Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara akwaa kisiki kwa njama zake

nokwenumuya

JF-Expert Member
Jun 29, 2019
810
2,851
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Ndugu Samuel Kiboye almaarufu namba tatu ameshindwa jaribio lake la kumuondoa katibu wa CCM wilaya ya Tarime baada ya kushindwa kumshawishi kuungana nae katika harakati za kumsaidia aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo Ndugu Kisyeri Werema Chambiri kuwa mbunge tena kwenye uchaguzi ujao wa 2020.

Baada ya katibu huyo kukataa kuwa upande wake na kumwambia yeye anasimamia maslahi ya chama na hana mgombea Mwenyekii huyo kwa hasira kuwa katibu kakataa kufuata maelekezo yake alianza kufanya njama za kuhakikisha anaondoka na akamtumia katibu wa mkoa katika jaribio hilo. Na alifikia mbali hadi kulitumia gazeti la majira kuandika kuwa katibu wa CCM Tarime hakubaliki kwa wanachama, jambo ambalo sio kweli.

Hata hivyo viongozi wa juu walijua njama hizo na kuhakikisha wanazima zoezi hilo na njama hizo.

Kwa sasa Mwenyekiti huyu wa mkoa hajui hatma ya mgombea aliyemuweka kibindoni itakuwaje, kwani wananchi wa Tarime mjini wanauliza kasahau nini baada ya kuwa mbunge kwa vipindi vitatu mfululizo kutoka 1990-2005 alipoangushwa kwenye uchaguzi mkuu wa 2005 na Marehemu Chacha Zakayo Wangwe (CHADEMA).
 
Ninawahakikisheni kuwa Kisyeri Chambiri hawezi kuwa tena Mbunge wa Tarime Mjini. Watu wa Tarime wana msimamo. Kama wanataka CCM ingukie pua basi wamrudishe Kisyeri Chambiri.
 
Back
Top Bottom