Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Singida ajiuzulu. Adai Kamati Kuu ni wanafiki...

mwenegoha

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
205
101
WILFRED NOEL KITUNDU
MWENYEKITI CHADEMA MKOA SINGIDA
S.L.P 260
3.12.2013
KATIBU WA CHADEMA MKOA
S.L.P 260
SINGIDA
YAH: - KUJIUZURU UENYEKITI MKOA SINGIDA
Somo hapo lahusika,
Ninapenda kukuarifu kuwa nimeamua kujiuuzuru nafasi yangu ya uenyekiti wa mkoa ambayo nimekuwa nikiitumikia kwa kipindi kirefu sasa kama kielelezo cha kuamini na kudai demokrasia ya kweli ndani ya chama.

Ikumbukwe kwamba mimi ndio mwanachama wa kwanza kujiunga na CHADEMA mkoa wa SINGIDA na ni mwanachama wa 300 kitaifa, hiyo ni heshima kubwa sana kwangu na sipo tayari kuipoteza kwa kukubali kuwa sehemu ya udharirishaji huu wa demokrasia uliopitiliza

Maamuzi na vitendo vinavyoendelea ndani ya chama chetu kwa sasa ni ubakaji na udharirishaji wa demokrasia ya kweli tunayoihubiri mbele ya umma.

Kwa barua hii basi, nimeonelea bora upate ufahamu huo kuwa si vema mimi kuendelea kupingana na dhamira yangu inayonituma kuwa mwanademokrasia wa kweli.

Kwa kipindi hiki kifupi mnaweza mkaendelea kuitumia anuani yangu ya posta mpaka hapo mtakapopata anuani yenu tayari.

Ninatanguliza shukrani zangu za dhati kwa wanachadema wote wanaopinga upuuzi huu uliofanywa na kamati kuu ya chama.

Kusimamia haki, katiba na misingi ya chama ni wajibu wangu, hivyo kwa namna yoyote ile sitaweza kuwa tayari kufumba macho pindi ujinga wa namna hii unapoendelea kutekelezwa kwa uwoga wa uchaguzi.


Nakutakia kila la heri kwenye majukumu yako.

………………………………………………….
Wilfred N. Kitundu
0764619335/0786215181


________________________

MSIMAMO WA MWENYEKITI CHADEMA MKOA WA SINGIDA DHIDI YA UAMUZI WA KAMATI KUU YA CHAMA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



UTANGULIZI
Ikumbukwe kwamba mimi ndio mwanachama wa kwanza kujiunga na CHADEMA mkoa wa SINGIDA na ni mtu wa 300 kitaifa kujiunga na Chama hiki. Nimejiunga mwaka 1992 siku ya mkutano mkuu kwanza wa uzinduzi chama uliofanyika mnazi mmoja.

Nimekuwa nikijitolea vya kutosha nguvu, muda na akili zangu nyingi kukijenga na kukilinda chama hiki mpaka sasa mkoa wetu wa singida umepata wabunge watatu mmoja wa kuchaguliwa na wawili wa viti maalum.

Tangu mwaka 1992 mpaka 2011, chadema imekuwa ikitumia nyumba yangu kama ofisi, nimekuwa nikifanya hivyo kama kielelezo change cha kudai na kupigania demokrasia ya kweli ndani ya nchi kwa kuijenga CHADEMA imara.

Kwa kipindi chote hicho nimekubali kujibana na kuipunja familia yangu stahili zake ili chama chetu kikue kwa kasi mkoani kwetu, nashukuru mungu wanasingida waliitikia ombi nletu na kutufuta majozi yaliyotokana na jasho langu kwa kutupatia mbunge mwaka 2010.

Hivyo nimehudhunika sana kwa kitendo kilichofanywa na wajumbe wa kamati kuu cha kukiuka utaratibu na kujivalisha mamlaka yasiyowahusu.


