Mwenyekiti wa Bavicha Kilimanjaro afikishwa Mahakamani kwa kusambaza video za ngono

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), Mkoa wa Kilimanjaro, Lemrus Mchome (30), amefikishwa mahakamani akikabiliwa na tuhuma za kusambaza nyaraka za ngono ikiwamo picha na video kwa nia ya kuleta ashki za ngono kinyume cha sheria.

Mchome ambaye ni mkazi wa Kisaranga, Wilaya ya Mwanga, amesomewa mashtaka yake katika Mahakama ya Hakimu Kisutu, jijini Dar es Salaam iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi, Vick Mwaikambo.

Wakili wa Serikali Mkuu, Tumaini Kuweka, alidai kuwa kati ya Januari Mosi na Aprili 30, mwaka huu, jijini Dar es Salaam mshtakiwa alitenda kosa la kusambaza nyaraka za ngono.

Kweka aliendelea kudai kuwa Mchome alisambaza nyaraka za ngono ikiwamo picha na video za mwanamume kupitia simu yake ya mkononi kwa nia ya kuleta ashki za ngono kitu ambacho ni kinyume cha sheria.

Mshtakiwa alikana mashtaka hayo na upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Hata hivyo, Kweka aliiomba mahakama isitoe dhamana kwa mshtakiwa huyo kwa sababu upelelezi unaendelea.

Mchome alidai mashtaka hayo yamemshtua kwa kuwa alikamatwa Mei 11, mwaka huu, lakini amezuiliwa kuonana na ndugu zake pamoja na wanasheria.

Alidai kesi hiyo sio ya kwanza kwa mahakama hiyo kwa kuwa zipo ambazo zilitolewa dhamana huku upelelezi ukiendelea.

Akijibu hoja hiyo, Kweka alidai huo ni mkakati wao wa kuendelea na upelelezi.

Hakimu Mwaikambo alisema uamuzi wa mabishano ya pande zote mbili kuhusu dhamana itatolewa Juni 2, mwaka huu, mshtakiwa arudishwe mahabusu.
 
Yaani kupiga picha gari ni kosa, tena huyo Diwani tunamlipa mshahara sisi wenyewe kweli Bongo bahati mbaya.
 
Kama ni kweli sheria ichukue mkondo wake na akatiwe adhabu kali iwezekanavyo! Ni kinyume na maadili ya mtanzania, kinyume cha maadili ya Chadema, na ni kinyume kabisa na mafundisho ya vitabu vitakatifu.

Kajituma mwenyewe huyo hakuna aliyemtuma! Lakini pia ni muhimu sana Chadema wakawa makini maana ndani humo kuna mamluki na mbwa mwitu wengi sana wanaowatumikia maadui nje huko. Be careful tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu.
 
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), Mkoa wa Kilimanjaro, Lemrus Mchome (30), amefikishwa mahakamani akikabiliwa na tuhuma za kusambaza nyaraka za ngono ikiwamo picha na video kwa nia ya kuleta ashki za ngono kinyume cha sheria.
Ikiwa kama amefanya kikweli kitendo hicho, basi tunaiomba serikali itoe adhabu kali sana kwa sababu kitendo hicho ni ujinga uliopita mipaka.

Ni lazima tulinde maadili ya taifa kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vya baadae.

MZALENDO.
 
Back
Top Bottom