MWENYEKITI WA CCM SINGIDA NARUMBA HANJE, AISHAMBULIA CHADEMA... kwa Kutumia kitabu cha dini

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
** Why is this CCM now they have to use religious books to prove it's existance? “The trouble ain't that there is too many fools, but that the lightning ain't distributed right!!!


Na Nathaniel Limu-Singida.

Mwenyekiti wa CCM Singida vijijini Narumba Hanje, amekitabiria Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwamba hakitaingia Ikulu milele kwa madai kuwa kimepoteza mwelekeo baada ya kuanza kutumia mbinu chafu ambazo hazitawasaidia kufikia lengo lao.

Hanje ametoa utabiri huo wakati akifungua mkutano mkuu wa Jumuiya ya umoja wa vijana (UVCCM) uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa shirika la Pride Singida Mjini.

Alisema CHADEMA sasa kimeacha kuwaeleza wananchi kitawafanyia nini ili waweze kuleta maendeleo endelevu, na badala yaje kueneza fitina, hasira, uadui, uzushi.

Aidha, Hanje amedai kuwa Chama hicho kimeundwa, ‘kiundugunaizesheni’ na kwamba hakina demokrasi na kuwa na mwonekano wa taasisi binafsi, na kuongeza kuwa kimepoteza muda mwingi kwa kuzunguka na kufanya maandamano ambayo hayana tija kwa wananchi.

Mwenyekiti huyo amedai chama hicho kimeonyesha dhahiri kwamba hakiwatakii mema Watanzania baada ya kuanza kuwadanganya na kuwashawishi wasichangie maendeleo kwa madai kwamba jukumu la kuleta maendeleo ni la serikali pekee.
“Sisi hapa mjini, tunachangia mambo mengi hata ya uzoaji wa takataka, sembuse maendeleo”, alihoji na kuongeza “CHADEMA hawana ubavu tena wa kuchukua nchi, wamepoteza mwelekeo, wamefikia mahali wanaifananisha Tanznaia na Misri”.

Hanje alisema CHADEMA ni ya kuogopwa kama ukoma, kwa madai kwamba viongozi wa chama hicho,wanatumia nafasi zao kujaza watu wa ukoo wao katika nafasi mbali mbali za uongozi.

Katika kuujengea nguvu utabiri wake huo, mwenyekiti huyo alisoma Agano jipya kitabu cha Wagalatia 5 mstari mdogo kuanzia 19-21.

Pamoja na mambo mengine, mistari hyo inasema ‘Fitina, wivu, hasira, husuda na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo, nawaambia kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo, hawataurithi ufalme wa Mungu.’



Mwenyekiti wa CCM Singida vijijini, Narumba Hanje akisoma Agano jipya kitabu cha Wagalatia mbele ya mkutano mkuu wa UVCCM Singida vijijini juzi.

Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa UVCCM​
 
Tunaelekea kubaya kweli kutumia Vitabu vya Dini kuambatanisha na Siasa zetu...

The more man clings to religion, the more he believes. The more he believes, the less he knows. The less he knows, the more stupid he is. The more stupid, the easier he can be governed! The easier to govern, the better he may be exploited. The more exploited, the poorer he get he become a fanatic... fanatism is the worst type of religious people they become zeal....
 
Aisee anguko la CCM limetimia,hao wazeee watano ndiyo vijana,tena huo ndiyo umati,kazi ipo watu wa magamba
 
Anahutubia viongozi wa Ccm,tena ndani ya ukumbi(wana uhakika wote waliomo humo ni watu wao)anaacha kuongea mambo ya ccm,anaongelea Cdm,kweli akili hipo hapo?
 
huyo mwenyekiti mwenyewe ni fisadi wa kutupwa na hafai kabisa katika jamii na hata c.c.m wilaya ya singida vijijini anakifanya kama mali yake na wateule wachache hivyo jinsi ya kuwasema wengine.
 
Aisee anguko la CCM limetimia,hao wazeee watano ndiyo vijana,tena huo ndiyo umati,kazi ipo watu wa magamba

Ndugu hao si wazee!!\
Ni vijana waliokamuliwa na akina Chiligati hadi kuonekana wazee!!
Hata weye ukipigika utaonekana kibabu!
 
Naona umati ulivyofurika na kusikiliza kwa makini na bashasha!

Kwa vile mmezoea mikutano ya hadhara basi mko busy kuangalia idadi ya watu hata kama mkutano wenyewe ni wa ndani. Imeelezwa kwamba huo ni mkutano wa UVCCM. Suala la umri kwa kuangalia maumbo ya watu, siyo kigezo pekee. Lakini hoja aliyoitoa si ndiyo ya kuijadili?
 
huwezi kujadili hoja isiyokuwa na mshiko na iliyotolewa na mtu asiyefikiri na mwenye kukata tamaa
 
kwa hiyo kabla ya kutamka hayo alikuwa ana amini chadema wataingia ikulu na wana uwezzo wa kuongoza nchi? Lakini kwa sasa wamepoteza dira? Ah ah ah ah huyu mwenyekiti akili zake aziko sawa nasikia ni gamba gumu san ambalo alitawezekanika kuvuliwa ajue ss chadema tuko makini kuliko anavyo dhani pole yake
 
Katika picha ni yeye pekee mnene wengine wamekonda ruziku zinawafikia huko au ni yeye anavimbiana ?
 
Ama kweli chadema inawatesa, kwa hali hii itaendelea kuwatesa vilivyo. Inawezekanaje katika mkutano wa wajumbe wa chama munaongelea mambo ya chama kingine. Sijui kama wamemwamini. Hao jamaa walifuata mshiko kwa kudhani watapewa kama walimu walivyopewa.

Dua la kuku!
 
Kashindwa kuvua gamba.
Anatafuta mchawi.mchawi wa gamba yumo ndan ya gamba.acha kutumia maandikoo kuficha magamba.
 
Kwa vile mmezoea mikutano ya hadhara basi mko busy kuangalia idadi ya watu hata kama mkutano wenyewe ni wa ndani. Imeelezwa kwamba huo ni mkutano wa UVCCM. Suala la umri kwa kuangalia maumbo ya watu, siyo kigezo pekee. Lakini hoja aliyoitoa si ndiyo ya kuijadili?

Duh hii kali!! ndani ya mkutano wa UVCCM (wa ndani) jamaa anajadili sera za CHADEMA?? Halafu hizo sura za hao jamaa zinaonesha wameshajikatia TAMAA.. wanatia hata huruma na hawamuelewi huyo jamaa anaongea nini?
 
ON LINE KABISAA KWA HILI , CCM & CDM (Christian Democratic Part) , HAWAJUI KUTUMIA MUDA ,WAKATI WA KUTAFUTA KURA WAMEPIGA KAMPENI, WAKATI WA KUTANGAZA MATOKEO WANAENDELEA NA KAMPENI , MUDA WA UTEKELEZAJI WAO NI KAMPENI TUU ! LOL, KAZI WATAFANYA SAA NGAPI ? AU TUMEWACHAGUA ILI WARUMBANE ? IT WIL BE GUD WAKIUNDA VIKUNDI VYA TAARAB , KIMOJA KIWE CCM STARS NA KINGINE KIWE CDM MODERN TAARAB THEN WASHINDANE KURUSHA VIDOLE JUU ! WENYE UBONGO KICHWANI WATAELEWA , WALIO NA TOPE KICHWANI WATALEWA TUU !
 
Back
Top Bottom