Mwenyekiti UVCCM aachishwa kazi Wizara ya Nishati na Madini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenyekiti UVCCM aachishwa kazi Wizara ya Nishati na Madini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwenda_Pole, Sep 3, 2009.

 1. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2009
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana Taifa wa Chama cha Mapinduzi (Uv-CCM) Hamad Yusuf Masauni, ameachishwa kazi katika Wizara ya Nishati na Madini.

  Hata hivyo, taarifa kutoka vyanzo vya habari zinasema kuwa uongozi wa wizara ulichukua uamuzi huo kutokana na fitna iliyosababishwa na msuguano wa kisiasa kati ya bosi huyo wa UVCCM na mtoto wa kigogo mmoja wa Ikulu.

  Hata hivyo, Masauni mwenyewe akizungumza na gazeti hili kwenye hoteli ya Court Yard, jijini Dar es Salaam jana alikataa kuwepo mizengwe kwenye hatua hiyo ya mkataba wake kutenguliwa.

  Masauni alifahamisha kuwa kilichofanyika ni taratibu za kisheria, ambazo zinaeleza wazi kuwa mtu hawezi kuwa kwenye utumishi wa umma wakati anashikilia nafasi ya juu katika chama cha siasa.

  "Hapana, nakataa hakuna aina yoyote ya mizengwe ni sheria tu, kilichofanyika ni sheria tu...kwa sababu huwezi kuwa mtumishi wa umma halafu unashikilia nafasi ya juu ya kisiasa," alisisitiza.

  Masauni alifafanua akisema: "Hata mimi mwenyewe nimeona si sahihi, niwe kwenye siasa na wakati huohuo niendelee na kazi za serikalini; nitakuwa sitendi haki."

  Masauni ambaye huzungumza mambo kwa umakini mkubwa, alisema hakuna athari wala tatizo lolote ambalo amelipata hadi sasa kutokana na uamuzi huo.

  "Kila kitu kinakwenda vizuri, mimi ndiyo mhusika mkuu, nakueleza na nakuhakikishia kuwa hakuna tatizo ambalo nimelipata hadi sasa hivi wala sijaathirika," aliongeza.

  Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Athur Mwakapugi alisema hakuwa amepata taarifa hizo hadi jana.

  "Hadi sasa hivi sijapata taarifa hizo, labda unipe muda nimuulize Mkurugenzi wa Utawala ndipo nitakupa jibu kuhusu suala hilo," alifafanua.

  Hata hivyo, vyanzo huru vya habari ndani ya chama na serikali, vilisema ingawa serikali ndiyo iliyomwachisha kazi Masauni, lakini inaelezwa inatokana na kutofautiana msimamo na mtoto huyo wa kigogo wa Ikulu.

  Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, mtoto huyo ambaye ana kiburi kinachotokana na madaraka ya mzazi wake, anapotafutwa na vyombo vya habari hujibu jeuri.

  Vyanzo hivyo viliongeza kwamba, karibuni baada ya kijana huyo kupishana kimsimamo na Masauni aliamua kupenyeza fitna wizarani na kusababisha bosi huyo wa UVCCM kuachishwa kazi, kwa kutumia mwanya wa kutenganisha utumishi wa umma na siasa.

  Vyanzo hivyo vinadai kuwa kijana huyo ana malengo ya kisiasa hapo baadaye na amekuwa akijaribu kujipenyeza kwa kasi, ili kufika kileleni na tayari ameshaanza mikakati yake.

  Kwa muda mrefu UVCCM imekuwa kwenye vita ya makundi ambayo inahusisha vigogo mbalimbali wakiwemo kundi la mafisadi na wale wanaopinga ufisadi.

  Uchaguzi uliowaingiza kina Masauni, ulitawaliwa na mchezo mchafu kati ya kambi hizo mbili, ambazo zote zilitaka kupandikiza watu wao.
  Source: Mwananchi 2/9/2009

  Wadau nimeona nilete hii hapa jamvini "where we dare to speak openly", magazeti yetu yamezoea kutuletea habari nusu nusu kama hizi kwa muda mrefu sana.
  Huyu mtoto wa kigogo anaitwa nani na Mzazi wake?? manake tulizoea kuona viongozi ndio wanafanya ofisi za umma mali zao sasa naona ofisi zimeanza kuwa mali ya familia.
   
 2. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mambo ndiyo haya!!! Ukweli kwa sheria za utumishi wa umma ukiingia kwenye Siasa ni lazima ujiuzulu kazi??? Sasa mnasema ameachishwa kazi au kiswahili ni kigumu?? Tofautisheni maneno yanayopotosha. Pia itapendeza kama mtatupatia hiyo barua ili tusome wenyewe sahihi kilichoandikwa huko.

  At the same Masauni ni mfano wa kuigwa, he is calm hata katika kongea na waandishi si kama yule dogo Zitto aliyesema ameacha kazi kwa kuheshimu maamuzi ya wazee na kuleta longo longo nyingi sana za kitoto!!

  Na hawa waandishi wapambane mambo!!! ...mtoto wa kigogo mmoja wa Ikulu!!!! Hii ni tata !!! Je inamaanisha mtoto mwenyewe yuko Ikulu au ni mzazi wake yuko Ikulu?? Tehe tehe. Ngoma nzito!!!
   
Loading...