Mwenyekiti wa BAVICHA atoa onyo kali kwa viongozi wa serikali akiwemo mkuu wa wilaya ya Igunga

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Akiongea na waandishi wa habari jana Heche ametoa tahadhari kwa polisi na wakuu wa mkoa na mkuu wa wilaya ya Igunga kuwa wasiwe chanzo cha kusababisha fujo nchini waviache vyama vya siasa vishindane kwa haki lakini wakiingilia kugeuza matokeo safari hii vijana wa Chadema hawatakubali. Ameongeza kama polisi hawatenda haki na kuendelea kutotoa ushirikiano watawashughulikia waharifu wakiwemo viongozi kama walivyomshughulikia mkuu wa wilaya jana.

Msikilize mwenyewe hapa anaonekana kama Julius Malema wa Tanzania

Last edited by a moderator:
"Natoa onyo kwa kiongozi yeyote atakaye temper na matokeo tutamshugulikia na jana mkuu wa wilaya ametolewa kwa ustaarabu sana lakini akirudia tena atafika polisi ameshugulikiwa" haya ni baadhi ya maneno yake Duh! Lakini kwanini safari hii Chadema wamejiamini sana?
 
Duh,hakyanani naomba tu polisi wasifanye mafunzo yao kwa
vitendo this time again
 
"Natoa onyo kwa kiongozi yeyote atakaye temper na matokeo tutamshugulikia na jana mkuu wa wilaya ametolewa kwa ustaarabu sana lakini akirudia tena atafika polisi ameshugulikiwa" haya ni baadhi ya maneno yake Duh! Lakini kwanini safari hii Chadema wamejiamini sana?

coz ni watetezi wa kweli na sio wanafiki.Na wanajua wana support kutoka kwetu.Aluta kontinua makamanda
 
busara zitumike katika kutatua maamuzi magumu
fujo hazitajenga, tunajua CDM kinapendwa na vijana wengi kiasi kwamba Viongozi wakiwamulisha kufanya vurugu wengi wata kubali kitu ambacho hatuombei kitoee. Tunaomba CDM wawe watulivu zaidi kwani NGUVU ya UMMA ipo nyuma yao " AMENI "
 
Ni vizuri busara kutumika zaidi badala ya vurugu.Kiongozi bora hutawaliwa na maamuzi bora.Tukiwalea hawa vijana kwa kusupport uvunjifu wa amani,iko siku watakuwa kikwazo pia kwa CDM.Heche aandae mazingira ya Ushindi kuliko kuandaa vurugu,kumbuka kuna CUF pia hapo sio CCM pekee hivyo hizo kura elfu 44 zitagawika kweli kweli na hakuna ushindi wa kishindo hapo.
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Mkuu, busara unayoiongelea hapa ni pamoja na kusema NO to upuuzi wowote unaopelekea kubaka demokrasia.
Ni vizuri busara kutumika zaidi badala ya vurugu.Kiongozi bora hutawaliwa na maamuzi bora.Tukiwalea hawa vijana kwa kusupport uvunjifu wa amani,iko siku watakuwa kikwazo pia kwa CDM.Heche aandae mazingira ya Ushindi kuliko kuandaa vurugu,kumbuka kuna CUF pia hapo sio CCM pekee hivyo hizo kura elfu 44 zitagawika kweli kweli na hakuna ushindi wa kishindo hapo.
<br />
<br />
 
Hawa polisi wengine wanawashwa sababu kazi yao si kupiga watu kazi yao ni mulinda wananchi na ieleweke kwamba wanalipwa kwa kazi ya kuwalinda wananchi kwahiyo naunga mkono hoja ya heche na kusisitiza kuwa vijana tuko macho kupambana na kila aina ya uonevu dhidi ya raia wema
 
Nguvu ya umma maana yake ni hiyo siyo kufuata taratibu maana huchukua muda mrefu na haki hupotezwa katika mchakato huo
 
Ni vizuri busara kutumika zaidi badala ya vurugu.Kiongozi bora hutawaliwa na maamuzi bora.Tukiwalea hawa vijana kwa kusupport uvunjifu wa amani,iko siku watakuwa kikwazo pia kwa CDM.Heche aandae mazingira ya Ushindi kuliko kuandaa vurugu,kumbuka kuna CUF pia hapo sio CCM pekee hivyo hizo kura elfu 44 zitagawika kweli kweli na hakuna ushindi wa kishindo hapo.
Mtu anakubakia mkeo halafu linatokea jamaa kama wewe linasema usimpige mbakaji tumia busara kama mimi nawachanganya wote wewe uliyeniambia nitumie busara na mbakaji mnapata kisago.
 
Namsapoti kijana kwa 100%
Kumbukeni;
  1. Tukiwa shule za misingi (Watu waliheshimiana baada ya kupigana)
  2. Nchi nyingi zenye maendeleo zilipitia kuchapana kwanza baada ya kukosekana haki (mfano USA, Kenya)
Ila siungi mkono fujo, sema serikali na vyombo vya usalama wanatakiwa waelewe wao kazi yao ni kulinda raia wote (yaani wao ndiyo baba na mama wa nchi) waige mfano wa aliyekuwa kamanda wa polisi Mwanza.
 
"Polisi watuache tucheze mpira na CCM na hao CUF waliowaleta"........kwenye bold hao Kafu wameletwa na nani?
 
Busara itumike na Polisi na DC kutokuingilia uchaguzi na kuminya haki za wananchni
 
Akiongea na waandishi wa habari jana Heche ametoa tahadhari kwa polisi na wakuu wa mkoa na mkuu wa wilaya ya Igunga kuwa wasiwe chanzo cha kusababisha fujo nchini waviache vyama vya siasa vishindane kwa haki lakini wakiingilia kugeuza matokeo safari hii vijana wa Chadema hawatakubali. Ameongeza kama polisi hawatenda haki na kuendelea kutotoa ushirikiano watawashughulikia waharifu wakiwemo viongozi kama walivyomshughulikia mkuu wa wilaya jana.

Msikilize mwenyewe hapa anaonekana kama Julius Malema wa Tanzania

http://www.youtube.com/v/OpUr0i0N3gU?version=3"><param

huyu mwenyekiti anatakiwa awe makini na maneno yake,kwanza kitendo walichomfanyia mkuu wa wilaya ni udhalilishaji,pili hawana adabu vijana walioenda kumtoa maana nilikuwepo eneo la tukio na hawakumtendea haki kumsikiliza kwani alikuwa akijitetea .tatu mtuwekee ushahidi halisi kuwa alikuwa anapanga kuwaingilia uchaguzi wenu?
 
Kasome sheria za uchaguzi!!!! Hakuna kutafuniwa hapa!!!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom