Mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya mjini, anusurika kupigwa jukwaani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenyekiti wa CHADEMA Mbeya mjini, anusurika kupigwa jukwaani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by the horse, Jun 15, 2012.

 1. t

  the horse JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 578
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  [​IMG]

  MWENYEKITI wa CHADEMA, wilaya ya Mbeya mjini, John Mwambigija, leo amenusurika kushushwa jukwaani na kupigwa na baadhi ya wanachama waliokuwa na mabango ya kutomtaka.

  Mwambigija aliokolewa na polisi waliofika kwenye mkutano huo, uliokuwa unafanyika eneo la soko la SIDO lililopo mjini hapa, baada ya kupata taarifa za kuwepo dalili za kutokea fujo kwenye mkutano huo.

  Mengi ya mabango yaliyokuwa yameandaliwa, yalikuwa yamekunjwa kwa kuhofia kukamatwa na polisi, lakini yalionyeshwa mara baada ya Mwambigija kupanda jukwaani na kuanza kuhutubia.

  Wakizungumza baadhi ya viongozi wa CHADEMA, ambao hawakutaka kutaja majina yao, walisema wamechoshwa na tabia ya Mwenyekiti wao huyo kukiharibu chama hicho, kwa kujenga makundi ndani yake.

  Waliongeza kutokana na adhima yao kushindwa kutimia kwa kuogopa polisi, watahakikisha wanaitisha mkutano wa ndani wa kumkataa Mwambigija, na baadaye watafanya mkutano mwingine wa hadhara ili kuanika udhaifu wa kiongozi huyo.

  Kwa mujibu wa wana-CHADEMA hao, Mwambigija amekuwa anakiendesha chama hicho jinsi atakavyo yeye, na hilo linachangiwa kwa kiasi kikubwa madai ya kuwa analindwa na Katibu Mkuu Taifa Dk.Willbroad Slaa.

  Naye Mwambigija alipotafutwa kuthibitisha tukio hilo, alisema yeye halifahamu na wala hakuona mabango yoyote katika mkutano huo.

  "Unajua tuna mamluki ndani ya CHADEMA, ambao wanaongozwa na aliyekuwa Katibu wetu wa mkoa, Eddo Mwamalala…baada ya kutoka kwenye uongozi amekuwa anaandaa mtandao wa kuhakikisha naondolewa kwenye uongozi" alisema Mwambigija.

  Aliongeza kuwa wanachama hao hawana ubavu wa kumshusha jukwaani wala kumpiga, na alikana tuhuma za kuendesha siasa za chuki kuwa huo ni uzushi ambao baadhi ya wana-CHADEMA wamekuwa wanamzulia.

  Hivi karibuni Mjumbe wa mkutano mkuu wa CHADEMA taifa, Mwamalala, akizungumza na vyombo vya habari alisema Mwambigija ni kiongozi ambaye amekuwa akitumia majukwaa ya siasa kupandikiza mbegu za uchochezi.

  Mwamalala alisema ni vyema Jeshi la polisi lianze kuzifanyia kazi kauli anazozitoa awapo jukwaani, kwani mwisho wa siku zitakuja kuvuruga amani ya mkoa wa Mbeya na taifa kwa jumla.
   

  Attached Files:

 2. DCONSCIOUS

  DCONSCIOUS JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,272
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Hakuna kosa ambalo watafanya chadema mbeya kama kumtoa mzee wa upako.tunajua jinsi ambavyo eddo anatumiwa na ccm kuivuruga chadema lakini kiukweli. Mwambigija ni noma sana na kwa siasa ya mbeya huyu jamaa anatufa sana.
   
 3. Mpangamji

  Mpangamji JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2012
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 536
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hiyo picha yenyewe imepigwa kimagumashi gumashi, toa hapa propaganda zenu za nyinyiem, CDM waelimisheni watu wa mbeya, mob physchology inaweza kutumika kuharibu chama. take care. Unrestless people suspects anything na uwezo wa kufikiri unashuka, ndivyo ilivyo kwa watanganyika kwa sasa.
   
