Mwenyekiti wa bodaboda Shinyanga ajinyonga.

jaffari yogo

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
685
148
NEWS ALERT!
Mwenyekiti wa Chama Cha Waendesha Pikipiki maarufu kama bodaboda manispaa ya Shinyanga Jacob Paul (36) amejiua kwa kujinyonga kwa kutumia waya wa simu chumbani kwake katika mtaa wa Mwinamila kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga.

Tukio hilo limetokea leo Jumamosi June 10,2017 mchana.
Tukio hili limetokea siku tano tu baada ya kutokea vurugu kati ya waendesha bodaboda na polisi baada ya mwendesha bodaboda mwenzao kufariki baada ya kukamatwa na askari wa usalama barabarani.
7235266998375b47175f40650970800b.jpg


====

Mwenyekiti wa chama cha waendesha Bodaboda mjini Shinyanga Bw.Jacob Joshua amefariki kwa kujinyonga kwa kamba ambapo inadhaniwa amechukua uamuzi huo kutokana na vitisho vya Bodaboda wenzake na ndugu zao wakimtuhumu kushirikiana na Polisi kuwakamata bodaboda zaidi ya 200 waliokuwa wanaandamana kufuatia kifo cha mwenzao siku tano zilizopita.
19029581_1239097706201201_2971603078133569065_n.jpg
19030464_1239097702867868_9155709763940995544_n.jpg
 
Bora angejigongesha kwenye mti na lipikipiki lake angepata umaarufu kama mwenzie!!! Aende Salama Huko Aendako
 
Ninapata Mashaka sana kwa hii aina ya kujinyonga kwa huyu mwenye kiti.
Nawaza kwa sauti kwamba eti amekutwa amejinyonga kwa kutumia waya Wa simu.....
Hapana hii haini ingii akilini kabisa kama ifuatavyo:-

1- Tazama mwili wa marehemu, bilashaka alikua na uzito kati ya 78-83 kgs.
2- Je wara wa simu unauwezo wa kuning'iniza uzito huo...
3- Eti amekutwa amejinyonga baada ya kutokea mgogoro kati ya police na waendesha pikipiki (boda boda).
4- Kuna nini kilicho sababisha hadi akajiuwa, na kwanini hakujiuwa kabla ya kutokea mgogoro huo na police....

Hapana hapa kuna kilicho jificha, maana hii habari haikai akilini kizembe hivyo aiseeeeee.......

R.I.P mwenyekiti wao...
 
Sasa Mura umikwenda jumula na hasira za Iringa bhana,,,Huchafanya vizuri mura-mweto bhora ungejichinga tu,,au umetundikwa kisasa mura manake ***** hawawachagi watu salama
 
Dhuluma huzaa chuki halafu kisasi.


Poleni watanzania,yote haya yameletwa na ccm.

Wito:Tume huru idaiwe mapema ccm itoke vinginevyo watanzania mtapata tabu sana.

Inauma sana.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom