Mwenyekiti UVCCM, Kheri James aomba radhi kwa watu wote waliokerwa na kauli yake

Kuna kauli walishauliwa kuwa wafanye chochote kama wataumiza tabaka lolote wataomba msamaha, lkn hizo ni za kuambiwa inatakiwa wachanganye na zao.
 
Mbona aliongea ukweli wa mambo ulivyo! kwani kuna tatizo gani na hayo maneno kwa muktadha wa sasa wa kisiasa name kiutawala?
 
Nilijua ipo siku atarudi kinyume nyume........natafakari damage Aliyotengeneza kwa hiyo kauli, na bado sio yeye tu,muda ndio huamua......wapo wengi watakuja kuomba msamaha hapo mbeleni.
 
Mimi binafsi sijakerwa na speech ile,kwangu ilikuwa ukweli,ukweli,ukweli..msema kweli ni mpenzi wa mungu.
 
"Nachukua nafasi hii kuwaomba Radhi Watanzania Wenzangu wote walio kerwa na ujumbe huo,na ninawashukuru viongozi wote wa kisiasa na kiraia walio nikosoa na kunikemea kwa maslahi mapana ya Taifa letu,ninawashukuru sana" Kheri James Mwenyekiti UVCCM Taifa

View attachment 822683

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James ametengua kauli yake inayosema ‘CCM ndiyo inayoamua maendeleo yaje au yasije na hakuna mwananchi anayeweza kuchukua hatua yoyote dhidi ya chama hicho’.

Akimnadi mgombea wa udiwani Kata ya Bagara, mkoani Manyara, Nicodemus Tlaghasi James alisema CCM haiwezi kupeleka maendeleo kwenye maeneo yanayoongozwa na upinzani.

James alitoa kauli hiyo wiki iliyopita katika mtaa wa Mpya wilayani Babati akisema CCM haiwezi kupeleka maendeleo kwa wananchi waliochagua viongozi wa upinzani badala ya CCM.

Akizungumza leo Julai 30, 2018 na Mwananchi James amesema amefikia uamuzi huo baada ya kupokea simu za kumkemea na kumuonya juu ya kauli hiyo.

“Anayepokea sentensi hiyo, hawezi kujua mwanzo ulisema nini na mwisho ulisema nini, nimeamua kufanya kitu cha kiungwana kwamba ilimradi kilichopokelewa kwenye jamii ni kibaya, tumeamua kuomba radhi bila kujali mwanzoni na mwisho nilisema nini,” amesema James.

Chanzo: Mwananchi

Hivi ya huko Manyara ni kali zaidi ya Cha-Arusha!
 
Huyo kijana hajitambui na inaonyesha amelewa madaraka lkn mpangaji ni mungu
 
Wapuuzi nyie, mmesema yaliyojaa mioyoni mwenu, je ulichosema si ni kweli? Au uongo?
 
Edward N Lowasa(rtd PM) alivyokutana na Rais wa URT aliusia viongozi kuchunga kauli zao kwani amani ya nchi hii ni muhimu kuliko chochote kile, na kuna watanzania walipambana mpaka hapa tulipo day and night, wengine wametangulia mbele ya haki na wengine bado wako hai, sifa ya kiongozi ni unyenyekevu kwa wale anaowaongoza, kiongozi akianza kutoa lugha ya kejeli , dharau na iliyojaa kiburi si ishara njema, nawashukuru hao viongozi waliomfahamisha kuwa kwa maneno yale alikuwa amekengeuka si lugha ya kuombea kura hata kidogo, na si kura tu ila si lugha inayotakiwa kutoka kwa kiongozi anaeamini katika utawala wa sheria na uongozi wa kidemokrasia, safari bado ni ndefu, M/Mungu awajaalie viongozi wetu wawe na lugha ya kistaarabu na kiasi katika shughuli zao , every word to them gonna ferry or bury them, they have to put their brain engaged before putting their mouth into gear , merci beaucoup!
Kuna aliyemtuma, Huyo ndo tatizo, huenda hatafurahi dogo kuomba msamaha.
 
Ila hio kauli MBONA isharudiwa sana kuanzia mnyeti arumeru na makonda kinondoni,pia katika hali halisi majimbo ya upinzani yanapewa vipaumbele kidogo sana kupewa hewa za maendeleo.
 
Back
Top Bottom