Mwenyekiti wa CCM na rais mstaafu mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ziarani nchini China

Peter Dafi

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
389
272
MWENYEKITI WA CCM NA RAIS MSTAAFU MHE. DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE ZIARANI NCHINI CHINA.

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi {CCM} na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete yuko nchini China kwa ziara ya kikazi ya siku sita (6) iliyoanza Aprili 17 mpaka April 23, 2016.

Ziara hiyo ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi inafuatia mualiko rasmi kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CCP) na Rais wa China Mheshimiwa Xi Jinping. Akiwa nchini China, anatarajia kukutana na viongozi wa juu wa Chama Cha CCP na viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na kufanya nao mazungumzo yanayolenga kuimarisha uhusiano kati ya CCM na CCP na serikali za nchi hizo mbili ulioasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere na Muasisi wa Taifa la China Mwenyekiti Mao Tse Tung.

Mhe Kikwete anatarajia kutembelea Jimbo la Fu Zhou, jimbo ambalo Rais wa sasa wa China amefanya kazi zake za siasa kwa miaka 18, zilizompatia umaarufu na uaminifu kwa watu wa China na kupelekea kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCP na Rais wa China.

Katika ziara hiyo Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ameongozana na wajumbe watatu wa Kamati Kuu Mhe Abdallah Bulembo, Dkt Maua Daftari na Mama Zakhia Meghji. Pia ameongozana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Dkt Titus Kamani, Mwenyekiti wa Wilaya ya Mkalama Dkt Charles Mgana na maafisa wawili wa Ofisi za Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi.
 

Attachments

  • 1461143667834.jpg
    1461143667834.jpg
    55.6 KB · Views: 92
  • 1461143695868.jpg
    1461143695868.jpg
    48.9 KB · Views: 79
  • 1461143715844.jpg
    1461143715844.jpg
    53.8 KB · Views: 82
Historia ya China na Tanzania haijaanza na Jakaya tu Mkuu Obama!

Urafiki huu tangu Enzi za Mwalimu na Mao
 
Inamaana kaonganisha juu kwa juu?napata ukakasi kama huyu jamaa kweli ni patriotic.HB wa msoga buana
 
Mwenyekiti tunategema busara zako katika kuboresha na kudumisha uhusiano mzuri na ndugu zetu wa Jmahuri ya watu wa China uliokuwepo kwa miaka kadhaa tokea mwanzo wa kuanzishwa kwa taifa hili.
 
hii inaewafaa wana CCM.. me napita tu,wengine wakija hapa kuchangia utaingia mitini soon coz huyu mzee watu bado wana hasira nae,katutia ulofa kiasi flani.... wizi, ubadhirifu, ufisadi, rushwa, income inequality, madawa ya kulevya, raia kunyanyaswa na mamlaka za serikalini, umungu mtu ktk taasisi za umma na uozo mwingine.. JK, the founding father.. hivi kweli viongozi wliotangulia walikuwa na watoto mapusha? nani? Nyerere,Mwinyi au Mkapa? Thubutuuu!!!!!!!!! imeeleweka...
 
Back
Top Bottom