Mwenyekiti UVCCM na wengine mbaloni kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi

Bongo Pix Blog

JF-Expert Member
Sep 13, 2011
213
33
POLISI mkoani Singida inawashikilia wakazi watatu wa Manyoni kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi wa Kidato cha Tatu katika Shule ya Sekondari Mwanzi ya mjini humo, kwa madai ya kuiba simu ya Sh 70,000.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Celina Kaluba, aliwataja watuhumiwa wa mauaji hayo kuwa ni Mwenyekiti mstaafu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Manyoni, Jamal Kuwingwa (37), Hamza Mahagile (38) na Juma Msilo (33).

Watuhumiwa hao wanadaiwa kumuua mwanafunzi Boniface Kawonga (19), kwa kumpiga vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake na kumvunja mguu wa kushoto kwa madai kuwa aliiba simu ya mkononi yenye thamani ya Sh 70,000, mali ya Kuwingwa.

Kamanda Kaluba alisema mauaji hayo yalifanywa Jumapili Septemba 25 saa 3:30 asubuhi mjini Manyoni.

Alisema mwanafunzi huyo alifariki dunia siku hiyo alasiri wakati wakati akiendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni.

Alisema upelelezi utakapokamilika, watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma ya mauaji hayo.

Habari zaidi kutoka eneo la tukio zinadai kuwa watuhumiwa hao walimdaka mwanafunzi huyo muda mfupi tu baada ya kupata dhamana Kituo cha Polisi na wakaamua kujichukulia sheria mkononi.

Source: Habari Leo
 
Angekua mw.kiti wa magwanda ingekua ishu kubwa .wanauwa mwizi wakati wenyewe ni majambazi wakubwa
 
Poleni wanamanyoni wenzangu kwa msiba raha ya milele uwape ee bwana na mwanga wa milele uwaangazie.....!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom