Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Iringa na wenzake wajiunga CCM

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
3,965
2,000
kapwanilukuvi.jpg


Aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema na mbunge ubunge Ismani Beny Kapwani (kushoto) akiwa na mbunge wa Ismani na waziri Wiliam Lukuvi

MAKADA watatu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Iringa Bensony Kapwani pamoja na mwenyekiti wa jimbo wa Chadema jimbo la Ismani Ally Mohamed Ally wamekihama chama hicho na kujiunga na chama cha mapinduzi (CCM)

Makada hao wa Chadema wamejiunga na CCM leo katika mkutano wa hadhara spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Anne Makinda ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa na mbunge wa jimbo la Njombe kusini,mkutano uliofanyika katika kijiji cha Tanagozi wilaya ya Iringa vijijini.

Akitangaza rasmi kujiunga na CCM na kurudisha kadi ya uanachana na Chadema pamoja na kujivua uenyekiti wa mkoa ,mbele ya spika Makinda ,kapwani alisema kwa upande wake ameamua kujiengua rasmi uongozi na uanachama Chadema kutokana na kuwa na imani kubwa ya mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Jakaya Kikwete ambaye amekuwa akisisitiza umoja katika uongozi wake.

Kapwani ambaye kabla ya kutangaza kujiunga na CCM alikuwa amesimamishwa nafasi yake ya uenyekiti wa mkoa wa Chadema kwa kutuhumiwa kukihujumu chama chake Chadema kwa hatua yake ya kushindwa kurudisha fomu ya kugombea ubunge jimbo la Ismani na kupelekea mgombea wa CCM Wiliam Lukuvi kukosa mpinzani na hivyo kupita bila kupigwa ,alisema kuwa Chadema imepoteza mwelekeo na kuwa kwa upande wake ameamua kurudi CCM ambacho ni chama chenye mwelekeo wa kweli .

Pia alisema kuwa kwa upande wake na wenzake hawajapendezwa hatua ya wabunge wa Chadema kutoka nje ya ukumbi wa bunge wakati Rais Kikwete alipokwenda bungeni kulihutubia bunge na kuwa kitendo kilichofanywa na wabunge hao wa Chadema ni utovu wa nidhamu na kwa upande wake hafungamani na uamuzi wa wabunge wake hao wa Chadema.

Naye aliyekuwa mwenyekiti wa jimbo la Ismani kupitia Chadema na mjumbe wa serikali ya kijiji cha Kimande ,Ally Mohamed Ally alisema kuwa hakuwa na mpango wa kuhama Chadema ila amefanya hivyo kutokana na jeuri ya wabunge wa Chadema na viongozi wa kitaifa ambao wameendelea kudai kuwa hawamtambui rais huku wakijua wazi kuwa Rais Kikwete hajajipeleka bungeni bali amekwenda kihalali kwa kura za wananchi wote wakiwemo baadhi ya wanachadema.

Mwanachama mwingine wa Chadema aliyejiujiunga na CCM ni Jella Lukinga ambaye alikuwa mpiga debe mkuu wa Kapwani wakati akigombea ubunge jimbo la Ismani kupitia Chadema.

Kwa upande wake Spika Makinda mbali ya kuwapongeza viongozi hao wa Chadema kwa kujiunga na CCM bado alisema kuwa uamuzi wao ni mzuri na umekuja wakati mwafaka ambao Taifa limeendelea kushuhudia ushindi wa CCM .

Pia alisema kuwa suala la wabunge wa Chadema kutoka nje ya ukumbi wa bunge ni utovu wa nidhamu na kuwa ilipaswa kumjulisha mapema juu ya uamuzi wao huo na ambao hata hivyo wabunge hao kanuni ilikuwa inawaruhusu kufanya hivyo ila kwa taarifa kwanza kwa spika.

Hata hivyo alisema anakusudia kuwaita wabunge wote na kuwasomea kanuni za bunge ili kila jambo wanalolifanya walifanye kwa kuzingatia kanuni badala ya kufanya kwa mkumbo .

