Mwenyekiti wa CCM ajiuzulu kwa kuhudhuria sherehe ya CHADEMA (Chanzo HabariLeo)

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,603
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Makanyagio wilayani Mpanda mkoani Katavi, Chifu Mlela Mallac, amejiuzulu nafasi hiyo kwa kile kinachoelezwa kwamba amekuwa akizongwa mara kwa mara na wanachama na baadhi ya viongozi wa chama hicho akituhumiwa kukisaliti.

Mallac anatuhumiwa kuhudhuria sherehe ya kumpongeza mama yake kwa kuteuliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani hapa mapema mwezi huu.

Mwenyekiti huyo anatoka kwenye familia ya wanasiasa kwani baba yake, John Mallac ni Mwanyekiti wa Chadema Mkoa wa Katavi, wakati mama yake, Anna Mallac ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chadema.

Mwanasiasa huyo pamoja na kuwa ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Makanyagio na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Mpanda, lakini pia ni Chifu wa eneo la Mpembe lililopo Tarafa ya Mwese ambako alitawazwa kijadi kuwa mtemi wa eneo hilo mwaka jana.

Katika mazungumzo yake ya simu na kisha akiwa dukani kwake maeneo ya barabara mbili mjini hapa, Mallac alikiri kujiuzulu nafasi hiyo, akisema kuwa kama mtemi ni mtu wa watu wote bila kujali itikadi zao za kisiasa, na pia kama mtoto alikuwa na haki ya kuhudhuria sherehe ya kumpongeza mama yake baada ya kuteuliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalumu mkoani hapa mapema mwezi huu.

Lakini alisema sababu kubwa iliyomfanya ajiuzulu nafasi hiyo ya kisiasa, ni kutokana na maadili mabaya kutoka kwa baadhi ya wanachama na viongozi wa CCM kutoka ngazi ya Kata hadi Wilaya ambapo anawatuhumu kuwa hawana siri wala uwajibikaji unaotakiwa.

Akifafanua, alisema hali hiyo ilijitokeza wakati wa mchakato wa uchaguzi wa Mbunge wa Mpanda Mjini ambapo baadhi ya wanachama na viongozi wa CCM wilayani, alidai walikisaliti chama tawala kwa kumuunga mkono mgombea wa jimbo hilo kupitia Chadema.

Katika uchaguzi huo, Said Arfi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa alishinda tena kiti hicho kwa miaka mitano ijayo; huku CCM wakishutumiana wenyewe kwa wenyewe wakimtafuta mchawi.

“Viongozi na baadhi ya wanachama wa CCM wamegawanyika baada ya kushindwa kulirejesha jimbo hali iliyojenga chuki miongoni mwetu kusema kweli.

Baadhi ya viongozi na wanaCCM wenyewe wakati wa mchakato wa uchaguzi kwa nafasi ya ubunge tulidhani tuko pamoja kumbe baadhi ya viongozi wenzetu walikuwa wanafiki...Walitusaliti kwa kumuunga mkono mgombea wa Chadema,” alidai Mallac.

Katika barua yake kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Mpanda, Jacob Nkomola, Mallac alisema anajiuzulu ili kutoharibu jina na sifa yake kwa jamii inayomwamini na kumfanya awe Chifu wao.


BADO MWENGINE
 
I hope Michuzi, Mjengwa et al. will post this story on their blogs also.
 
Nachojua kinacho wazuia watu CCM ni ulaji sasa safari hii haupo kwa sababu wapinzani ni wengi, wananchi watafaidi sana labda kwa sehemu ambazo kuna CCm tu ndo watakwapua kwapua wananchi na vijana tuwe macho na hawa jamaa.
 
Hivi Mke wangu (CCM) akipata mafanikio katika Chama chake mimi (TLP) nisimpongeze? Nimnunie? Nigombane naye?
 
Na bado tunasubili wengine

Mimi CCM na serikali yao wananishangaza sana, wakishindwa wanaamini kuna mtu anawasaliti hivi wao hawawezi kukiri udhaifu hadi watafute mtu wa kumtwishwa gunia la misumari?

Mfano mwingine ni vyuoni, kukiwa na vuguvugu la wanafunzi kudai mambo ya msingi ambayo serikali inapaswa kuyatimiza lakini yaifanyi hivyo, utasikia wanasema hawa wanafunzi wanatumiwa na vyama vya upinzani, mara wataitwa ni genge la wahuni, huu ni ujinga wa hali ya juu. Hivi wanafunzi hawana akili ya kujua nini ni haki yao nini siyo?

Endeleeni kujiudhulu CCM kwani chama kisicho na dira
 
Jamani naona itafikia kipindi CCM watawaambia wafuasi wao wazikane familia zao
 
very good kaonyesha kwamba yeye ni msafi na hataki kuchafuliwa, chifu mzima unakuwa sisiemu si unafiki huo . big up
 
Karibu cheif kwenye chama makini na chenye wanachama makini kama wazazi wako,
Chadema peoples powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
Back
Top Bottom