***** MWENYEKITI CHADEMA KITANZINI KWA WIZI WA MAFUTA YA WAKANDARASI WA BARABARA YA TUNDUMA -SUMBAWANGA *********
Wakati chama kikipita katika wakati mgumu wa ombwe la uongozi kuanzia ngazi ya taifa mpaka ngazi za kata,kiongozi aliyesimikwa uenyekiti na Mbowe ili kupanga safu yake ya ushindi,Mzee ZENO NKOSWE mwenyekiti wa Chadema mkoa wa RUKWA juzi aliashikiliwa na kuhojiwa na polisi katika kituo cha polisi Sumbawanga kwa tuhuma ya wizi wa mafuta aina ya disel yanayosadikika kuibwa kwa wakandari wa Aaslef Interbeton wanaojenga barabara ya Tunduma -Sumbawanga.
Tukio hilo lilitokea juzi tarehe 28 novemba 2013 majira ya saa 8 mchana baada ya polisi kufanya msako maeneo mbalimbali na ndipo muda huo wakavamia nyumbani kwa mwenyekiti huyo na kukuta madumu ya lita 20 yanayokadiriwa kufika 50 yakiwa yamehifadhiwa katika moja ya chumba kilichopo kwa mzee Nkoswe.
Ndipo polisi wakambeba na kwenda nae kutoa maelezo juu ya hujuma hiyo inayofanyika dhidi ya miradi mikubwa ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi.
Kigogo huyo wa chama cha upinzani yupo nje kwa dhamana akisubiri hatua zitakazofuata baada ya upelelezi kukamilika.
Hiyo ni muendelezo tu wa kashfa nzito za uhujumu zilizowahi kumkumba Mzee Nkoswe kwani wakati akiwa mkuu wa wilaya mbalimbali nchini aliwahi kujimilikisha ng'ombe za wananchi ambao walitoa kama mchango kwa ajili ya wanajeshi wetu waliokuwa vitani kumng'oa Nduli Iddi Amini dada, aliwahi kufanya ufisadi mkubwa pia katika mgodi wa machimbo ya makaa ya mawe na kujimilikisha ardhi kubwa ambayo imeibua minong'ono kwa wananchi ambao hawana maeneo ya kilimo.