Mwenyekiti wa CCM Singida amtoza Mwanafunzi faini ya 200,000 kwa kufanya ngono

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
ZUBERI Manjemi, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Manyoni mkoani Singida amemtoza faini ya Sh. 200,000 mwanafunzi wa kike wa Darasa la Nne kwa madai ya kufanya ngono.

Hatua ya mwenyekiti huyo kumtoza fedha binti huyo imezua mjadala Manyoni kwa madai, amekwenda kinyume na taratibu katika kukomesha tabia ya watu kufanya ngono na wanafunzi.

Hata hivyo, Mhandisi Mathew Mtigumwe, Mkuu wa Mkoa wa Singida ameliagiza Jeshi la Polisi wilayani Manyoni, Singida kumkamata mara moja mwenyekiti Manjemi.

Mhandisi Mtigumwe ametoa agizo hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika Kijiji cha Rungwa, Tarafa ya Itigi, Manyoni baada ya mwananchi Ally Ramadhani kutoa malalamiko yake kwamba, Manjemi ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la usuluhishi la kata hiyo kwenda kinyume na taratibu.

Akifafanua zaidi Ramadhani amesema kuwa, kitendo cha mwenyekiti huyo kumtoza binti adhabu ya faini ya Sh. 200,000 na kutokuchukua hatua zo zote za kisheria dhidi ya mkazi aliyekuwa akituhumiwa kuwa na uhusiano wa kingono na mwanafunzi huyo, hakikuwa sahihi.

“Mkuu wa Mkoa adhabu hii ya upande mmoja haivumiliki kabisa, kwani mwanaume ambaye alikuwa akimrubuni mwanafunzi wa kike kufanya naye mapenzi ameachwa huru bila kupewa adhabu yote yote ile,” amesema kwa masikitiko.

Mkuu wa mkoa huyo alipomtaka Manjemi kueleza sababu ya kumtoza faini binti alisema kwamba, alitoa adhabu hiyo kwa madai binti huyo alitenda kosa kwa kukubali kupokea simu ya kiganjani kutoka kwa mwanaume, ili waweze kufanikisha mawasiliano ya kimapenzi.

Hata hivyo, baada ya maelezo hayo ya utetezi, ndipo Mkuu wa Mkoa alipomuagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo kumkamata na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

“Haingii akilini eti mwanafunzi wa kike atozwe faini huku mtu aliyekuwa akimrubuni anaachwa bila kuchukuliwa hatua zo zote za kisheria,” amesisitiza Mhandisi Mtigumwe.

Mhandisi Mtigumwe amesema kuwa, serikali imekuwa ikijitahidi kuhakikisha wanafunzi wa kike wanafikia ndoto zao za kielimu lakini baadhi ya wanaume wakiwemo viongozi,wamekuwa vikwazo dhidi ya juhudi za serikali.

Mtigo ulivyokuwa; Baada ya walimu wa Shule ya Msingi Rungwa kutilia wasiwasi kuhusu umiliki wa simu ya mkononi ya mwanafunzi huyo, walimuhoji ambapo binti huyo alikiri kuhongwa.

Kisha walimu hao walimtaka mwanafunzi huyo kumpigia simu aliyempa simu hiyo ili kusikiliza mwenendo wa mazungumzo yao.

Mwanafunzi alifanya kama alivyoagizwa na walimu wake na ndipo walipobaini mwanaume huo kupokea na kuzungumza maneno ya mahaba kwa mwanafunzi huyo.

Baada ya hapo walimu hao walichukua namba ya simu ya mwanaume huyo na kuifikisha katika Baraza la Kata kwa hatua zaidi.

Chanzo: Mwanahalisi Online
 
Sasa wakuu wa namna hii ukiwachapa mbele za watu kutakuwa ni kosa la uvunjifu wa haki za binadamu?
Watendaji wa dizaini hii wana komaa sura na mwili lakini akili bado zi changa
 
Mwenyekiti wa CCM wa Manyoni mkoani Singida ndiye kapiga faini ya 200000/=......Siyo kweli.....CCM chama tawala...chama kongwe...chama makini....viongozi shapu....narudia siyo kweli au weka picha ya Mwenyekiti kavaa shati lake la kijani tuone.
 
kama ni kweli jinga kabisa ilo maana ana halalisha katoto kaendelee kugegedwa na uyo jamaa kwani ndo kwenye uwezo kumlipia iyo faini. Afungwe tu ili wababe wakamzibue chemba
 
Sishangai mana hata maauz mengne wanayofanya maboc wake n pumba tupu
 
Hii habari ilirushwa na kituo cha ITV ijumaa iliyopita, ilikuwa itigi
 
Hilo mbona kwa CCM ni jambo dogo sana maana Kilolo wanakusanya ushuru kwenye vilabu wakati ni vya serikali.
 
Anatuletea mambo ya uharabuni hapa. Mwanamke anaripoti polisi kuwa amebakwa matokeo yake mlalamikaji anawekwa ndani akisubiri kesi ya "kufanya uzinzi" huku mbakaji wala hatafutwi na hawana haja naye.
 
Back
Top Bottom