HISTORIA YA USALITI KWENYE CHADEMA
Viongozi wa chama chetu wamekuwa na historian a tabia ya kutubadilishia wasaliti na kuwapachika kila aina ya shutuma kila kunapokaribia uchaguzi ndani ya chama.

Tuliambiwa na kuaminishwa kuwa KABURU ni msaliti mkubwa ndani ya chama.

Tukaambiwa na kuaminishwa kuwa CHACHA WANGWE alikuwa msaliti, tukafanyishwa vikao vya ndani, tukaanzishiwa mikakati mbali mbali kuwa wangwe ni msaliti na kwamba anatumika.

WANGWE alipofariki hali ikatulia kidogo, tukaanza kuimba na kumsifia kwamba ni kamanda, tukamuita majina yote ya kishujaa lakini haikuwa na faida yoyote.

Sasa hivi tumeanza kuaminishwa wasaliti wengine wapya, safari hii wasaliti hawa wamevuka usaliti na kuwa WAHAINI, masikitiko yangu ni hawa wahaini ndio wale wale wengine waliokuwa wakikitetea chama kipindi kinapingwa na waliokuwa wasaliti.
Bahati mbaya sana na cha kufurahisha kama si cha kusikitisha hakujawahi kutokea Msaliti, Mhaini Wala kiongozi yeyote anayetuhumiwa kukihujumu chama mwenye asili ya KILIMANJARO ama KASKAZINI kwa ujumla, wahaini na wasaliti wote wanatokea mikoa yetu sisi wanyonge.

WAVAMIZI NDANI YA CHAMA
Bahati mbaya sana, harakati hizi za kuibua na kuwashuhulikia hawa wanaoitwa wasaliti zinafanywa na wavamizi ama wahamiaji ndani ya chama, nitatoa mifano michache muda huu.

1. GODBLESS LEMA tulimpokea kwenye chama hiki mwaka 2009 akitokea TLP aliposhindwa kufanya siasa za ushindani baada ya kushiriki kukiua chama hicho, lema alikwenda TLP akitokea NCCR-mageuzi aliposhindwa kutimiza malengo yake ya kisiasa na kushuhudia akikiua chama hicho. Leo LEMA ndio mpambanaji mkuu dhidi ya Zitto Kabwe, Dokta Kitila mkumbo na demokrasia ya kweli ndani ya chama chetu, anaambatana na kijana mwengine anaitwa MAWAZO, huyu wakati sisi tunapambana na CCM mwaka 2010 kuwanadi wagombea wetu wa ubunge urais na udiwani, yeye alikuwa anagombea udiwani kupitia CCM tuliyokuwa tunaipinga, ameingia chadema na sasa wale waliokuwa wanampinga akiwa huko leo anawaita WASALITI na WAHAINI.

2. MCH. MSIGWA naye huyu ni hivyo hivyo tulimpokea CHADEMA baada ya kushindwa na kuigombanisha NCCR na baadae TLP. Baada ya kuvimaliza vyama hivyo sasa wamehamia chadema kutugombanisha na kutuharibia chama chetu kwa makusudi kabisa.

3. Wengine vinara kwenye mgogoro huu ni Tundu Lissu, bensoni kigaila, john mrema na wengineo hawa ni vijana tuliowapokea kuja kujenga chama na sio kukibomoa chama kama wanavyofanya

4. TUNDU LISSU yeye ni kinara sana wa kumshambulia zitto kwenye hili, lakini ninasikitika kusema kuwa Tangu nimekuwa mwanachadema na Tangu nimemfahamu Lissu alipohamia CHADEMA hajawahi kufanya mkutano hata mmoja wa kujenga chama ndani ya mkoa wa SINGIDA ukiondoa jimboni kwake. Tumemuona Zitto akitoka bungeni na mara nyingine hata kigoma kuja kufanya mikitunano maeneo mbali mbali hapa singida ikiwemo iramba, singida mjini na kwingineko, na mtakumbuka zitto amewahi kukamatwa na polisi mkoni singida akikinadi chama, hakuwa lissu. Sasa leo anapotoka mbele na kujinadi kuwa ana mapenzi mazuri na chama kushinda zitto kabwe ni upuuzi unaopaswa kukemewa kwa nguvu kubwa sana.

Ninasikitika sana kuona Mwenyekiti Mbowe na Katibu mkuu Slaa wanawakumbatia hawa, ninashangaa sana kuona viongozi hawa wanakubali kuwa sehemu ya ubakaji huu mkubwa wa demokrasia.

Ninaamini kabisa vijana hawa wanatumiwa na mwenyekiti na katibu mkuu kuutumia uzoefu wao walioutumia kwenye vyama vyao vya awali mpaka kuviua.


KUHUSU KAMATI KUU NA MAAMUZI YAKE.

Uamuzi wa kuwavua nyadhifa zitto kabwe na wenzake kwa madai ya kuwa na mkakati wa siri wa uchaguzi, ni uamuzi wa kipuuzi na wa kupuuzwa, kwenye hili kamati kuu imedhihirisha namna gani inaundwa na watu wasio na weledi na hawaongozwi na misingi na taratibu za chama.

Katika chama chochote kile, kamati kuu haiwezi kuwa mshitaki mkuu, hiyo hiyo iwe mwendesha mashitaka, hiyo hiyo iwe shahidi, hiyo hiyo iwe hakiku na hiyo hiyo iwe muandika hukumu. Hapa wamedhihirisha ni namna gani wanaongozwa na Hisia na chuki zinazotawaliwa na hofu ya uchaguzi ndani ya chama.

Kamati kuu hii ya sasa haipo kwa ajili ya maslahi ya wanachama na chama kwa ujumla, ipo kwa maslahi ya mbowe na slaa pengine na watu wa kaskazini.

Kwa hiyo kuwazuia watu wenye mawazo tofauti na wao na kuwaita wasaliti na wahaini ni sawa kuasisi na kuimiza mpasuko ndani ya chama, maana kuna mambo kamati kuu inaweza kufanya na kuna mengine haiwezi, hii haiwezi kufanya hili walilolifanya sasa hawawezi kulifanya.

Nionavyo mimi na wanachama ninaowaongoza hapa singida ni kwamba kamati kuu imekurupuka na kufanya maamuzi yaliyotawaliwa na hofu, chuki na uroho wa madaraka dhidi ya zitto kabwe na wenzake walioonyesha nia thabiti ya kukivusha chama kwenye harakati za kuilikomboa Taifa.

MSIMAMO WA CHAMA SINGIDA
(i) Tunalaani, kuipinga na kuikemea kamati kuu ya chama dhidi ya maamuzi yao haya ya kipuuzi yaliyojaa chuki, hofu na wasiwasi mwingi kuelekea uchaguzi mkuu wa ndani ya chama

(ii) Tunamtaka mwenyekiti na katibu mkuu waitishe mara moja mkutano wa baraza kuu la chama kutolea maamuzi suala hilo.


(iii) Tunamtaka katibu mkuu awazuie wakurugenzi na maafisa wake aliowatuma kusambaa mikoani kusambaza waraka wa siri unaowachafua zitto na kitila na kwamba kufanya hivyo ni kujidharirisha wao wenyewe.

(iv) Tunampa onyo kali katibu mkuu Dkt. Slaa kuwa asithubutu kukanyaga SINGIDA ikiwa bado hajayafanyia kazi maelekezo yetiu hapo juu, kuzunguka kwake mikoani baada ya kumvua vyeo zitto ni kwenda kuthibitisha kuwa amefanya makusudi mpango wake huo.


(v) Tunapenda wanachadema na watanzania watambue kuwa Hatuna Imani na Mwenyekiti wa Taifa wa chama, Katibu Mkuu wa Chama, Kamati kuu kwa ujumla na tunamuagiza mbowe aivunje mara moja kisha nay eye ajiudhuru.



