Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
"Nachukua nafasi hii kuwaomba Radhi Watanzania Wenzangu wote walio kerwa na ujumbe huo,na ninawashukuru viongozi wote wa kisiasa na kiraia walio nikosoa na kunikemea kwa maslahi mapana ya Taifa letu,ninawashukuru sana" Kheri James Mwenyekiti UVCCM Taifa
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James ametengua kauli yake inayosema ‘CCM ndiyo inayoamua maendeleo yaje au yasije na hakuna mwananchi anayeweza kuchukua hatua yoyote dhidi ya chama hicho’.
Akimnadi mgombea wa udiwani Kata ya Bagara, mkoani Manyara, Nicodemus Tlaghasi James alisema CCM haiwezi kupeleka maendeleo kwenye maeneo yanayoongozwa na upinzani.
James alitoa kauli hiyo wiki iliyopita katika mtaa wa Mpya wilayani Babati akisema CCM haiwezi kupeleka maendeleo kwa wananchi waliochagua viongozi wa upinzani badala ya CCM.
Akizungumza leo Julai 30, 2018 na Mwananchi James amesema amefikia uamuzi huo baada ya kupokea simu za kumkemea na kumuonya juu ya kauli hiyo.
“Anayepokea sentensi hiyo, hawezi kujua mwanzo ulisema nini na mwisho ulisema nini, nimeamua kufanya kitu cha kiungwana kwamba ilimradi kilichopokelewa kwenye jamii ni kibaya, tumeamua kuomba radhi bila kujali mwanzoni na mwisho nilisema nini,” amesema James.
Chanzo: Mwananchi
Last edited: