Mwenyekiti wa CHADEMA - London aenguliwa wadhifa

Kibadachi

New Member
Apr 14, 2012
2
6
Habari zilizopatikana hivi punde kutoka kwenye vikao vya CHADEMA kupitia Kurugenzi ya Mambo ya Nje, Mwenyekiti wa CHADEMA tawi la London Bwana. Lukosi, amesimamishwa kuendelea kuwa mwenyekiti wa CHADEMA London kutokana na maswala ya kinidhamu.

Inasemekana Bw. Lukosi alienda nchini Tanzania mwezi Septemba mwaka huu na kukutana na wakuu wa Serikali ambapo aliahidiwa kupewa tenda kubwa ya kuclear mizigo ya Serikali. Kutokana na ahadi hiyo Bw. Lukosi alirudi jijini London na kuanza kuivuruga CHADEMA hali ambayo imesababisha kusimamwishwa kwake kuwa mwenyekiti wa CHADEMA -LONDON.

Stay tuned for more details...

Taarifa Rasmi Kutoka Chadema UK Blog

Ikiwa ni takribani miezi minne tangu tawi la CHADEMA UK lifunguliwe rasmi na Mr Godbless Lema, kumekuwepo na maendeleo makubwa ya ujenzi wa tawi hili lakini vile vile kumekuwepo na changa moto mbali mbali kutokana na uelewa wa watu ktk dhana nzima ya M4C. M4C ikiwa na maana ya Movement for Change, ni sharti mtu yeyote anayeingia ktk movement hii kwenye ngazi ya uongozi aelewe haya machache ya msingi:

1) Kwanza aone matatizo yanayomgusa yeye na jamii yake

2) Ajue na kutambua fika chimbuko la matatizo haya

3) Awe tayari kuwa kiini cha mabadiliko ya kweli anayoyataka kwa jamii

4) Aweze kutoa ufumbuzi kwa kukemea maovu, kuelimisha na hata yeye binafsi kuelimika

5) Ili afanikiwe ktk kipengele cha (4) ni sharti ajitambue yeye binafsi ya kwamba ni:
i) Lazima awe safi na mwenye sifa za kukemea waovu
ii) Aweke maslahi ya jamii mbele na si yake binafsi
iii) Awe na sifa za uongozi zinazotakiwa, nidhamu ikiwa nambari moja ktk orodha.
iv) Awe na msimamo wa kiitikadi

Kwa hiyo, uongozi wa CHADEMA UK kwa baraka za watetezi wa haki ya kweli (CHADEMA TZ) unawatangazia umma watanzania kokote mlipo kwamba kuanzia leo tarehe 12/12/12, Mr Christopher Lukosi amevuliwa rasmi uongozi na amesitishwa uanachama kutokana na kutokidhi mengi ya yaliyotajwa hapo juu.

Uongozi wa CHADEMA UK unamshukuru sana kwa mchango na ushirikiano wake mkubwa kwa kipindi ambacho matundu ya chujio yalikuwa makubwa. Tutaendelea kumkumbuka na hata kutumia misemo yake yenye maana nzito kwa jamii ya kitanzania, kama vile: -

i) Sisi sote ni ndugu, tatizo ni CCM
ii) Kila kwenye msafara wa mamba na kenge wamo

Uongozi unamwakikishia Mr Christopher Lukosi kwamba mamba wote wa CHADEMA UK kwa kushirikiana na wote wenye kuelewa mageuzi ya kweli, tutaliondoa tatizo ifikapo 2015. Tunamtakia kila la kheli katika maisha na ni imani yetu tutaendelea kuwa ndugu yake baada ya tatizo kutatuliwa !!!!.

"We fail in most of our endeavours because we too often underestimate People's Power" [M4C UK, 2012]

Sorce: CHADEMA UK BLOG - chademauk.blogspot.co.uk
 
Aisee mwaka huu tutasikia mengi!

Msafara wa mamba kenge wamo, bora CHADEMA mmegundua mapema. Wapo wengi wakutimua ndani ya CHADEMA ambao ni mamluki. CHADEMA kuweni macho zaidi safisheni chama toeni makapi yote.

Bora kuwa na watu wachache wenye moyo ndani ya uongozi wenu kuliko kuwa na makapi yatakayotia shombo juhudi zenu za kuikomboa nchi yenye maziwa na asali
 
Kama ni kweli basi atakuwa MJINGA wa Mwaka.

Kwani sasa CCM wanamuhitaji tena? CCM fukuzeni huyu Msaliti.

Kama aliweza kusaliti chama chake cha CDM, basi hata nyie atawatenda. Fukuzilia mbali na tenda asipewe.
 
Chilisosi,
Kamanda tufahamishe kinachoendelea huku London, juzi tu mlikuwa na Lema mkaonana na Meya wa London mkapewa Chopa imekuaje tena.
 
Last edited by a moderator:
Chilisosi,
Kamanda tufahamishe kinachoendelea huku London, juzi tu mlikuwa na Lema mkaonana na Meya wa London mkapewa Chopa imekuaje tena.
Habari kama hizi naona ndizo unazotaka! Na leo napo utashindia hapa mithili ya nzi anayetaka kufia kwenye kidonda!!!
 
Nimeamini kila mtu ndani ya Chadema ananunulika, tatizo bei.

Mkuu si kweli, makamanda halisi ndani ya CHADEMA hawanunuliki.

Vinginevyo mgeshawanunua wote.

Hakuna kamanda ndani ya Chadema ambaye hajawahi kushawishiwa kwa pesa yenu ya mafisadi akisaliti chama.
 
mwaka huu watasaga mahindi yakiisha watasaga magunzi bata muwekee majimasafi ataona kioo bado baba colin slaa naye karudisha kadi
 
Huyu jamaa juzi juzi tu alikua CHADEMA damu leo ndio imekua hivi tena? siamini kabisa
 
Ni kweli huyu jamaa kavuliwa cheo chake kwani kilikuwa cha muda, anaweza kutimkia magamba wakati wowote na maneno kibao, hasa baada ya kupata zabuni ya kuclear mizigo ya serikali .......
 
Ni kweli huyu jamaa kavuliwa cheo chake kwani kilikuwa cha muda, anaweza kutimkia magamba wakati wowote na maneno kibao, hasa baada ya kupata zabuni ya kuclear mizigo ya serikali .......

Mkuu ebu andika vizuri tukuelewe naona unazunguka tu.
 
Huyu jamaa juzi juzi tu alikua cdm damu leo ndio imekua hivi tena?siamini kabisa

Huyo ndio aliyempokea Lema Uingereza. Nakumbuka Lema alisema jamaa kampa magari matatu pamoja na Chopa.
 
Habari zilizopatikana hivi punde kutoka kwenye vikao vya CHADEMA kupitia Kurugenzi ya Mambo ya Nje, Mwenyekiti wa CHADEMA tawi la London Bwana. Lukosi, amesimamishwa kuendelea kuwa mwenyekiti wa CHADEMA London kutokana na maswala ya kinidhamu.

Inasemekana Bw. Lukosi alienda nchini Tanzania mwezi Septemba mwaka huu na kukutana na wakuu wa Serikali ambapo aliahidiwa kupewa tenda kubwa ya kuclear mizigo ya Serikali. Kutokana na ahadi hiyo Bw. Lukosi alirudi jijini London na kuanza kuivuruga CHADEMA hali ambayo imesababisha kusimamwishwa kwake kuwa mwenyekiti wa CHADEMA -LONDON.

Stay tuned for more details...

good move! Sio kama sisiem diwani aliuza kiwanja cha kilombero ambalo lilikuwa eneo la wazi na stand ya muda huko Arusha badala ya kuwafukuza wamewarudisha kuwa wanachama na hawakuchukuliwa hatua yoyote na mmoja ndie alie ndani ya lile kundi linalojiita wanasisiem waliofungua kesi ya kamanda Lema!
 
Back
Top Bottom