Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa DSM adaiwa kutapeli Sh. mil 57 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa DSM adaiwa kutapeli Sh. mil 57

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Freestyler, Feb 24, 2011.

 1. Freestyler

  Freestyler Senior Member

  #1
  Feb 24, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 24th February 2011 @ 08:20

  MTOTO wa aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Tatu Ntimizi, Said Ntimizi amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam akikabiliwa na mashitaka mawili likiwemo la kujipatia Dola za Marekani 38,400 (Sh milioni 57.6), kwa njia ya udanganyifu.

  Said, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam alifikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mfawidhi Kwey Rusema.

  Mwendesha Mashitaka Mkuu David Mwafimbo alidai mbele ya Hakimu Rusema kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Januari 13, mwaka huu katika Mtaa wa Migombani, nyumba namba 147 eneo la Mikocheni.

  Katika shitaka la kwanza ilidaiwa kuwa, katika siku na muda ambao haujafahamika, mshitakiwa pamoja na wenzake ambao hawajafikishwa mahakamani hapo, walipanga njama ya kutenda kosa hilo.

  Mwafimbo alidai mshitakiwa akiwa na wenzake, alijipatia fedha hizo kutoka kwa Said Maenda kwa madai kuwa wangemuuzia kilo 36 za vipande vya dhahabu, jambo ambalo si kweli.

  Mshitakiwa alikana mashitaka na kuachiwa kwa dhamana hadi Machi 9, mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena.

  Katika hatua nyingine, Shabani Yasini (31) na Swalehe Shabani (25), wamefikishwa katika mahakama hiyo kwa tuhuma za kuiba kompyuta ndogo ya mkononi yenye thamani ya Sh milioni mbili mali ya Aloyce Mushi.

  Mwendesha Mashitaka Masini Mnubi alidai mbele ya Hakimu Susan Kihawa kuwa Februari 14, mwaka huu saa moja jioni katika eneo la Ubungo Plaza, mshitakiwa aliiba kompyuta hiyo.

  Mshitakiwa alikana mashitaka na kuachiwa kwa dhamana hadi Machi 9, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

  source: HabariLeo

  Hivi vyombo vya usalama huwa havina nafasi ya kuwafanyia 'vetting' viongozi ambao wanaweza kuja kushika nyadhifa kubwa mbeleni? Maana sitegemei atabadilika akija kushika unaibu waziri, uwaziri, ubunge nk..Huyu Said anafahamika kwa utapeli mjini,ilikuwaje kushika nafasi kama hii?

  Na UVCCM Taifa kama baba na mama zao (CCM) huwa hawachukui hatua zozote kwa watu wa aina hii...Benno, Shigella na wengineo kazi kwenu baada ya Mwenyekiti wa Ruvuma (Ngwenya) sasa wa DSM...

  Na wa Ruvuma pia alionyesha njia-gonga hapa
   
 2. MmasaiHalisi

  MmasaiHalisi Senior Member

  #2
  Nov 5, 2011
  Joined: Jan 15, 2009
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 3. MmasaiHalisi

  MmasaiHalisi Senior Member

  #3
  Nov 5, 2011
  Joined: Jan 15, 2009
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  2015 ndiye mrith wa yule Al shabaab,Ismail madeni ya maharage pale tabora mjini
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,185
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  ukipanda mahindi unavuna mahindi sio mabua
  kaulize mamake aliiba ngapi ndio utajua waliopo ndio wapo
   
Loading...