MWISHO

Kutokutii maamizio yetu haya ni kusababisha mgogoro usiokuwa na kikomo ndani ya chama hiki,

Singida tunasema kuwa '' kamati kuu inaweza kumvua zitto kabwe uongozi, inaweza kumuondolea heshima yake ndani ya jamii, inaweza pia kumsingizia kila aina ya uwongo itakavyo, lakini kamwe kamati kuu haiwezi KUZUIA MPASUKO NDANI YA CHADEMA.''




Kwa kuzingatia utangulizi wangu hapo mwanzo, na kwa kuona ukweli kwamba chama chetu sasa kimevamiwa na kuwa na vyama viwili ndani ya chama kimoja,

Nimeonelea ni vyema sasa niilinde na kuithibitisha dhamira yangu ya demokrasia ya kweli, nimeona ni vema nihakikishe demokrasia tunayoiimba tunaitenda kwa vitendo.

Kwa misingi hiyo sasa, nimeamua kukaa pembeni ya udhalimu huu wa demokrasia unaoasisiwa na viongozi wakuu wa chama wanaoogopa kivuli cha uchaguzi mkuu wa ndani ya chama,

Nimeona ni vema sasa niuthibitishie umma wa Tanzania kuwa kwenye chadema unaruhusiwa kugombea vyeo na nafasi zote isipokuwa uenyekiti wa Taifa ndio maana zitto tuliyemuunga mkono leo hii anashambuliwa kwa dhamira yake safi ya kidemokrasia.

Nimechoka sasa, nimebadili mawazo, sipo tayari tena kuwa msukule wa fikra mbele ya watu wanaopenda kuigiza na kujifanya watetezi wa wanyonge kumbe ni wanafiki wa kutupwa.

Nimememuandikia barua katibu wangu wa mkoa kumueleza maamuzi yangu ya kujiudhuru uenyekiti wa mkoa, sihitaji tena kuwa mwenyekiti wa mkoa kwenye chama ambacho hakitendi kinachoyasema, sihitaji tena kuwa mwenyekiti wa mkoa kwenye chama ambacho dakika na saa yoyote unaweza ukageuzwa na ukaitwa msaliti na muhaini wa aina ya kopekee.

Mimi kitundu, sihitaji kuendelea kuwa dalali wa mafanikio ya kisiasa kwa ajili ya watu wa kaskazini dhidi ya watanzania wenzangu.

Nimejiuzuru uenyekiti wa mkoa wa SINGIDA kuanzia leo tarehe 3.11.2013 na kuahidi kuwa nitapambana mpaka mwisho wa tone la damu ya uhai wangu kuhakikisha demokrasia ya ndani ya chama hiki inaheshimiwa na kwamba watanzania hawadanganywi tena.

Nawashukuru sana.

Wilfred Noel Kitundu
Mwenyekiti Mkoa SINGIDA
Muasisi na mlezi wa CHADEMA Singida 1992-2013
Mjumbe wa Baraza Kuu TAIFA 1992 – 2013
Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa 1992-2013
+255786215181/0764619335

____________________________________________________________________

ALILOSEMA LISSU JUU YA KUJIUZULU KWA MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA SINGIDA

akijib mjadala pale wanabidii....

|•••••|•••••|•••••|•••••|•••••|••••|

Wanabidii,

Kwa vile aliyejiuzulu ni Mwenyekiti wangu wa Mkoa, na kwa vile amenituhumu specifically kuwa ni mmoja wa 'wavamizi' ndani ya CHADEMA ambao ndio 'vinara' wa migogoro ndani ya chama chetu, nafikiri nitasemehewa nikiweka utetezi wangu hapa jukwaani.

Wilfred Kitundu is probably the longest serving regional chairman wa CHADEMA katika nchi hii. Na ni kweli, Kama anavyosema, kwamba kwa muda wa karibu miaka ishirini ya uenyekiti wake, sebule ya nyumba yake ilikuwa ndio Ofisi ya chama ya Mkoa. Which is another way of saying, kwa miaka yote hiyo, chama hakikukua.

CHADEMA haikuwa na Mwenyekiti wa kitongoji, wala wa kijiji, wala Diwani, achilia mbali Wabunge. In fact, viongozi wetu wa kwanza wa kuchaguliwa - wenyeviti wa vitongoji na wa vijiji - walichaguliwa mwaka 2009, mwaka mmoja baada ya mimi kuvamia na/au kuhamia CHADEMA Singida. Mwaka 2010 tulipata, kwa Mara ya kwanza tangu mungu aumbe mbingu na nchi, Wabunge na Madiwani wasiokuwa maCCM.

Sitaki kujisemea sana katika hili, lakini nafikiri mchango wangu katika kuijenga CHADEMA Singida ni mdogo. On the other hand, zaidi ya kutuwekea Ofisi ya Mkoa sebuleni kwake, sidhani kama Mzee Kitundu ametoa mchango mwingine wowote katika mafanikio haya. Zaidi ya kula pesa zetu za kampeni ya udiwani katika Kata ya Urughu mwaka 2011 wakati wengine tukiwa kwenye mapambano ya uchaguzi mdogo wa Igunga, sidhani kama nitakuwa namsingizia Mzee huyu nikisema kwamba hatujamwona akishiriki kwa maana yoyote katika harakati za kisiasa za CHADEMA Singida. Mtu aliyemwokoa kutokana na hasira ya wanachama baada ya kula hela za kampeni kata ya Urughu ni ....... Jaza mwenyewe!!!

Mwaka huo huo wa uchaguzi, kulikuwa na skandali ya mgombea ubunge wetu wa Singida mjini kuenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi kwa maelekezo ya Mh. Zitto Kabwe. Mtu aliyetumiwa kuweka pingamizi ili mgombea wetu aenguliwe alikuwa wakati Mwenyekiti wa CHADEMA Singida mjini Wazaeli Nakamia. Tulipambana hadi tukamrudisha mgombea wetu kwa kushinda rufaa kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Mzee Kitundu hakuwahi kusema chochote, either way, kilichokuwa kinaendelea kwa sababu Mhusika Mkuu wa skandali hiyo, kama alivyo Mhusika Mkuu aka MM wa Mkakati wa Mapinduzi 2013, alikuwa mfadhili wake yaani Zitto Kabwe.

CHADEMA imekuwa sana katika Mkoa wa Singida tangu 2010. Kwa kiasi kikubwa, pengine kuliko mtu mwingine yeyote katika Mkoa wetu, ni mvamizi na mhamiaji Tundu Lissu. I can say with a straight face kwamba Jimbo pekee ambalo sijawahi kufanya mikutano ya hadhara ni Iramba Magharibi. Mengine yote nimefanya mikutano ya hadhara hata kabla sijawa Mwenyekiti wa M4C Kanda ya Kati.

In brief, naweza kusema, as a matter of fact, kwamba Mzee Kitundu amejiuzulu kwa sababu mfadhili wake ameng'olewa madarakani na Kamati Kuu. I also can say with clear conscience kwamba Mzee Kitundu ataondoka peke yake CHADEMA Singida. Hana following yoyote Mkoa ule. Hata mkutano wa Mtaa hawezi kuitisha akapata watu. Kuondoka kwake ni good riddance, at least inatupunguzia mizigo ambayo tumeibeba kwa miaka mingi!

One final point: kwa vile amemtaja marehemu Chacha Wangwe kama mmoja wa wasaliti waliong'olewa CHADEMA siku za nyuma, ni vizuri wananchi wafahamu kwamba Mzee Kitundu, kama Zitto Kabwe, alikuwa mmoja wa Wajumbe wa Kamati Kuu 'iliyowaaminisha' Watanzania kwamba Chacha Wangwe alikuwa msaliti mwaka 2007! Kama anabisha mwuulizeni jamaa yake anayempigania sasa hivi!

