Mwenyekiti wa CCM na mkakati wa kumdhibiti Dr Slaa

Joblube

JF-Expert Member
Mar 4, 2011
369
151
Kwa wiki hizi mbili mfululizo kutokana na matamshi ya viongozi mbalimbali wa CCM nimeweza kugundua kuwa CCM sasa wanajua kabisa kuwa hawana mtu ambaye anaweza kupambana na Dr Slaa iwapo atateuliwa na CDM kuwania tena urais 2015 hata kwa kuchakachua, hii nikutokana na hasira, uelewa wa Watanzania kwa sasa.

Kwa kutambua hilo na kwa kujua kuwa sasa hivi wao sio wamoja na hamna dalili za kuwa wamoja Mwenyekiti wa CCM anapanga mpango wa kumteua mgombea mwanamke hasa Dr AshaRozi Migiro ili kwatumia wanawake waliowengi kuwarubuni wapiga kura.

Hii ni nimeiona kuanzaia wiki hii ambapo watu wa karibu na Mwenekiti huyo (Mama Sofia Simba, Mama Salma Kikwete) wakinenA kuwa sasa ni zamu ya Rais mwanamke, naona mbinu hii nikama ile iliyotumika kumwengua Samweli Sita kuwania Uspika.

Katika hili viongozi wa CCM wako radhi kuungana pale penye hatari ya CCM kupoteza uongozi wa nchi kwa kuwa wanacho ogopa wao sii CCM kushindwa bali yale machafu waliofanya (Kagoda,Meremeta, Rada) kuwekwa wazi na viongozi wa chama kingine ndio maana wako radhi kutumia hata mabomu kuutafuta uongozi.

Kumbuka usemi wa hakuna aliyemsafi ndani ya CCM. Wadau mnasemaje kuhusu mbinu hii mbadala?
 
Dullo

JF-Expert Member
Oct 24, 2009
251
64
Kinachosubiriwa ni muda tu, safari ya CCM kubakia kuwa historia umefika.
 
Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
409
Sasa unachukia nini? Kwani kuna dhambi gani kwa chama kupanga mikakati ya ushindi katika uchaguzi kwa kuangalia kutoka miongoni mwa kadi zake ni yupi anayeweza kuwa chaguo bora la kupambana na whoever atakayepitishwa na washindani wengine? Nilidhani kuna mikakati haramu kumbe ni yale yale ambayo yanafanywa na kila chama kilicho hai na chenye nia ya kushika dola. Afterall, unajuaje kama Chadema watampitisha Slaa kuwa mgombea wake? Kwanza umri wake umeshaenda sana na tunakoelekea huko turufu ya generational change au gender inaweza kuwa na mashiko.
 
Vin Diesel

JF-Expert Member
Mar 1, 2011
9,095
6,321
Hizi habari za kutungia kwenye keyboard zachekesha sana...eti hakuna msafi ndani ya CCM...says who?
 
Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
409
Halafu unajiuliza kama ni lazima mtu u-post thread kama hujui unachosema.
 
HISIA KALI

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
694
108
Kwa wiki hizi mbili mfululizo kutokana na matamshi ya viongozi mbalimbali wa CCM nimeweza kugundua kuwa CCM sasa wanajua kabisa kuwa hawana mtu ambaye anaweza kupambana na Dr Slaa iwapo atateuliwa na CDM kuwania tena urais 2015 hata kwa kuchakachua, hii nikutokana na hasira, uelewa wa Watanzania kwa sasa.

Kwa kutambua hilo na kwa kujua kuwa sasa hivi wao sio wamoja na hamna dalili za kuwa wamoja Mwenyekiti wa CCM anapanga mpango wa kumteua mgombea mwanamke hasa Dr AshaRozi Migiro ili kwatumia wanawake waliowengi kuwarubuni wapiga kura.

Hii ni nimeiona kuanzaia wiki hii ambapo watu wa karibu na Mwenekiti huyo (Mama Sofia Simba, Mama Salma Kikwete) wakinenA kuwa sasa ni zamu ya Rais mwanamke, naona mbinu hii nikama ile iliyotumika kumwengua Samweli Sita kuwania Uspika.

Katika hili viongozi wa CCM wako radhi kuungana pale penye hatari ya CCM kupoteza uongozi wa nchi kwa kuwa wanacho ogopa wao sii CCM kushindwa bali yale machafu waliofanya (Kagoda,Meremeta, Rada) kuwekwa wazi na viongozi wa chama kingine ndio maana wako radhi kutumia hata mabomu kuutafuta uongozi.

Kumbuka usemi wa hakuna aliyemsafi ndani ya CCM. Wadau mnasemaje kuhusu mbinu hii mbadala?

Wakiweka mwanamke tu ndio mwisho wa CCM Ikulu. Kuna ushahidi wa kimazingara unaoonyesha kuwa wanawake hawapendi kuwachagua mwanamke mwenzao wakati anapokuwa anagombea na wanaume. Tena hii huwa inatokea sana kwenye jamii ambayo inaamini mfumo dume. Jamii ya Tanzania ina amini sana mfumo dume.
 
Tony Almeda

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
397
122

Wameweza Kawe tu.
 
Arafat

JF-Expert Member
Nov 17, 2009
2,582
755
By the way wanatumia katiba gani na sheria ipi kusema hayo?

Au Yahya amewapa urithi wake!
 
mikatabafeki

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
12,790
4,621
Wakiweka mwanamke tu ndio mwisho wa CCM Ikulu. Kuna ushahidi wa kimazingara unaoonyesha kuwa wanawake hawapendi kuwachagua mwanamke mwenzao wakati anapokuwa anagombea na wanaume. Tena hii huwa inatokea sana kwenye jamii ambayo inaamini mfumo dume. Jamii ya Tanzania ina amini sana mfumo dume.
hata wakiweka mwanaume sidhani ka 2015 sisiem wana chao
 
aja

Member
Nov 26, 2010
35
17
Wakiweka mwanamke tu ndio mwisho wa CCM Ikulu. Kuna ushahidi wa kimazingara unaoonyesha kuwa wanawake hawapendi kuwachagua mwanamke mwenzao wakati anapokuwa anagombea na wanaume. Tena hii huwa inatokea sana kwenye jamii ambayo inaamini mfumo dume. Jamii ya Tanzania ina amini sana mfumo dume.

hii ni janja ya ccm ya kutaka kuhalalisha matakwa ya uislm wao.dalili za kutaka uislmu kwa namna yoyote kwa visingizio vya uzanzibar na swala la wanawake ni mtindio wa nyani kundule au mbuni kuficha kichwa mchangani wakati kiwiliwili kiko angani.namkitekeleza haya, ni sawa na kuleta ushindi kwa chadema.tuna omba mtekeleze mpango huo
 
We Know Next

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
797
363
Toka lini mafuriko unayweza kuyazuia? toka lini unaweza kupambana na Tsunami? tola lini unaweza kupambana na tetemeko la ardhi linalofikia richer scale 9.998? Basi mabadiliko wanayotaka watanzania wengi kwa sasa ni kama hayo mafuriko, tsunami, na matetemeko. Basi mwenye kuyazuia na ayazuie.
 
Konakali

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
1,534
256
Siku ya kufa nyani miti yote huteleza...! Watakimbilia kila kona, watatapatapa huku na huko, watakimbilia kila mti, lakini mwishowe yote huteleza....! Hata hivyo husadikika kuwa huenda marekani baada ya kumuona options zilizobakia zilikuwa ni Obama na Hillary tu, basi na kutokana na mafunzo waliyoyapata wao hasa katika kumsaka aliyekuwa Rais wa Iraq; Sadam, basi wakaona wanaweza kuiuza nchi yao kwa kumchagua Hillary kuwa Rais wao....!
Nakubaliana nawe kuwa mbinu za kumuweka Spika mwanamke ni hizo hizo, lakini kumbuka kwamba huyo spika alikuwa amekwisha andaliwa nafasi baadaya kuthibitisha kuwa kura nyingi ni za CCM.....! Je, wakifanya hivyo kwa huyu, si watamleta kwetu uraiani?
Hata hivyo haikuwa haramu sana kufanya hivyo, bali kama ni kweli ndio tayari ni kosa sasa, maana haukupaswa kujulikana mapema....! Nadhani ni wajibu wa vyama vya upinzani sasa kutumia nafasi ya ule usemi kuwa "kumjua adui yako ni nusu ya kumshinda"....!
 
woyowoyo

Senior Member
Jul 24, 2011
173
12
Huyo slaa mnayemfagilia hana sifa hizo, mnataka tuje turudie uchaguzi kizee cha miaka 69 mpaka 2015 kina miaka 74 lengo lenu muitie serikali hasara.
 
Omr

JF-Expert Member
Nov 18, 2008
1,160
99
CCM hata ikimweka Rostam agombee urais basi atashinda. Watu wanachagua chama sio mtu,hii ndio Tanzania.
 
Najijua

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
1,039
179
Hakuna mapana yasiyo na ncha!kila lenye mwanzo linamwisho!hata wamsimamishe nani zaidi ya miaka 50 walio tawala itakuwa imewatosha mpk ikifika 2015 wanao washangilia leo watawazomea,wanao waringia leo eti mtaji wao hakika ndo watakuwa anguko lao
 
PAMBA1

Member
Sep 13, 2011
55
26
hawa ccm mbinu yao haitafanikiwa ila tu nawaomba kupitia vitabu na kusoma dola zilizokuwa na nguvu duniani na zimeangushwa kama dola iliyokuwa ya warumi.sembuse ccm ya vasco da gama pamoja na mafisadi wezake.
 
Twasila

JF-Expert Member
May 12, 2011
1,913
595
Tunataka rais atakayeongoza TZ kwa uadilifu. Uaminifu, mwenye vision, adui wa mafisadi, anayejua matatizo yetu, anayejua kuwa tunaweza kuendelea kwa kujitegemea.

Hayo ya kina sofia na salma ni upungufu wa busara na hekima. Wtz hatuwezi kuchagua rais kwa sababu tu ni m'ke. Hatuwezi kuongoza nchi kwa kupeana zamu.
Huu ni ubakaji wa demokrasia. Mawazo haya unaweza kuyapata kwa waropokaji kama ss.

Kuwa na mawaziri kama sofia inatufanya tuone ni uzalilishaji wa wanawake.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom