Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kutua Houston Tx USA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kutua Houston Tx USA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkwawa, Aug 14, 2012.

 1. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,290
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 160
  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) anatarajiwa kukutana na Watanzania waishio Houston TX tarehe 25 august 2012 Jijini Houston.
   
 2. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #2
  Aug 14, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,745
  Likes Received: 6,021
  Trophy Points: 280
  Another mistake! Hiyo tarehe ni siku ya sensa, ina maana yeye hatahesabiwa? Kwa mtu mzito kama yeye alitakiwa kuwa mfano tena awe wa kwanza kuhesabiwa katika eneo analoishi/atakaloamkia.

  CHADEMA wanatakiwa kujiepusha na kila hila inayoweza kutumiwa na magamba. Magamba ni lazima wataitumia hii kama turufu ya kisiasa na kwa uelewa wa watu wetu lazima wata-win baadhi. Be careful you guys.
   
 3. t

  thatha JF-Expert Member

  #3
  Aug 14, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Hapo Houston kuna nini, mbona viongozi wa CDM wanapapenda sana? au ndo chimbuko la M4C? inawezekana kuna ukweli ndani ya kauli ya NAPE.
   
 4. t

  thatha JF-Expert Member

  #4
  Aug 14, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Wewe unaelewa sifa mojawapo ya FREEMASONS member?
   
 5. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #5
  Aug 14, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Itafika mahali tumuombe Mungu watu wasife siku ya sensa. Kinachotakiwa ni kuacha kumbukumbu sahihi tu.
   
 6. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #6
  Aug 14, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280

  sensa au ulaji wa magamba?
   
 7. t

  thatha JF-Expert Member

  #7
  Aug 14, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Nadhani anakwenda kumtafuta mtu aliyemvalisha LEMA t-shirt ya CCM. Akicheza naye ataivaa.
   
 8. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #8
  Aug 14, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu sisi tumeambiwa na shekhe Ponda tusishiriki sensa na Mbowe nae kakubaliana na Ponda
   
 9. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #9
  Aug 14, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Unaanza kuleta mambo ya FB? hapa ni JF, mijitu mingine bana... masaburi tupo!
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Aug 14, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kwani tz wote watahesabiwa..?
   
 11. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #11
  Aug 14, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,745
  Likes Received: 6,021
  Trophy Points: 280
  Mkuu mimi nimetoa ushauri tu, sina la zaidi. Nilichosema ni kwamba KWA UELEWA WA WATU WETU hilo laweza kutumika kisiasa. Kuna sababu gani ya ku-commit mistakes halafu baadaye utumie muda mwingi kukanusha au kuelimisha wananchi?

  Vitu vidogo vidogo kama kauli za kawaida (Ref. Nasari and Mzee Mtei), n.k. yamekuwa yakiwagharimu sana CHADEMA. Ni lazima watambue kama kuna "the most wanted either dead or alive" hapa nchini kwa muda huu basi ni CHADEMA.

  Kauli, matendo, na lolote lifanywalo iwe na viongozi au wanachama yanafuatiliwa kwa kila namna ili kutafuta KASORO kwa ajili ya propaganda; na bahati mbaya kwa watanzania tulio wengi kwa hulka ya ushabiki tulio nao, kufuata mkumbo, na uduni wa elimu na uelewa wetu propaganda hizi hukamata wengi.
   
 12. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #12
  Aug 14, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,290
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 160
  Tupe kumbukumbu wamekwenda mara ngapi na ni akina nani??? Tupe hayo matukio kwani nahisi wengi hawayajui.
  Hii M4C moto wake umewaka. Nape msamehe bure lazima afanye kazi ya kueneza uongo na habari za kutunga, dunia ya leo anashindwa nini kusema ukweli, Watanzania wamejaa kila kona ya dunia. Namshauri Nape atambue Watanzania tunashida kubwa ya ukweli kwani waongo na wazushi ndio wanatutesa leo kwa hali mbovu ya uchumi, habari za kuzusha ndivyo walivyoweza kutuibia kwani utu umewaisha, ni waongo na wanaweza kutunga habari yeyote kwa faida ya matumbo yao. Ni vyema vijana tujifunze kuwa wakweli.

