Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe atuma Salamu za rambirambi kufuatia Msiba mzito wa Rais Magufuli

Mbowe kwenye busara namkubali, huwa hanaga paapara kabisa na mdomo wake una break.
Ila aache kung'ang'ania uenyekiti, miaka 20 wewe tu utafikiri HAKUNA wengine
"---ila aache kung'ang'ania uenyekiti,----".

Inawezekana ukawa sawa, kama wewe ni mgeni Tanzania.

Je, inawezekana uwepo wa CHADEMA, kama ilivyo sasa, katika hali ngumu kabisa iliyokikabiri chama katika miaka mitano iliyopita huenda ingekuwa ni tofauti kabisa na iliyopo sasa?

Hili ni swali tu, hata wewe unaweza kujiuliza na kulijibu kivyako!

Mimi nadhani CHADEMA, kama ingebahatika kuendelea kuwepo kama chama, hali yao ingekuwa ni tofauti sana chini ya uongozi wa mtu mwingine mbali ya Mbowe.

Usinielewe vibaya. Sisemi kamwe kwamba hakuna viongozi wengine ndani ya CHADEMA, ambao pengine ni imara zaidi na hata kuwa bora zaidi ya Mbowe; lakini wakati CHADEMA ilipopata dhoruba kali, ilibahatika sana kuwepo na Kiongozi imara kama Mbowe.

Bila shaka, kama dhoruba lile litakuwa limepita, inawezekana sasa hata Mbowe mwenyewe na chama chake wakawazia jambo la kupata uongozi mpya.
Huo utakuwa ni uamzi wa wanachama wao, na sio shurti kutoka nje.
 
Mimi nimo ndani ya chama
 
Miaka 20 kwenye uenyekiti ni mingi Sana.
Ila namkubali ana busara Sana na pia Sio mropokaji
As long as hajaua, hajateka, hajatesa, havunji katiba, hapori mali za watu na wala hajawahi kupoteza watu mwache aendeshe chama hata miaka 100.
 
Tanzania flag-XXL-anim.gif

Katiba Mpya Tume HURU ya Uchaguzi kuachiwa wafungwa wote wa Kisiasa wakiwamo Mashekhe kuachiwa kwa wafungwa wa kubambikiziwa kesi akiwemo Mdude Nyagali na wale waliobambikiziwa kesi za uhujumu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom