Mwenyekiti wa CCM Shinyanga kuvaa gwanda? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenyekiti wa CCM Shinyanga kuvaa gwanda?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KIMOSTODO, Jun 1, 2012.

 1. K

  KIMOSTODO Member

  #1
  Jun 1, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Hamis Mngeja, amewashukia wasomi hapa nchini kwa kuendekeza mambo ya semina, makongamano, warsha pamoja na tafiti mbalimbli huku wakiiacha nchi ikiendelea kudidimia kiuchumi.

  Mngeja ambaye pia ni Kaimu Mwenyekiti wa Shirika lisilo la Kiserikali la Mzalendo Foundation, aliiambia Tanzania Daima kuwa baadhi ya wasomi wameshindwa kutumia utaalamu wao kulisaidia taifa hususan kuinua maisha ya wakulima ambao sasa wanakandamizwa.

  Alisema mfumo wa bei za mazao ya wakulima katika masoko haueleweki na kusababisha kuyumba kwa bei ya mazao kila wakati na kusababisha mkulima badala ya kunufaika na bei inamdidimiza.

  Mgeja alimwomba Waziri wa Kilimo Christopher Chiza kusikia kilio cha wakulima wa mazao hususan yale ya biashara ambayo yamekumbwa na mtikisiko wa kuporomoka kwa bei mara kwa mara.

  Aliitaka serikali kujielekeza katika kulinda viwanda na kutumia malighafi za ndani badala ya kupeleka nje ya nchi jambo linaloyanufaisha mataifa mengine.

  Alisema kuwa ikiwa taifa litawekeza kwa wingi katika viwanda vya ndani uchumi wa nchi utakuwa imara na thamani ya kilimo itapanda na kupendwa na kila mtu kwa sababu ndio njia pekee anayoamini itawasaidia wananchi kuondokana na umaskini walionao
   
 2. Ditto

  Ditto Member

  #2
  Jun 1, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Habari yako haifanani na kichwa chako cha habari.. Jipange mkuu
   
 3. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,808
  Likes Received: 1,122
  Trophy Points: 280
  Kila kitu sasa hivi ni kuvua gamba?.
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Huyo mwenyekiti wa ccm Shinyanga anataka tuamini hali tuliyonayo nchi hii imesababishwa na wasomi? kwamba warsha, makongamano etc ndio kiini cha matatizo yetu?
   
 5. Shixi889

  Shixi889 JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 322
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  propaganda nyingine hovyo jipange mkuu acha kukurupuka!!!!!!!au badili hiyo heading.
   
 6. K

  KIMOSTODO Member

  #6
  Jun 1, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ibadilishe wewe mkuu hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 7. K

  KIMOSTODO Member

  #7
  Jun 1, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  sahihi sasa weka ya kwako halafu iokosoe hahahaaa
   
 8. r

  ralphjn Senior Member

  #8
  Jun 1, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Haijaeleweka.Info ulizotoa hazina uhusiano na kuvaa Gwanda
   
 9. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2012
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,806
  Likes Received: 1,053
  Trophy Points: 280
  watu wanaweweseka na gwanda hata ukiulizwa jina lako nani utasema gwanda
   
 10. Mpangamji

  Mpangamji JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2012
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 536
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Huyu jamaa niliwahi kumsikia kwa masikio yangu akilalamikia shule za kata kuwa zitasababisha Magamba wapate shida kwa kuwa zinawapa watu wengi sana ufahamu hasa hasa vijana. hayo maneno nayoyasema ni usanii tu
   
 11. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #11
  Jun 1, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
 12. Ng'wamapalala

  Ng'wamapalala JF Gold Member

  #12
  Jun 1, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 6,332
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 145
  Yeye ndiyo anakiua Chama mkoani kwa kuendekeza majungu na fitina. Ama kweli, nyani haoni kundule.
   
 13. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #13
  Jun 1, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,611
  Likes Received: 4,719
  Trophy Points: 280
  Hatumtaki yuko kwenye payroll ya EL.Huyu gamba lake ni gumu mno kuvuka abakie huko huko.
   
 14. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #14
  Jun 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Pamoja na Habari kuwa Si Sawa huyu Jamaa ni Mpenda Maraha - Fisadi; na Rafiki ya Mbunge wa Shinyanga Mjini Ambao

  Walichakachua Kura na kumshinda aliyekuwa anagombea wa CHADEMA ambaye nadhani sasa ni Marehemu; kwahiyo

  Sidhani CHADEMA itapokea bila kuangalia historia ya hao watu; Na Ni kibendera cha Majungu NEC ya CCM
   
 15. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #15
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,999
  Likes Received: 37,703
  Trophy Points: 280
  Mbona haongelei safari za raisi!Safari za raisi nazo ni kama mchwa kwenye hazina ya taifa.
   
Loading...