Mwenyekiti wa chadema mbeya mjini asema hayuko tayari kwenda kuhojiwa na polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenyekiti wa chadema mbeya mjini asema hayuko tayari kwenda kuhojiwa na polisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Duble Chris, Jul 13, 2012.

 1. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  [h=3]MWENYEKITI WA CHADEMA MBEYA MJINI ASEMA HAYUKO TAYARI KWENDA KUHOJIWA NA POLISI KUHUSU TUHUMA ZA UCHOCHEZI KWENYE MIKUTANO YA HADHARA[/h]

  [TABLE="align: center"]
  [TR]
  [TD][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Mbeya Mjini John Mwambigija,
  akiongea na waandishi wa habari katika hotel ya mbeya peak[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="align: center"]
  [TR]
  [TD][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, aliwaambia waandishi wa habari kwamba Mwenyekiti huyo anahitajika polisi kwa ajili ya kutoa maelezo kuhusu tuhuma zinazomkabili.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="align: center"]
  [TR]
  [TD]

  MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Mbeya Mjini John Mwambigija, amesema hayuko tayari kwenda kuhojiwa na polisi kuhusu tuhuma zinazomkabili za kutoa kauli za uchochezi kwenye mikutano ya hadhara.


  Kauli zinazodaiwa kutolewa na Mwenyekiti huyo zilitolewa kwenye mikutano ya wananchi wakati wa ziara ya viongozi wa CHADEMA katika Jimbo la Lupa Wilayani Chunya kwenye opareshini ya Chadema ya Twanga kotekote (NATO).


  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, aliwaambia waandishi wa habari kwamba Mwenyekiti huyo anahitajika polisi kwa ajili ya kutoa maelezo kuhusu tuhuma zinazomkabili.


  Alisema, moja ya tuhuma zilizolifikia jeshi la polisi kutoka kwa wananchi ni kwamba kiongozi huyo amekuwa akitoa maneno ya uchochezi huku akiwahamasisha wananchi kufanya vurugu zilizoambatana na uharibifu wa mali za watu.


  Alisema, kiongozi huyo akiwa katika mikutano, wananchi hueleza matatizo yanayowakabili amekuwa akiwahamisisha wakazi hao kudai haki kwa kufunga barabara na hata kuchoma nyumba za viongozi kama walivyofanya uharibifu wa mali za askari katika Kata ya Lupa Tinga-Tinga.


  “Kiongozi huyu amekuwa akiwahamasisha wananchi kuchoma matairi ikiwa na kufunga barabara pindi wanapotaka kutatuliwa madai yao kwa serikali jambo ambalo ni kinyume cha utaratibu wa sheria, hivyo jeshi la polisi linamtaka kiongozi huyo kufika kituoni ili kutoa maelezo ya tuhuma zinazomkabili,”alisema.


  Alisema, kazi ya askari ni kupokea malalamiko kwa maandishi na kuyafanyia kazi na kwamba katika utekelezaji askari huchukua maelezo ya pande zote mbili na ndio maana kiongozi huyo anahitajika kwenda kutoa maelezo ya upande wa pili.
  Aidha, Kwa upande wa Mwambigija alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza opareshini yao, alisema yeye yupo tayari kwenda kituo cha polisi endapo atakuwa na makosa ya jinai lakini kwa masuala ya kisiasa hawezi kufanya hivyo na endapo wataendelea kumfuatilia patachimbika kupitia nguvu ya umma.
  Alisema, kazi ya jeshi la polisi ni kufanyia kazi taarifa wanazozitoa na si kumwita yeye kwenda kutoa maelezo na kwamba wanachokifanya wao kwa wananchi ni kutoa elimu jinsi ya kukabiliana na changamoto za maisha.
  “Polisi tunawasaidia kufanya kazi na mimi sitaenda polisi kwa sababu tu za kisiasa kama ni hivyo CHADEMA kinawanasheria wengi ambapo tumekuwa tukikamatwa mara kwa mara na tunashinda kesi hizo,”alisema
  Mwambigija na kuongeza kuwa chama cha CHADEMA kinanguvu ya umma isiyotumia silaha bali maneno hivyo hatuwezi kufundishwa kutumia maneno matamu majukwaani.
  Alisema, kitendo cha polisi kuwaita kituoni kwa ajili ya kutoa maelezo eti kwa sababu walitoa maneno makali na kwamba hilo ni jambo ambalo hawezi kulifanya kamwe bali kama ingekuwa ni kosa la jinai.
  Hivi karibuni Mjumbe wa mkutano Mkuu Taifa kupitia chama cha Chadema, Edo Mwamalala alilitupia lawama jeshi la polisi kwa kushindwa kumchukulia hatua Mwenyekiti huyo wa Chadema wilaya kutokana na kauli zake za uchochezi anazozitoa kwenye mikutano ya hadhara.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  sorce MBEYA YETU
   
