Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau amani iwe kwenu.
Mpaka sasa, jumla ya wabunge saba wa CHADEMA wamesimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge kwenye mkutano huu wa bunge la bajeti unaoendelea. Wabunge waliosimamishwa kuhudhuria vikao hivyo ni John Heche, Halima Mdee, Tundu Lissu, Pauline Gekul, Ester Bulaya, Anatropia Theonist pamoja na Suzan Lyimo. Mbunge mwingine aliyekumbwa na adhabu ni Zitto Kabwe ambaye naye ni mtoto wa Freeman Mbowe kupitia CHADEMA ambaye kwa sasa yupo ACT. Wabunge hao wamesimamishwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kukiuka kanuni za bunge pamoja na kusema uongo bungeni huku wakishindwa kuthibitisha kauli zao.
Kwa kawaida, ukiona familia moja inakuwa na watoto wengi watovu wa nidhamu na wenye kila aina ya uovu, basi ujue tatizo lilikuwa ama lipo kwa wazazi. Wazazi ndio wanaotoa mwelekeo wa aina ya watoto wao watakavyokuwa. Kama mzazi ni mlevi muda wote basi kuna uwezekano mkubwa wa watoto wake kukosa malezi bora. Vivyo hivyo kama mzazi ni changudoa.
Binafsi siamini kuwa UKAWA ndio inayozaa malezi mabaya ya wabunge wa CHADEMA mpaka kuadhibiwa bungeni. Kwani UKAWA inaundwa na vyama vinne ambavyo ni CHADEMA, CUF, NCCR MAGEUZI na NLD ambayo haina uwakilishi bungeni. Hata hivyo, kati ya vyama hivyo, ni wabunge wa CHADEMA tu ndio ambao wamekuwa wakikumbwa na adhabu mbalimbali bungeni. Sijapata kusikia mbunge wa CUF ama James Mbatia wakikumbwa na adhabu za aina hiyo.
Kwa vile ni wabunge wa CHADEMA pekee ndio wamekuwa wakikumbwa na adhabu, nashawishika na naamini pia na wewe msomaji unashawishika kuamini kuwa wabunge hao wanakosa malezi bora kutoka kwa mzazi wao CHADEMA chini ya Mwenyekiti Freeman Mbowe.
Ni wakati sasa wa wadau mbalimbali kumsaidia Mbowe kuwalea watoto wake kwani kwake malezi yamemshinda.