Mwenyekiti wa chadema aliyetimuliwa monduli akwamisha mkutano wa chama

THINKINGBEING

JF-Expert Member
Aug 9, 2010
2,779
1,304
Amani Silanga aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Monduli amekwamisha mkutano wa chama hicho uliokuwa ufanyike kesho tarehe 3/12/2013.
CHADEMA wilaya walipeleka barua ya kulijulisha jeshi la polisi kuhusu mkutano huo siku ya jumapili tarehe 1/12/2013.Hata hivyo viongozi wa CHADEMA walipokwenda polisi kupokea majibu ya barua yao walikutana na kikwazo cha kwanza kwamba ETI viwanja vya sokoni walivyoomba kufanyia mkutano kuna tawi la CCM hivyo hawataruhusiwa kufanyia mkutano wao hapo.
Baadae viongozi wa CHADEMA walipendekeza kiwanja kilichopo karibu na jeshi hilo lakini walikataliwa bila kupewa sababu yoyote.
Hata hivyo baada ya majadiliano ya muda mrefu walikubaliana kwamba mkutano huo ukafanyikie kwenye viwanja vilivyopo karibu na ofisi za CHADEMA.
Katika hali ambayo haikutarajiwa viongozi wa CHADEMA wakiwa katika maandalizi ya mkutano huo waliitwa tena kituo cha polisi na kujulishwa kwamba aliyekuwa mwenyekiti wao(aliyetimuliwa)naye ameenda kuomba kufanya mkutano siku hiyohiyo kwani yeye bado ni mwenyekiti halali wa CHADEMA.

Polisi walidai mwenyekiti huyo amewaweka njia panda kwani hawajui wamsikilize nani kwakuwa mwenyekiti huyo aliwahoji polisi kama wana barua yoyote inayoonesha kama amesimamishwa jambo ambalo jeshi la polisi limekiri kutokuwa na barua hiyo na hivyo kuzuia mkutano huo mpaka barua hiyo itakapoletwa.

Kitendo cha CHADEMA mkoa kutopeleka barua ya kumsimamisha kiongozi huyo kimewasononesha sana wapenzi,washabiki na wanachama wa chama hicho wilayani Monduli kwani kinaonekana kama ushindi mkubwa kwa mwenyekiti huyo aliyepanga kuwakomoa.
 
Mwaka 2013 tunauhitimisha kwa kuona mengi, halafu ni mwaka usiogawanyika na hivyo kukosa alternative.

Huu mwaka huu....2013 !?!?
 
hapo ni namna tu ya kuwataarifu wana CDM kiustraabu kuwa kile kikao kimeshindikana kufanyika -wanaume wamegoma, unadhani M/kiti ana nguvu kuliko wanachama? mara ohhhh walisahau kumkabidhi barua ya kumsimamisha uongozi-inaingia akilini kweli? AIBU HIYO , Ziara zote mtaahirisha za SLAHA
 
Ni vizuri huyo mwenyekiti ameonyesha rangi zake halisi. Hamkini taratibu zitawekwa sawa
 
1.Tumeahirisha mkutano hadi Alhamis wala sio kwa ajili ya huyo mwenyekiti aliyesimamishwa,hata hivyo tayari ameshakabidhiwa barua yake ya kujulishwa maamuzi ya chama
 
kwani taratibu zinasemaji juu ya utoaji wa taarifa za mikutano? Kwani ni nani alitangulia kutoa taarifa ya huo mkutano kati yao?
 
Back
Top Bottom