Kama ilivyo katika historia ya mapambano ya ukombozi ya zama zote, hakuna mapambano yasiyokuwa na akina Yuda Iskariote wake, yaani wale wanaosaliti cause kwa vipande thelathini vya fedha! Haijaanza jana wala juzi. Na haitaisha kesho. Kitu muhimu zaidi ni kwamba wasaliti wa aina hii hawajawahi kuzuia jua la haki kuchomoza na giza la ufisadi na uonevu kutoweka. Haitakuwa tofauti kwa CHADEMA. We, too, shall overcome. Tutashinda. Kama anavyosema mwanafasihi Shaffi Adam Shaffi katika kitabu chake Kuli: 'Yana mwisho haya'!

Tundu
 
Hawa ndiyo tunaowatafuta, bora waondoke kabla ya kuwanywa.
Chungu kiko motoni, hii siyo CCM iliyoshindwa kutoa magamba.
Hatuonei mtu huruma, tutawapiga chiniiiiii wote
 
TUNTEMEKE kweli wapenda kuanzisha mada! Unasubiriwa ukajibu maswali kwenye ile mada uliyoianzisha kuhusiana na Mchungaji Msigwa kuwasilisha rambirambi alizokuwa akidaiwa!
 
Last edited by a moderator:
Tunakushukuru Baba Mungu Muumba wa mwingu na nchi kwa kutonyesha haya makapi mapema. Mimi naomba wale wote wanaoona viongozi waliopo hawafai ondokeni Chadema mapema sana. hii itatusaidia kujipanga vizuri tukiwa na watu watiifu na waaminifu. Nenda Nenda tangulia. CCM wanawadanganya na 5,000,000 ambazo zitaisha kwa miezi miwili mnadanganyika. Go Go Go and goodbye.
 
Tunakushukuru Baba Mungu Muumba wa mwingu na nchi kwa kutonyesha haya makapi mapema. Mimi naomba wale wote wanaoona viongozi waliopo hawafai ondokeni Chadema mapema sana. hii itatusaidia kujipanga vizuri tukiwa na watu watiifu na waaminifu. Nenda Nenda tangulia. CCM wanawadanganya na 5,000,000 ambazo zitaisha kwa miezi miwili mnadanganyika. Go Go Go and goodbye.

una roho ngumu mlokole wewe kama moyo wa mwendawazimu!
 
haya hayana budi kutokea ili Giza lijitenge na Nuru..watu dhaifu hawana subir..waseje tu wakakuta mlango umeshafungwa
 
Good enough kuna mdau alinitonya juu ya ujio wa hili tamko toka Singida!!! Kweli unafiki ni zaidi ya dhambi yoyote!!
 
Dah! Naona Kamanda ameandika kwa hisia kali sana!

Lakini anaonekana mpenda mageuzi maana bado amewaachia CHADEMA waendelee kutumia anuani yake kwa ajili ya shughuli za chama.

'Wasaliti' wote waondoke CDM wawaache 'wanademokrasia wa kweli'
 
Sasa huyu ameshajiuzulu halafu anatoa tamko kama kiongozi na anaweka maagizo ya kuitishwa Baraza kuu kana kwamba yeye bado ni kiongozi.

Ukisoma tamko hili , ukirejea la Nyakarungu, ukisoma l. Mwenyekiti wa Temeke , ukisoma la yule Mwenyekiti feki wa Matawi ya. Chadema Mwanza ........utaona kuwa yamefanyika na mtu mmoja , hawa wanasoma tu.

Kitundu huyu amekuwa Mwenyekiti wa. Chadema Mkoa wa Singida tangu mwaka 1992 , leo anasema kuwa anaipinga Kamati kuu , eti demokrasia hakuna , eti katiba ilichezewa , mbona yeye amekaa muda mrefu kuliko wengine ?

Sarakasi ,zao kamwe hazitafanikiwa kwani wanachama wako imara na kamwe hawaendeshiwa Propaganda, eti Mwenyekiti wa Mkoa an ajiuzulu hata bila mfuasi mmoja nyuma yake ? Kuna la kujifunza hapo......
 
28 Reactions
Reply
Back
Top Bottom