Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Iringa na wenzake wajiunga CCM

Hawa ni waganga njaa.Ni opportunists ambao kwa kitendo chao hicho, wamewasaliti wananchi maskini wa Tanzania. Wananifanya niamini kwamba hawajui wanachokiamini. Uwezekano mkubwa mkubwa hata hivyo ni kwamba walikuwa mapandikizi.

Kwa hiyo ni vema wameondoka mapema. Kwa vile hata hivyo wasinge saidia katika vita dhidi ya uonevu wa watanzania maskini.
 

MAKADA watatu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Iringa Bensony Kapwani pamoja na mwenyekiti wa jimbo wa Chadema jimbo la Ismani Ally Mohamed Ally wamekihama chama hicho na kujiunga na chama cha mapinduzi (CCM)

Akitangaza rasmi kujiunga na CCM na kurudisha kadi ya uanachana na Chadema pamoja na kujivua uenyekiti wa mkoa ,mbele ya spika Makinda ,kapwani alisema kwa upande wake ameamua kujiengua rasmi uongozi na uanachama Chadema kutokana na kuwa na imani kubwa ya mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Jakaya Kikwete ambaye amekuwa akisisitiza umoja katika uongozi wake.

Kapwani ambaye kabla ya kutangaza kujiunga na CCM alikuwa amesimamishwa nafasi yake ya uenyekiti wa mkoa wa Chadema kwa kutuhumiwa kukihujumu chama chake Chadema kwa hatua yake ya kushindwa kurudisha fomu ya kugombea ubunge jimbo la Ismani na kupelekea mgombea wa CCM Wiliam Lukuvi kukosa mpinzani na hivyo kupita bila kupigwa ,alisema kuwa Chadema imepoteza mwelekeo na kuwa kwa upande wake ameamua kurudi CCM ambacho ni chama chenye mwelekeo wa kweli .(Maneno haya ni ya watu wasiokuwa na mwelekeo kisisasa)

Pia alisema kuwa kwa upande wake na wenzake hawajapendezwa hatua ya wabunge wa Chadema kutoka nje ya ukumbi wa bunge wakati Rais Kikwete alipokwenda bungeni kulihutubia bunge na kuwa kitendo kilichofanywa na wabunge hao wa Chadema ni utovu wa nidhamu na kwa upande wake hafungamani na uamuzi wa wabunge wake hao wa Chadema.


Habari hii ni kwa hisani ya blog ya Francis Godwin

Hili halinishangazi; mtu huyu alishajulikana tangu mwazo, na ningeshangaa kama angeendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA.
 
Melo,

Kwa Taarifa ya Wasomaji wako Mhe. Kapwani alikwisha kufukuzwa Chadema katikati ya Kampeni kwa makosa yafuatayo:

i) Aliuza jimbo la Isimani baada ya kuchukua fomu na dakika ya mwisho hakutokea kuirudisha hiyo Fomu. Taarifa inayoonyesha alifanya hivyo makusudi kwa makubaliano na mgombea wa CCM, na kuna viashiria kuwa alipewa fedha taslim 30 Millioni.

ii) Licha ya hiyo, na licha kutakiwa kujieleza alishindwa kujieleza, lakini wakati wa Kampeni alikuwa akifanya Kampeni ya NCCR Mageuzi na kuiombea NCCR Mageuzi jukwaani, na kutamka hadharani kama Wapiga kura hawatampa mgombea wa NCCR Mageuzi basi apewe kura mgombea wa CCM na siyo wa Chadema ambaye alikuwa akimkandia wazi wazi jukwaani. Akaandikiwa Barua ya kufukuzwa na siku mmoja kabla barua haijamfikia alijiuzulu uenyekiti wa Mkoa na kujitoa kwenye Chama .

Nilipokuwa kwenye Mkutano wa Kampeni Iringa nilieleza hadharani hali hiyo. Hivyo tunamtakia heri huko alikoenda, na sioni kwanini hiyo iwe habari leo wakati tuliisha kutangaza hadharani. Yeye hakutokea wakati wowote wa Kampeni katika kampeni ya Chadema Iringa Mjini. Ni vema wasomaji wa Jamvi hili wakamfahamu ni mtu wa aina gani.

Chadema daima itachukua hatua kwa watu wa aina hiyo, alimradi mtu amepewa nafasi ya kujieleza na kujitetea. Matendo ya uhaini wa aina hiyo na yenye sura ya ufisadi kamwe hayatavumiliwa pale yanapojitokeza.

Bila shaka kwa sura hiyo ameenda nyumbani kunakomstahili.
 
Wanafiki kama ninyi waliondoka na ndiyo sababu chama hiki chenye nia ya kuwasaidia wanyonge kinaendela, na kama kuna wengine wanafiki uliokuwa unashirikiana nao ni vema wakaondoka mapema kabla hajafukuzwa kwani inaonyesha chadema wako makini kufuatilia nyendo za wanachama wake.
Inaonyesha maji yamezidi unga ndo ukondoka.
 
Daima mimi huamini binadamu kama walivyo mamals wote tuna kipaji cha utambuzi wa tabia ya mtu kwa kuangalia ishara za usoni. Ndivyo tunavyomtambua taahira hata ktk TV. Nikimuangalia alivyo, sioni uelewa wowote na hata uaminifu.

Lakini pia nahisi bado CCM hawaamini yaliyowatokea ktk uchaguzi uliopita. Wataendelea kugawa pesa za kodi zetu mpaka 2015 ili tu kuonyesha kwamba CHADEMA haifai.

CCM watatue matatizo yao badala ya kuhangaika na maamuzi ya wa-TZ.
 
mkuu DR slaa phd wa kweli na siyo hao wanaogawiwa ambao hata kirefu cha phd hawajui. wanafiki kama kapwani wako wengi, naomba tuanze kuwahughulikia. huko moshi vijijini kuna mnafiki mwingine aitwae akwlini chuwa , yeye amekwamisha kesi ya kupinga ccm kuiba kura na kumtangaza chami badala ya mbunge halali komu, tunasikia amepewa chochote nachami. unda tume mkuu wetu
 
Ni haki yao kuhama kutoka chama hiki kwenda kingine! Wanatumia haki yao ya msingi au.....!
 
Namsikitikia Makinda kudai eti angewashauri wabunge wa chadema kama wangempa taarifa mapema. Yaani adui umpe mbinu ya kupigana?? Mama kilaza sijawahi kuona
 
Hata sishangai maana mwanzo wa hoye alitaka kugombea jimbo la Iringa Mjini akatolewa nje sasa kwa hasira akataka kuvuruga wezake wakamshtukia ndiyo mwanzo wa yote hayo. aende tu atajutia na mtamsikia yuko NCCR Mageuzi
 
Hawa wanafuatia kuganga njaa au kutafuta umaarufu. CCM isishangae kuwa iko siku na sio mbali wataondoka kwenda kwenye maslahi zaidi, labda CCM iwe ni wahongaji wakubwa. "Nendeni wana wa kwenda".
 
Back
Top Bottom