kazi za chama ibara ya 10 (IX), "Kiongozi asijihusishe au kushiriki na vikundi au vitendo vya kuchonganisha au kuzua migogoro ndani ya uongozi wa chama au wanachama wake".

AZIMIO LA BARAZA LA UONGOZI LA MKOA WA ARUSHA:
Baraza la uongozi la mkoa lililoketi tarehe 29 Novemba 2013, limepokea mapendekezo ya kamati tendaji ya wilaya na kuzingatia hofu kubwa iliyoainishwa na kamati tendaji kufuatia matendo mengi yanayotia shaka ya uadilifu na uwezo wa kiuongozi wa Mchungaji Amani Silanga na hivyo baraza la uongozi la mkoa limeridhia kuwa amevunja kanuni za maadili ya chama sura ya KUMI ibara ya (VII) hadi (XII) na hivyo kupelekea ukomo wa yeye kuwa Mwenyekiti wa wilaya kuanzia tarehe 29 Novemba 2013. Baraza la mkoa likiwa mamlaka ya nidhamu kwa mujibu wa katiba ibara ya 6.3.6 (a) (iv) limemjulisha tuhuma zake na hatua hii stahiki iliyochukuliwa. Kwa vile Mchungaji Amani Silanga alikiri kosa hili mbele ya kamati tendaji ya wilaya bila kulijutia au kuomba msamaha, baraza la mkoa limechukua hatua hii stahiki kwa maslahi ya chama na kuwa uchunguzi zaidi utafanyika ili kufikia maamuzi makubwa zaidi ya tuhuma nyingi kwa mujibu wa kanuni za hatua za kinidhamu.

Baraza la uongozi la mkoa wa Arusha, linatoa onyo kwa wote ambao wapo katika mtandao huu mchafu, ama watoke wenyewe mapema maana hawatavumiliwa kamwe. Baraza la uongozi wa mkoa liliona kuwa Mchungaji Silanga amepotoka na hivyo yeyé kuendelea kuwepo ndani ya chama wakati wa uchunguzi wa tuhuma hizi nzito dhidi yake ni hatari zaidi kwa ustawi wa chama na hivyo baraza likaridhia kwa kuzingatia tafsiri ya katiba ya chama ibara ya 6.3.4 (c) wa yeyé kukoma uongozi na hivyo akae nje kwa muda na waliopotoka wenzake.Amani Golugwa
Katibu wa CHADEMA – Mkoa wa Arusha.
(Kwa niaba ya Baraza la Uongozi la Mkoa wa Arusha)
Tarehe 30 Novemba 2013

==========================
 
M

Martin Jr

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2011
Messages
582
Points
0
M

Martin Jr

JF-Expert Member
Joined Nov 29, 2011
582 0
Chadema chama cha maamuzi. .......
 
M

Martin Jr

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2011
Messages
582
Points
0
M

Martin Jr

JF-Expert Member
Joined Nov 29, 2011
582 0
Mwenyekiti wa cdn monduli afukuzwa nadikiri title ingepaswa kuwa hivi
 
Mungi

Mungi

JF Gold Member
Joined
Sep 23, 2010
Messages
16,982
Points
1,500
Mungi

Mungi

JF Gold Member
Joined Sep 23, 2010
16,982 1,500
Kwa wale wapuuzi kama akina Chitanda huko waendako wasome katiba za taasisi, nimeshangaa mtu ana package ya sheria lakini hajui katiba.

mshenzi ni mshenzi tu hata uwe na degree 200
 
Zuberi Magoha

Zuberi Magoha

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Messages
208
Points
0
Zuberi Magoha

Zuberi Magoha

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2013
208 0
Kwa wale wapuuzi kama akina Chitanda huko waendako wasome katiba za taasisi, nimeshangaa mtu ana package ya sheria lakini hajui katiba.

mshenzi ni mshenzi tu hata uwe na degree 200
Mungi
Chitanda ni empty bucket hana package aina yeyote ni fundi wa makelele majukwaani.Baba yake tamaa kubwa unategemea mtoto awe fofauti kiasi kikubwa ?Haiwezekani na Chitanda ana kundi lake mfu kama yeye .
 
manning

manning

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2013
Messages
3,525
Points
1,250
manning

manning

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2013
3,525 1,250
Hili fagio la chuma alilopewa Mwinyi CCM wakalitelekeza jalalani na CHADEMA wakaliokota naona wanalitumia vizuri. Nawapongeza ninyi safisheni nyumba watu wanaweza kukimbia vumbi kwa muda lakini baadae watakuja wengi zaidi kwa sababu mazingira yanaruhusu mtu aishi kwa raha bora kuliko kuishi jalalani.
 
K

kakururwechu

New Member
Joined
Sep 8, 2013
Messages
4
Points
0
K

kakururwechu

New Member
Joined Sep 8, 2013
4 0
Sure bila kuwa na uamuzi sahihi chama kitakuwa change ajabu bila mwelekeo we need to do things at aright time
 
Zak Malang

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Messages
5,405
Points
0
Zak Malang

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined Dec 30, 2008
5,405 0
Safi sana! Pulizia dawa kunguni, mende na mbu wote watokomezwe CDM. Twataka CDM mpya kabisa.
 
M

Martin Jr

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2011
Messages
582
Points
0
M

Martin Jr

JF-Expert Member
Joined Nov 29, 2011
582 0
Hongera cdm huyu mchungaju ni mnafiki sana bora amefukuzwa
 
Crashwise

Crashwise

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Messages
22,173
Points
2,000
Crashwise

Crashwise

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2007
22,173 2,000
Kwa wale wapuuzi kama akina Chitanda huko waendako wasome katiba za taasisi, nimeshangaa mtu ana package ya sheria lakini hajui katiba.

mshenzi ni mshenzi tu hata uwe na degree 200
kama wabakaji wa ccm.. wanawaza kubaka tu
 
mangikule

mangikule

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2012
Messages
3,617
Points
2,000
mangikule

mangikule

JF-Expert Member
Joined Jun 11, 2012
3,617 2,000
Intelligence unit leta majina ya mamluki wote tuwasafishe wote!!
 
Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined
Jan 18, 2007
Messages
14,597
Points
2,000
Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined Jan 18, 2007
14,597 2,000
Swift and bold action.Kusema kweli kutika kuwashughulikia watu kama hawa sipendi urasimu.Hatua za haraka kama hizi ndiyo zinazofaa.Hongera sana kwa uongozi thabiti wa mkoa.
 
Mungi

Mungi

JF Gold Member
Joined
Sep 23, 2010
Messages
16,982
Points
1,500
Mungi

Mungi

JF Gold Member
Joined Sep 23, 2010
16,982 1,500
Huyu Amani bila shaka ni moja wa wale mbweha 45 wanaotusumbua kwenye chama......


CHADEMA - Chama chenye maamuzi yanayozingatia haki na ukweli
 

Forum statistics

Threads 1,326,837
Members 509,593
Posts 32,236,901
Top