  Sensa huwa wanahesabu kwa kaya na kama sikusei dodoso linajazwa na mtu mmoja kwenye kila kaya baba au mama. Sensa ya makazi sidhani kwamba wanavizia watu barabarani. Wahesabu watu huenda kwenye kila nyumba na kutaka kujua hiyo nyumba ina watu wangapi wanaoishi humo.

  Wataalamu wa sensa wanajua kuna watu huwa wapo safirini, masomoni nje ya nchi, matibabu nje ya nchi na kadhalika. Swala kubwa nikuhakikisha huhesabiwi mara mbili ndani ya Tanzania, ila kila kaya itahesabiwa mtu. NB nenda kwenye web ya sensa na angalia madodoso utaona jinsi ya kujaza na jinsi sensa itakavyoendeshwa.
   
 13. i

  iseesa JF-Expert Member

  #13
  Aug 14, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mistake iko wapi sasa? wewe unataka nchi itlulie tuli hiyo siku hata wanaotaka kusafiri (kwa mfono kwenda kwenye matibabu) wasisafiri? hayo ni mawazo finyu.
   
 14. N

  NG'ONGOVE Senior Member

  #14
  Aug 14, 2012
  Joined: Apr 28, 2012
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mtu anaruhusiwa kusafiri siku hiyo kikubwa akumbuke kuacha taarifa zake muhimu
   
 15. MARCKO

  MARCKO JF-Expert Member

  #15
  Aug 14, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 2,265
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  acha uoga. Mwache jamaa aende. Kuna mke wake nyumbani, atatoa data.
   
 16. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #16
  Aug 14, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,745
  Likes Received: 6,021
  Trophy Points: 280
  Inaonekana hatuelewani au inaoenekana napinga safari ya Mbowe. Hamjaelewa repercussion ya hiyo safari ya Mbowe kisiasa. Chama kijiandae kutumia muda mrefu kwa ajili ya utetezi na kupambana na propaganda chafu badala ya kujikita kwenye mambo mengine.
   
 17. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #17
  Aug 14, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Liwalo na liwe, swala la ukombozi wa nchi hii ni mhimu sana kuliko hiyo Censer Mkuu dudus.
   
 18. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #18
  Aug 14, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,745
  Likes Received: 6,021
  Trophy Points: 280
  Mkuu nakubaliana sana na wewe. Tatizo ni tafsiri ya neno "mtu". Mbowe ni "special" mtu na kila afanyalo lina athari kubwa kwa chama either positively or negatively na adui daima hupenda kutumia mianya ya kipuuzi kama hii; sote tunajua siasa za nchi yetu.

  Sensa ni jambo kubwa hutokea mara moja kila baada ya miaka kumi zaidi hata ya uchaguzi mkuu. "Ingekuwa Uchaguzi Mkuu angeenda Marekani?"; adui atahoji na wengi watamwamini! Ingekuwa ni mimi au "mtu" mwingine wa kawaida kasafiri wala tusingejali au kuhoji lakini sio Mwenyekiti. Huyu ana nafasi ya pekee na adhimu - kila mtu anamtazama na kufuatilia nyendo zake akiwepo adui!
   
 19. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #19
  Aug 14, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 4,914
  Likes Received: 5,351
  Trophy Points: 280
  mawazo kama yako ndio wayatumiayo ccm. Kwani taratibu za sensa zinasemaje?? Acha kutishwa ni mengi yatasemwa na kunenwa na kutendwa ila ukweli utabakia palepale.kwani ni lazima kila raia wa tanzania aandike kwa mkono wake juu ya kuhesabiwa??? Kama ni NO basi mbowe hana kosa lolote?? Wewe unako elekea utaogopa kivuli chako mwenyewe ???
   
 20. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #20
  Aug 14, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Safari njema kamanda mkuu, sauti ya zee, mzee wa anga...We are supporting you, M4C mpaka kieleweke!
   
Loading...