Mwenyekiti wa CCM anakwenda kuamua tena nani agombee ubunge kama alivyofanya Hayati Magufuli kipindi kilichopita. Ukimkosoa Mwenyekiti umeumia

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Ndani ya CCM ulizaliwa mfumo wa wabunge kupita kwa hisani ya Mwenyekiti, mfumo huu unakenda kuzima mabishano ya hoja.

In long-run hakutakua na kiongozi nchini atakayetoboa bila kumnyenyekea mwenyeti, na kwa mantiki hiyo tunaelekea kipindi ambacho malengo yako kisiasa utafikia pale tu utakapowaza kama mwenyekiti.

Kinyume chake nenda upinzani au tafuta kazi ya kufanya hadi siku tutapata Katiba Mpya.
 
Sio huko tu, hata kule bungeni Spika atakaepatikana lazima ajipendekeze kwa mwenyekiti wa chama chake kwasababu atakuwa bado anakumbuka msuto uliompata mtangulizi wake.

Wabunge wanajipendekeza, spika anajipendekeza, wasio na vyeo wanajipendekeza twitter, mawaziri wanajipendekeza, sasa wanaibuka "wapinzani" nao wanajipendekeza, nchi imeoza kwa kujipendekeza.

Matokeo yake taifa linakuwa na mawazo mgando, hakuna wanaokuja na hoja mpya za kubadili hali ya mambo kwa kuogopa kumuudhi mtukufu/mshirika wao.

Hapo umasikini utaendelea kuwepo, kukopa nje kutaanza kuwa sifa, uwezo wa kufikiria unazidi kushuka kila siku huku tunaenda ikulu kuimba tuna imani na mtukufu.

Taifa la giza kabisa.
 
Tatizo kubwa ni kukosa upinzani unaojielewa, wapinzani kwasababu ya chuki yao dhidi ya Ndugai, wameungana na CCM wahuni/maslahi kumuuondoa spika. In the process, wamedhoofisha bunge ambalo walikuwa wanasema ni dhaifu, mara milioni ya vile ulivyokuwa mwanzo.
Ingekuwa ngumu sana kumuunga mkono Ndugai sababu ndani ya CCM amelikoroga nje ya CCM ndio wapinzan ambao amewasulubu muda wote alipokuwa spika
 
Ndani ya CCM ulizaliwa mfumo wa wabunge kupita kwa hisani ya Mwenyekiti, mfumo huu unakenda kuzima mabishano ya hoja.

In long-run hakutakua na kiongozi nchini atakayetoboa bila kumnyenyekea mwenyeti, na kwa mantiki hiyo tunaelekea kipindi ambacho malengo yako kisiasa utafikia pale tu utakapowaza kama mwenyekiti.

Kinyume chake nenda upinzani au tafuta kazi ya kufanya hadi siku tutapata Katiba Mpya.
Ukiwa chama cha upinzani usipoelewana na Mwenyekiti unaweza kupitishwa kugombea Ubunge?
 
Sio huko tu, hata kule bungeni Spika atakaepatikana lazima ajipendekeze kwa mwenyekiti wa chama chake kwasababu atakuwa bado anakumbuka msuto uliompata mtangulizi wake.

Wabunge wanajipendekeza, spika anajipendekeza, wasio na vyeo wanajipendekeza twitter, mawaziri wanajipendekeza, sasa wanaibuka "wapinzani" nao wanajipendekeza, nchi imeoza kwa kujipendekeza.

Matokeo yake taifa linakuwa na mawazo mgando, hakuna wanaokuja na hoja mpya za kubadili hali ya mambo kwa kuogopa kumuudhi mtukufu/mshirika wao.

Hapo umasikini utaendelea kuwepo, kukopa nje kutaanza kuwa sifa, uwezo wa kufikiria unazidi kushuka kila siku huku tunaenda ikulu kuimba tuna imani na mtukufu.

Taifa la giza kabisa.
Hata humu Jf wengi nao wanajipendekeza.
Kwa maoni yangu huu ni wakati muafaka kupigania kwa nguvu zote mgombea binafsi aruhusiwe. Ingawa najua vyama vyote havitaki kwa sababu itaua tabia ya kuabudiwa viongozi wa vyama. Kwa kuwa katiba mpya ni ngumu kupatikana basi tujikite zaidi kutaka vipengele viwili vibadilishwe navyo ni kuruhusu mgombea binafsi na tume huru ya uchaguzi.
 
Tatizo kubwa ni kukosa upinzani unaojielewa, wapinzani kwasababu ya chuki yao dhidi ya Ndugai, wameungana na CCM wahuni/maslahi kumuuondoa spika. In the process, wamedhoofisha bunge ambalo walikuwa wanasema ni dhaifu, mara milioni ya vile ulivyokuwa mwanzo.
Halafu ukiwa na upeo wa ziada, wanalia uko neutral, hawajui hii michezo inachezwaje, wamekariri maisha tu kwao sifa ni kukomaa kama jiwe, kama unampinga mtu yeyote ni kumpinga tu kila atachosema mpaka mwisho wa dunia.

Ndio maana wamejikuta kwenye huo mtego wa kutumbukia kwa Samia sababu wanasiasa za kukariri, hawajui kuwa neutral sometimes kuna epusha mitego ya kitoto kama hiyo.

Hizi akili migando ni tatizo sana.
 
Hata humu Jf wengi nao wanajipendekeza.
Kwa maoni yangu huu ni wakati muafaka kupigania kwa nguvu zote mgombea binafsi aruhusiwe. Ingawa najua vyama vyote havitaki kwa sababu itaua tabia ya kuabudiwa viongozi wa vyama. Kwa kuwa katiba mpya ni ngumu kupatikana basi tujikite zaidi kutaka vipengele viwili vibadilishwe navyo ni kuruhusu mgombea binafsi na tume huru ya uchaguzi.
Ili hili kuwezekana madai ya Katiba Mpya yahamishwe kutoka kwa vyama, nani wawe mbadala wa kuongoza mashambulizi, wakulima? wafugaji? mamalishe? wavuvi?

Akishapatikana huyo kiongozi, ndio madai ya mgombea binafsi au Tume Huru yawepo, japo najua yote hayo yapo kwenye ile rasimu ya Warioba.
 
Back
Top Bottom