Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge Esther Matiko waachiwa kwa dhamana baada ya kushinda rufaa ya dhamana

What is that supposed to mean? embu acheni kufikiri kila mtu anajua hayo mambo yenu ya maigizo huko mahakamani
 
Mimi si Ufipa. Sina unasaba na Ufipa,. Hoja yangu ni wapinzania watendewe haki! Angalia Judgement, Judge amemuumbua huyu fidhuli wa Kisutu (now "Judge" of the high court, , najisi ya High court)
Ukipigwa unaonewa, ukiachwa unaogopwa; ha ha ha kaaz kwel kwel.
 
Mbowe, Matiko warejea uraiani (waachiwa huru)

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na mhazini wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Esther Matiko wamerejea uraiani baada ya kushinda rufaa yao Mahakama Kuu Dar es Salaam.

zaidi soma hapa
Lilikuwa linahitajika limepatikana. Hebu lete video zao wajkati wanaingia na za mwishoni. Wamejifunza, hawatakaa wavunje shr=eria za nchi na kama mnawapenda washaurib=ni hivyo. G Lema na Sugu wameelewa na hawavunji sheria hovyohovyo. Kila nchi ina sheria na hamna aliye juu ya sheria! nina hakika somo limeeleweka!
 
Jaji Rumanyika ni mwislam swala tano haswa. Ana hofu ya kweli ya Mungu si ka Jiwe na uchamumgu wake uvhwara wa kujionesha mbele za watu ili asifiwe. Jaji Rumanyika ni mtu wa haki kwa sababu ni mwislamu wa ukweli! Asante Jaji.
 
Daah kule Si kuzuri kabisa, jambo la heri kama wametoka,ila ni vema wasirudie kosa kama hilo la kuidharau mahakama
 
Maneno ya Jaji Rumanyila sums it all. Hivi hakuna utaratibu wa "kijaji" kuwatia discipline mahakimu wanaokanyaga kwa makusudi haki za wengine left right and center?
 
Jaji Sam Rumanyika Katika kufuta uamuzi wa mahakama ya Kisutu kuwafutia dhamana Freeman Mbowe na Esther Matiko ametaja misingi 9 ya Mahakimu kuzingatia Katika Maombi ya dhamana.

1. Kesi inadhaminika
2. Kutoa dhamana ni tafsiri dhahiri ya mahakama ya dhana ya katiba ya kuwa mtu hana hatia mpaka mahakama itakapomhukumu vinginevyo.
3. Kufuta dhamana kunahitaji sababu kubwa kuliko sababu za kumpa mtu dhamana
4. Mahakama izingatie Ukubwa wa kosa Kutoa masharti ya dhamana
5. Masharti ya dhamana yawekwe bila kuleta hisia kuwa mpango ni kunyima mtu dhamana.
6. Mahakama izingatie adhabu kwa makosa yaliyopo mbele yake ili Pale ambapo mshatikiwa akitiwa hatiani asiwe amedhibiwa mara 2.
7. Sababu ziwe zinakubalika mahakama yeyote duniani
8. Mahakama izingatie Msongamano uliopo gerezani na je kutoa dhamana au kufuta dhamana kunachangia au kupunguza msongamano gerezani
9. Mahakama izingatie kuwa Uhuru ya mshatakiwa hauna mbadala.

Jaji Rumanyika sio tu amewaachia huru Mbowe na Matiko bali pia amefuta masharti ya dhamana ya kuripoti Polisi kila wiki.

Tanzania bado Ina majaji kwa hakika. Mola ampe maisha marefu Jaji Sam Rumanyika
 
Maneno ya Jaji Rumanyila sums it all. Hivi hakuna utaratibu wa "kijaji" kuwatia discipline mahakimu wanaokanyaga kwa makusudi haki za wengine left right and center?
Yule Hakimu amekuwa Jaji

Sent from my TECNO CX Air using Tapatalk
 
Esther Matiko dhamana akipewa atimue mbio akawakumbatie polisi awaombe wampe ulinzi hadi nyumbani huyo mkware Mbowe asije mngangania ukitilia maanani kakaa ndani muda mrefu ana usongo.
Akili za lumumba hizi!!!Wako wapi akina babu seya?Walibaka vitoto na wakasamehewa tena wakakaribishwa na ikulu!
 
Back
Top Bottom