 4. F

  Froida JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Duuh Mwamalala inamaana bifu yake haijaisha tu , kwa hiyo anatengeneza mazingira ya kuharibu chama Mbeya ili wakose wote si amfuate bosi wake shitambala akiache chama
   
 5. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  napita,wafu wazikane wenyewe
   
 6. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,975
  Likes Received: 6,613
  Trophy Points: 280
  the horse acha mchezo mchafu. Hapa jf sio sehemu ya kuchafuana na kupigiana debe.
  Umelipwa bei gani hadi ulete picha za uongo. kwanini ufiche sura ya aliyeshika bango? na huo mkutano ulikuwa na watu wangapi? Haijaniingia akilini. kajipange upya. Mia
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. t

  the horse JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 578
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Ina maana hapa JF hakuna wakazi wa mbeya mjini waje wakujuze kilichotokea coz siku zote huwa hamtaki kuamini kutoka kwa wale baadhi ambao wanasema msiyotaka kuyasikia.
   
 8. M

  Molemo JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Wanaompinga Mwambigija ni vibaraka wa Shitambala/ccm
   
 9. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Uchunguzi ufanyike ili ukweli ubainike. Majungu na fitna ni siasa za magamba.
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Jun 15, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Magwanda vs CHADEMA ? kwi kwi kwi teh teh teh.

  Halafu ndio tuwape nchi hawa? Maawee!
   
 11. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #11
  Jun 15, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,108
  Likes Received: 7,366
  Trophy Points: 280
  Hiyo picha imepigwa makao ya ccm, angalia background.

  Kwanza imepigwa kuelekea juu ili kuficha kujua watu waliokuwepo karibu.

  Propaganda zako zimejulikana we farasi pori
   
 12. K

  KISAKA MORIS JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 372
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtatupa tu maana imewashinda nyie' kamuulize mwenyekiti wako wa taifa anavyotamani kuikabidhi nchi hata leo ila anaona aibu anatamani 2015 iwe hata leo.


  Chadema Mbeya kuweni na uvumilivu tutatue matatizo yetu kwa amani kama kawaida yetu, tusizipe hasira nafasi. Mungu awe pamoja nanyi.
   
 13. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #13
  Jun 15, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  tumia akili wewe kuendesha propaganda zako za kijinga hapa JF ni watu na akili zao hakuna utakae mshika na hiyo taarifa yako ya kiseng...nimeonge na washikaji wanasema hakuna ktu kama hicho hiyo picha umepigwa na mmeo ili uilete jf..
   
 14. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #14
  Jun 15, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,278
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  umechemsha mbeya hakuna huo upuuzi!
   
 15. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #15
  Jun 15, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,839
  Trophy Points: 280
  Mta hangaika sana mwaka huu kutafuta habari za cdm
   
 16. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #16
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Molemo naamini Mbeya ni sehemu ya ngome za CDM, kumbe nako kumesheheni mamluki? Ina maana Shitambala bado ana kundi kubwa huko CDM la kuweza kumtikisa Mwambigija?

  Domokrasia ni pamoja na kupingana lakini CDM siku hizi wana mtindo kila mtu akipinga anaitwa mamuluki. Ukisoma kwa makini na kama alichoripoti mtoa mada ni kweli basi utaona mzizi wa makundi ndani ya Chama. Haya makundi siyo kwamba yako huko mikoani tu bali yanaanzia mbali.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #17
  Jun 16, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,015
  Likes Received: 2,663
  Trophy Points: 280
  We mleta mada mbona watu hawaonekani?na ni mkutano gani usiokuwa na watu,halafu mbona hapo nyuma kuna maduka?

  Uliwahi ona wapi mwanachadema anaogopa kubeba bango eti kwa kuhofia police?
  kwani hayo mabango yalikuwa yameandikwa matusi mpaka wafiche?

  propaganda zako zimekwama kajipange upya.
   
 18. N

  Njaare JF-Expert Member

  #18
  Jun 16, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Unafiki mbaya! Hii picha umeipigia home kwako. Mbona hukuonyesha mkutano wenyewe?

  Pili mi ninavyojua Mwenyekiti wa chama anachaguliwa na si kuwekwa na makao makuu. Iweje mumchague nyie halafu mumtake Dr. Slaa amtoe? Mnaijua katiba kweli?

  Ha ha haa! Mnanikumbusha ule msemo kuwa ndoa mfungishane kwa padre kwa vifijo na nderemo halafu songombingo la kuachana mumpelekee hakimu!
   
 19. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #19
  Jun 16, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  the horse, Tume ya katiba, ritz, Rejao, MAFILILI siyo watu wa kuaminika Mkuu usiumize kichwa
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #20
  Jun 16, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  Jamani kama hafai ni kheri aondolewe, tuzingatie maslai ya chama kwanza mtu badae
   
Loading...