Spika makinda alisema kuwa kwa upande wake suala la wabunge wa Chadema kutoka nje ya ukumbi wa bunge alikuwa akilisoma katika vyombo vya habari pekee na kama wangempa taarifa mapema basi angeweza kutoa baraka zake na kuwapa kanuni zaidi.

Akizungumzia hatua ya mwenyekiti wa Chadema mkoa kujiunga na CCM mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Taifa Chiku Abwao ambaye ni mbunge wa viti maalu mkoa wa Iringa alisema kuwa kuondoka kwake si tishio kwa Chadema na kuwa wao walijua mapema kama angekwenda CCM.

Pia alisema kuwa Chadema itaendelea kujengwa na wanachama wenye moyo na wasio ndumila kuwili kama kapwani na wenzake na kuwa kuondoka kwake ni mwanzo mzuri wa kuendelea kujenga mapinduzi ya kweli kati ya CCM na Chadema katika mkoa wa Iringa na kuwa Chadema siku zote itaendelea kubaki bila kuyumbishwa na wanachama kama akina Kapwani.

Habari hii ni kwa hisani ya blog ya Francis Godwin
 

kweleakwelea

JF-Expert Member
Nov 29, 2010
3,058
2,000
hahahah go away! tANZANIA ITAJENGWA NA WENYE MOYO NA ITALIWA NA WENYE MENO!!! NANI ANAVYO VYOTE?
 

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,814
2,000
CCM ingeacha kukumbatia watu kama hawa maana leo wanaisaliti CHADEMA na kesho ni CCM.

Siasa za TZ zimegeuka kama mpira tu. Wanachama hawana mapenzi tena na vyama na wanajali maslahi yao tu.
 

Ehud

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
2,686
0
Huyo mwenyekiti alishasimamishwa long time alichofanya ni kukamilisha taratibu zake za kurudi ccm!
 

seniorita

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
674
0
in the first place hawakuwa true to CDM, so sidhani kinashangaza kuondoka kwako....go in peace and serve fisadi, as you are also fisadi
 

Jasusi

JF-Expert Member
May 5, 2006
11,522
2,000

This says it all:

Kapwani ambaye kabla ya kutangaza kujiunga na CCM alikuwa amesimamishwa nafasi yake ya uenyekiti wa mkoa wa Chadema kwa kutuhumiwa kukihujumu chama chake Chadema kwa hatua yake ya kushindwa kurudisha fomu ya kugombea ubunge jimbo la Ismani na kupelekea mgombea wa CCM Wiliam Lukuvi kukosa mpinzani na hivyo kupita bila kupigwa ,alisema kuwa Chadema imepoteza mwelekeo na kuwa kwa upande wake ameamua kurudi CCM ambacho ni chama chenye mwelekeo wa kweli .
 

kipipili

JF-Expert Member
Jul 29, 2009
1,590
1,250
actually huyo mwenyekiti alikuwa mwenyekiti jina tu, yaani bonge ya mvurugaji. ukweli ni kuwa uongozi wa chadema kimkoa(iringa)ulikuwa unaendeshwa na uongozi wa manispaa chini ya Mch Msigwa. Imagine kulikuwa hakuna ofisi ya mkoa bali ofisi ya chadema manispaa. no gape left
 

Abdulhalim

Platinum Member
Jul 20, 2007
17,113
2,000
This clown kapwani I had a bad feeling hata alipotua hapa JF..thats just me I guess.
 

Horseshoe Arch

JF-Expert Member
Aug 10, 2009
13,147
2,000
Njaa zitawafikisha pabaya....waondoke tu..walikuta mlango wazi wakajiunga,watumie mlango ule ule kuondoka..watakaodumu hadi mwisho ndo wazalendo wa kweli...
 

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,694
2,000
RIP Kapwani. Baada ya lile saga la kumpitisha huyo kuwadi wako nilijua huu ndio utakuwa mwisho.
Ulikuwa mwana ccm tangu zamani lakini hukutaka ku announce mapema. RIP you and your fellows.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom