Mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Kinondoni na mjumbe wa Baraza Kuu ahamia ACT

Na Mwanza, iringa, Mbeya, Rukwa, sisi wote ni wa Kaskazini? Hiyo Jiografia yako nadhani ni aheri mtoto wa darasa la nne ana uelewa ulio bora.

Watabakia wakaskazini peke yao kina Kilweo na wenzake, watanzania wanajitambua.
 
Si jambo la kufurahisha kupoteza wanachama au viongozi lakini kama walikuwa vibaraka wa ACT (ambayo pasi na shaka ni tawi la kijasusi la CCM) ni nafuu sana kuondoka kwao wakati huu maana kuvuja kwa pakacha ni aheri ya mchukuzi.

Kamanda naona umeamua kujifariji na kujiliwaza, huku Chadema inazama.
 
Atabaki mbowe na slaa peke yake, wenye kuchanganya na za kwao haoooo
 
BWANA PAUL WAZIRI ALIYEKUWA MJUMBE WA BARAZA KUU LA CHADEMA TAIFA NA PIA MWENYEKITI JIMBO LA KINONDONI AHAMIA ACT-TANZANIA


Bwana Paul Waziri aliyekuwa Mjumbe wa Baraza kuu la Chadema Taifa na pia Mwenyekiti Jimbo la kinondoni.
Na alikuwa Mwenyekiti wa kata ya Mwananyamala.

=====updates
Uongozi mzima wa chadema jimbo la kinondoni waachia ngazi


2 hours ago
ACT yaendelea kuimarika ndani ya Jimbo la Kinondoni.
1.Aliyevaa miwani ni Bwana Karama Kaila aliyekuwa:-
a)Katibu Mwenezi wa Jimbo la Kinondoni CHADEMA (2011-2014 alipojiuzulu pamoja na Bwana Paul Waziri aliyekuwa Mwenyekiti wa Jimbo Hilo)
b)Mjumbe Kamati Tendaji ya Jimbo la Kinondoni.
c)Mwenyekiti wa Bavicha Kata ya Magomeni.


2.Mwingine ni Bwana Moses Raymond aliyekuwa:-
a)Katibu wa Kata ya Mzimuni 2011-2014 alipojiuzulu
b)Katibu Mwenezi Jimbo La Kinondoni (2000-2011)
c)aligombea uenyekiti serikali ya Mtaa wa Kinondoni Shamba mwaka 2004 na 2009 kwa tiketi ya CHADEMA.

Taifa kwanza Leo na kesho.

Huyo jamaa ni tapeli wa viwanja ile mbaya!Kama nakosea muulizeni Mh,Dr.Mdungulile!
 
Kwenda ACT ni sawa na kustaafu siasa tu maana Chama chenyewe kimejifia kabla hata hakijaanza kutambaa...By the way kwa nini hiki chama kimashangilia sana kupata viongozi toka CHADEMA, je ni CHAMA CHA UPINZANI CHA CHAMA CHA UPINZANI?

Adui wa adui yako ni rafiki yako..

Adui wa CDM ni CCM, therefore ACT ==CCM

CDM endeleeni, hawa wenye njaa tushawajua...na wanajua tunawajua...waacheni wahangaike kwanza
 
Watabakia wakaskazini peke yao kina Kilweo na wenzake, watanzania wanajitambua.
Kaskazini imekutoa hapo ulipo,walau umeweza kuandika neno "Kilweo"Hata hivyo si vibaya ukaendelea kujifunza toka kaskazini.
Huyo babu yenu KMKM katuletea janga nchi hii.Hana tofauti na Mangungu!
 
Kwenda ACT ni sawa na kustaafu siasa tu maana Chama chenyewe kimejifia kabla hata hakijaanza kutambaa...By the way kwa nini hiki chama kimashangilia sana kupata viongozi toka CHADEMA, je ni CHAMA CHA UPINZANI CHA CHAMA CHA UPINZANI?
Chadema kubalini chama kinateketea, leo mwenyekiti wa jimbo anaondoka mnajifariji, chukueni hatua jahazi linazama.
 
Mbona hata haonyeshi mashamsham ya furaha kujiunga name easaliti,yuko kama anajistukia.
Kuna kitu hakiko sawa, hata wapambe hamna,kama kashikishwa hiyo bendera.

Huyo bado ana safari hajafka anapoenda kwani hapo alipo hajafka hata nusu ya safari yuko njiani.
 
Hao ndiyo wamefunga rasmi story zao kisiasa ..... RIP guys


CHADEMA ni mpango wa Mungu, itaendelea kuimarika na kuimarika, makapi yatajitenga na ngano safi
 
Hao ndiyo wamefunga rasmi story zao kisiasa ..... RIP guys


CHADEMA ni mpango wa Mungu, itaendelea kuimarika na kuimarika, makapi yatajitenga na ngano safi

unaandika huku nafsi inakusuta....you are too local
 
Back
Top Bottom