Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,343
- 217,378
Hii ndio Taarifa mpya kutoka Chadema kwa sasa, ambapo watu wasiofahamika wakiwa na bunduki wamemchukua Mzee Hashimu Issa nyumbani kwake Unguja na kuondoka naye, tena bila kusema wanampeleka wapi.
Taarifa zaidi zitaendelea kuwajia kwa kadri zitakavyotufikia.
====
UPDATES
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kumshikilia mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chadema (Bazecha), Hashimu Issa Juma kwa tuhuma za uchochezi wa kujenga chuki kati ya Serikali na wananchi.
Issa alikamatwa Oktoba 3,2021 mjini Unguja, Zanzibar kisha kushikiliwa kwa muda kabla ya kusafirishwa jana Jumatatu Oktoba 4,2021 kuletwa Dar es Salaam kwa mahojiano zaidi.
"Uchunguzi wa shauri hili unaendelea na ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo," amesema Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam,Jumanne Muliro katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Juma ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya Chadema anadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba Mosi,2021 wakati wa mkutano wake na wanahabari uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya Chadema Kinondoni.
=====
Mwenyekiti wa baraza la Wazee Chadema afikishwa Mahakamani
Akisoma mashtaka hayo, Wakili wa Serikali Yusuph Aboud alidai Mshitakiwa huyo alitenda makosa hayo October 1 mwaka huu mtaa wa Ufipa, Kinondoni, Dar es Salaam ambapo katika shitaka la kwanza ilidaiwa akiwa eneo hilo alichapisha taarifa ya uongo kwa njia ya kompyuta na kusambaza katika mtandao wa YouTube kwa lengo la kumchafua na kumdhalilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro.
Ilidaiwa alichapisha kuwa ‘IGP Sirro ni gaidi namba moja hapa nchini Tanzania na fisadi’ na katika shitaka la pili ilidaiwa katika tarehe na eneo hilo, alichapisha taarifa ya uchochezi kwa lengo la kutengeneza chuki kwa Wananchi dhidi ya IGP Sirro kuwa ‘IGP Sirro ni gaidi namba moja hapa nchini Tanzania na fisadi’.
Baada ya kusomewa mashitaka hayo upande wa mashitaka ulidai upelelezi wa kesi hiyo upo katika hatua za mwisho hivyo wapangiwe tarehe nyingine ya kutajwa na Hakimu alikubali ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 28 mwaka huu huku Mshitakiwa akiachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana likiwemo kuwa na wadhamini wawili wenye vitambulisho vya kura au cha taifa watakaosaini bondi ya Sh.Mil 3 kila mmoja.
Pia, soma: Hashimu Juma, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee CHADEMA[BAZECHA afutiwa mashtaka na DPP