Mwenyekiti Ulinzi na Usalama (W) anaporatibu vurugu wilayani

WanaJF

Baada ya matukio ya kihuni yaliyoratibiwa na wahuni na washenzi kule jimboni Hai ya kuwashambulia kwa mawe na silaha kwa lengo la kumdhuru Mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Lissu watu mbalimbali wametoa maoni yao

Kwa vile Molemo Media ni Taasisi huru tutawaletea maoni hayo bila kuyachuja.

Kwanza wananchi wote waliohojiwa wanaamini vikundi hivyo vya wahuni jimboni Hai vinaratibiwa na mkuu wa wilaya hiyo Sabaya Ole Lengai kutokana na chuki kubwa aliyonayo kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kwa sababu alishajiapiza atahakikisha Mbowe harudi Tena Bungeni.

Wananchi wengi wamewashutumu viongozi wa CHADEMA kuanzia ngazi ya Jimbo, Mkoa na Kanda ya Kaskazini kwa kuonyesha udhaifu mkubwa wa kuwalinda viongozi wao.

Wananchi hao wamesema vitendo hivyo vya kihuni vya Jimbo la Hai ni vya muda mrefu na inajulikana anayeviratibu kwa lengo baya na la kishenzi.

Wananchi wamesema Jimbo la Hai zaidi ya robotatu ni wanachama wa Chadema na idadi kubwa ya wafuasi vijana ni Chadema ambao wakiamua Wana uwezo wa kuteketeza wahuni hao wanaotumwa kuvuruga mikutano ya Chadema.

Wananchi hao wamesema kwa vile vitendo hivyo vya kihuni vimekuwa vikiratibiwa muda mrefu na Polisi wamekuwa hawachukui hatua yoyote Basi ni wajibu wa viongozi wa Chadema kuanzia Jimbo, Mkoa na Kanda kuwaandaa vijana wa Chama hicho kulinda viongozi wao na kusambaratisha wahuni hao.

Wananchi hao wamesema itakuwa aibu na Fedheha kubwa kwa wahuni wasiozidi 50 kuvuruga kila Leo mikutano ya Chadema inayohudhuriwa na watu kwa uchache elfu 5.Viongozi wanapaswa kuwaandaa vijana wa Chadema kuwakabili vilivyo kwa nguvu kubwa wahuni hao ili iwe onyo na fundisho kwamba mikutano ya Chadema siyo ya kuchezea.

Baadhi ya wanachama wa Chadema Jimbo la Ubungo DSM wamewataka viongozi wa Kanda ya Kaskazini waseme wazi Kama wameshindwa kuwaandaa vijana wa Chadema kuwakabili na kuwateketeza wahuni hao Basi waombe msaada Kanda nyingine za chama hicho.

Wanachama wa Chadema Tarime wamesema inasikitisha kusoma kwenye mitandao ya kijamii viongozi wa Chadema Kanda ya Kaskazini wakitoa maandiko ya kulalamika kuvamiwa na kupigwa badala yake wanatakiwa waandike wahuni wametuvamia tumejilinda na wanne Kati ya wahuni hao wako mahututi KCMC na kupona yao ni Majaliwa!

Kwa maoni haya ya Wananchi na wanachama Molemo Media inaamini viongozi wa Chadema Kanda ya Kaskazini watajitafakari na kuchukua hatua kwa lengo la kulinda heshima ya viongozi wake.
Unyonge Sasa baasi, Nini kwa jino
 
Hivi hakuna hata mmoja aliyeuawa? Haiwezekani kikundi cha watu wachache wanaojifanya wahuni wavamie msafara wa mgombea uraisi afu wasifanywe chochote.
Mbowe anatakiwa achane na habari za tunamwachia Mungu, Mungu mwenyewe alikua anawapa wana Israeli mbinu za kuwapiga maadui zao wakati wakiendea nchi ya ahadi
 
Chadema acheni ujinga, mlitakiwanaenda kulipoti police wakati vijana hata watano hao mmewaua.
Ili siku nyingine hao vijana wawe wanaogopa kutumika
 
Hapo wanatafutiwa sababu viongozi wawaambie wananchi nao wajihami kisha wapewe kesi viongozi wa chadema kuwa wao ndio wamesababisha. Ila me mwenyewe naisikitikia Chadema kutoweka mazingira mazuri ya Kujilinda. Hata sioni mantiki ya Kauli mbiu yao ya "Sasa basi", inafanya kazi wapi? Lini na kivipi?
 
Hapo wanatafutiwa sababu viongozi wawaambie wananchi nao wajihami kisha wapewe kesi viongozi wa chadema kuwa wao ndio wamesababisha. Ila me mwenyewe naisikitikia Chadema kutoweka mazingira mazuri ya Kujilinda. Hata sioni mantiki ya Kauli mbiu yao ya "Sasa basi", inafanya kazi wapi? Lini na kivipi?
Viongozi wanachukua maoni ya wananchi
 
Ni aibu kwa ccm na DC mpumbavu kutaka kuingiza nchi katika vita isiyo na maana!
Lakini kabla hatujamlaumu CD wa Hai, tuwalaumu viongozi wa jimbo na kanda ya Kaskazini kwa hiki kilichotokea. Mimi naungana na wananchi wanaosema viongozi wetu hawakuwajibika ipasavyo! Tuache kulialia!
 
Haya maoni siyo ya wananchi, ni ya wanachama wa Chadema. Kwahiyo sahihisha kauli yako. Habari haipo balance, inaonekana hicho kimedia chenu kimejaa makanjanja.
 
Naviona vikwazo vya kiuchumi kwa mbaaali. Naona complaints rasmi zikipelekwa ICC na UN huku uchunguzi rasmi ukiamliwa kufanyika dhidi ya Tanzania, kiongozi mkuu wa Tanzania na wakuu wake wa vyombo vya usalama hasa IGP, DGIS, na viongozi wa kisiasa kama Ole Sabaya, Paul Makonda(aliyekuwa RC DSM) na wengineo wengI...
Haya mawazo ni ya kibangibangi kabisaaa.. yaani it is typical hallucinations. Unahitaji tiba ya haraka sana na uache hicho kitu unachotumia.
 
Chama kijipange, kisitegemee vyombo vya dola kulinda usalama wao japo wananchi wa vyama vyote wanalipa kodi ambayo moja ya matumizi yake ni kulipa vyombo hivyo ili vihakikishe ulinzi na usalama upo kwa raia wake

Chama kiwe kinaandaa wanasheria kabisa, ikitokea vurugu kama hizo,wafuasi wawashughulikie inavyotakiwa na iripotiwe inavyotakiwa
Mkuu umeongea kitu kikubwa sana na chadema hii pointi waichukue.
 
Huyo mmasai ni sharti afahamu kuwa, Magufuli will never be there always to protect him, someday he will stand alone in the dock to account for these rubbish he is perpetrating.
 
Daah Inavyoonekana hao watu waliletwa na Lisu kuwafanyia fujo wakazi wa hai.

Ni ajabu sana mgombea wa nafasii ya Urais kutembea na vikund vya wahuni

Wahuni si hao wanaongea utopolo hapo hao au huoni wahuni hata uso unaonekana wenye haya
 
Back
Top Bottom