 2. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  Nadhani kuzidi kumtafuta huyo mwenyekiti ni kumtafutia umaarufu wa bila sababu, ushauri wangu ni kumwacha wananchi watampima wenyewe na kiasi kwamba maneno yake ni tathmini tosha ya nini kitakuwa kwa aina ya viongozi wajao
   
 3. M

  MKALIKENYA JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,198
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 133
  Tena wala asithubutu kwenda kwani JESHI LA POLISE limeisha poteza moral authority.
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ni vema Mkuu Saed Mwema ukajitafutia muda wa peke yako tu faragha na ukajihoji mwenyewe, BILA KUTUMIA MABAVU KATIKA KILA JAMBO, kwamba kulikoni wananchi tuwe tumefikia mhali hapo ya kutoliamini tena jeshi letu la polisi nchini wakiwa chini ya uongozi wako????????
   
 5. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,286
  Likes Received: 597
  Trophy Points: 280
  Kwenye wekundu ni sahihi?
   
 6. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Mkuu Mbugi,hapa kuna agent wawili wa ccm wanaopambana na mpambana na mpambanaji wa CHADEMA Mzee wa upako Mwambigija. 1. Policeccm na 2. Edo Mwamalala anayeshilikiana kwa karibu sana na Shitambala kuihujumu CHADEMA hapa Mbeya. Swaga za Mwambigija zimeisambaratisha ccm hapa wanapumulia mashine ambayo ni police na Edo Mwamalala.
   
 7. Makala Jr

  Makala Jr JF-Expert Member

  #7
  Jul 13, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hakuna cha maelezo,Mzee Mwambigija yuko sahihi kabisa.Hawa police tunawalipa kodi zetu then wanaanza mambo ya kipuuzi tu kisa wanatumika kisiasa.Kwanza huyo Edo ameongea ujinga sana...eti wananchi wanachochewa maanake hawana akili? Hivi unaweza kumwambia mtu kavunje kile nae akavunje meaningless? Huo uchochezi wanaufanya viongozi wa CHADEMA pekee? Mhe.Livingstone Lusinde amenukuliwa akitukana wapinzani mara kibao ,kwani huo siyo uchochezi mbona hahojiwi? Mafisadi wanafilisi mali za umma na kuchochea ugumu wa maisha kwa kukosekana kwa huduma za kijamii hivyo kupelekea social unrest kwani wamewahoji wangapi? N.B Tuongeze sifa za kiwango cha elimu kwa wanaojiunga jeshi la police,nadhani hawana fikra pevu na wanatumika kirahisi na wanasiasa.Kabla ya Mwambigija wamhoji Kandoro kwani aliwahi kuchochea fujo za machinga kwa kauli ya kuwahamisha kwa nguvu bila miundo mbinu kujengw
   
 8. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  ukiniambia juu ya Edo mwamalala na Mwambigija naweza kupata picha kidogo, lakini juu ya police kuwa ccm sikubaliani nanyi hasa police wa mbeya kwani nakumbuka sana nafasi ya police kwa uchaguzi uliopita kwa ushiriki wao mkubwa kuhakikisha MH sugu anachomoka na mshindi, moja ni ilie ya moja kwa moja ya kumpigia kura, na hata namna walivyokuwa wanatoa maelekezo na fursa fulani kwa vijana ktk kupenyeza ishara muhimu, kama kupanga foleni kwa kutumia vidole viwili nk.
  USHAURI
  Kwa mzee upako ningemshauri atii amri aende police, aachane na vyombo vya habari nchi yoyote ile haiwezi kwenda kwa ubabe bila sheria, na pili haileti picha nzuri kwa umma, na swala la mageuzi ni mwendo mdundo kwani hata kama chama chake kikapata nchi watajitokeza wenye mrengo tofauti na ambao bado watataka mageuzi zaidi, na kama mwendo ni huu wa kutotii waliomadarakani hatuwezi kufika? hivyo niombe aende tu aeleze then sidhani kama hiyo yaweza kuwa tatizo hasa ukuzingatia ukiwa mwenyekiti haupo juu ya sheria.
   
 9. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 180
  Hebu irudia wewe mwenyewe kuisoma au utumbie umailewaje.
   
Loading...