Mwenyekiti wa CCM Mara asema Rais Samia ataongoza nchi hadi mwaka 2030, awaonya wanaompinga

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,206
42,068
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Mara Samuel Kiboye maarufu kwa jina la Namba tatu amesema Rais Samia Suluhu Hassan ataongoza nchi hadi mwaka 2030 kwani wananchi wa Kanda ya Ziwa wanampenda na wanamkubali.

Ameyasema hayo mbele ya Rais Samia ambaye yuko ziarani mkoani mwanza. Mwenyekiti huyo amemuhakikishia Rais kuwa wananchi wa kanda ya Ziwa wako pamoja nae na wana muunga mkono sana na hawatokubali mtu yeyote au kikundi chochote kimyumbishe Mh Samia ambaye ni chaguo la Mungu kwa Watanzania.
 
Hata hawa walikuwa mpango wa Mungu.

"Yapo mazingatio kwa wenye kufikiri"

FB_IMG_1623299513121.jpg
 
na hawatokubali mtu yeyote au kikundi chochote kimyumbishe Mh Samia ambaye ni chaguo la Mungu kwa watanzania.....

Source Mwananchi

#MwananchiUpdates
Mr. Hamnazo naye mlisema ni chaguo la mungu, ajabu alipojiondokea kwa kchomwa mbigiri kwenye makagari, mmemnawa. Hata Kubwa Jinga wa enzi hizo naye mlisema ni chaguo la mungu.

Huyo mungu bila shaka hajui kuchagua kwa usahihi au ana akili ndogo Sana.

Kumbuka: Unaposoma post hii, kichwani mwako tofautisha mungu na Mungu.
 
Hawa wapumbavu wameanza tena ujinga wao. Hivi watu wa hii kanda mnashida gani?
Kwa kweli hii kanda kuna shida mahali. Hivi watu wa kanda ya ziwa tatizo lao ni nini? Mimi huwa siwaelewi kabisa. Yaani unafiki, uuaji, roho mbaya, kuua watu kama akina Mawazo, kuamuru wenzao wapigwe risasi, watu kuswekwa kwenye viroba, kuua albino, yote ni wao. Kuna nini kanda ya ziwa?
 
Kwa kweli hii kanda kuna shida mahali. Hivi watu wa kanda ya ziwa tatizo lao ni nini? Mimi huwa siwaelewi kabisa. Yaani unafiki, uuaji, roho mbaya, kuua watu kama akina Mawazo, kuamuru wenzao wapigwe risasi, watu kuswekwa kwenye viroba, kuua albino, yote ni wao. Kuna nini kanda ya ziwa?
Kwani wananchi ndiyo wameongea ama kaongea kiumbe mmoja tu ambaye ni mwenyekiti wa CCM tu? Usiwahukumu wananchi kwa vigezo vyako vya matukio ambayo huwa yapo mikoa yote ikiwemo uchunaji ngozi kule Mbozi mbeya hakuna mkoa wenye malaika watupu Tanzania hii kila wilaya inao wahalifu wake, Mh Rais Samia kaletwa na mungu kuja kuwatibu watanzania ambao walijeruhiwa na mtukufu magufuli enzi za uhai wake, si ajabu kusikia matamko ya viongozi wa CCM kwani lazima wafanye hivyo kama ilivyokuwa kawaida yao,watanzania tuendelee kuchapa kazi na kumuomba mungu amjalie afya njema Rais wetu aziti kuliongoza Taifa kwa Amani na upendo
 
Hawa wapumbavu wameanza tena ujinga wao. Hivi watu wa hii kanda mnashida gani?
Mtu mmoja tena mwenyekiti wa mkoa mwingine ana uhusiano gani na watu wa kanda nzima? Acha kuhukumu watanzania wengi kwa kigezo cha fikra binafsi za kada wa CCM
 
Hayo ni mawazo binafsi ya huyo CCM wa mara siyo mawazo ya wananchi wote ambao wanajua katiba inavyoelekeza juu ya ukomo wa kuwa Rais wa Tanzania
 
Hata Mwendazake walisema hivyohivyo na zaidi ila leo imekuwa story. Mipango ya Mungu ni tofauti na mwanadamu
Falsa ya wanaccm mda wote ndiyo walivyokuwa wao ni watu wa kutengeneza mazingira ambayo hawajawasiliana na mungu
 
Wameanza tena ngonjera nyimbo za sifa na mapambio lukuki,ngoja tuone muda huwa ni Mwl mzuri sana!
 
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Mara maarufu kwa jina la Namba tatu amesema Rais Samia Suluhu Hassan ataongoza nchi hadi mwaka 2030 kwani wananchi wa Kanda ya Ziwa wanampenda na wanamkubali.

Ameyasema hayo mbele ya Rais Samia ambaye yuko ziarani mkoani mwanza, Mwenyekiti huyo amemuhakikishia Rais kuwa wananchi wa kanda ya Ziwa wako pamoja nae na wana muunga mkono sana na hawatokubali mtu yeyote au kikundi chochote kimyumbishe Mh Samia ambaye ni chaguo la Mungu kwa watanzania.....

Source Mwananchi

#MwananchiUpdates
huo ndio ukweli,,Hadi #2040 inshallah
 
Back
Top Bottom