Mwenyekiti Ulinzi na Usalama (W) anaporatibu vurugu wilayani

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,745
71,103
Mkuu wa wilaya ya Hai Sambai ametajwa Leo katika mahojiano ya Polisi Moshi kuwa aliratibu vijana wa kufanya fujo Bomang'ombe na kurusha mawe kwa ujira wa Elfu 20 kila mmoja.

Hivi Rais Magufuli, uliwatoa wapi vijana kama hawa na kuwapa madaraka? Kweli mtu anayekuwa mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama wilayani anaweza kuunda kikundi cha kurusha mawe ndani ya kundi la watu wakiwa katika shughuli zao? Huyo ndio mwakilishi wako?

Katika nchi zilizo starabika huyu kesha chafua hadhi yako ya uteuzi na alipaswa kuwekwa pembeni uchunguzi ukiendelea. Lakini sio ajabu akapongezwa na kuheshimiwa zaidi kwani kafanya jambo linalo kupendeza.

Hizi zaweza kuwa sababu za kukunyima kura mheshimiwa Magufuli.

Screenshot_20200814-222856.jpg
 
Sasa wale mabaunsa walikuwa wapi? walinzi wa mbowe walikuwa wapi? hai bila kutoa hela ya mbege watakudunda tu, hata mbowe analijua hilo,
 
Mkuu wa wilaya ya Hai Sambai ametajwa Leo katika mahojiano ya Polisi Moshi kuwa aliratibu vijana wa kufanya fujo Bomang'ombe na kurusha mawe kwa ujira wa Elfu 20 kila mmoja...
Kwa hali ya kawaida tu ya kibinadamu lazima Magufuli na genge lake wawe na woga. Mtiti wa Lissu sio wa kitoto ule hamani muoneeni huruma.

Tushukuru Mungu hakuna madhara Makubwa.
 
Kama Mungu aliamua kuwalinda Watanzania dhidi ya Ugonjwa wa Korona na watu wakamshukuru Mungu kwa uwezo wake mkuu na jinsi alivyowapenda Watanzania basi hata hili nalo Mungu atawalinda watu wake kwa kuwafukuzilia mbali wale wote wanaogeuka kuwa wabaya na kuchukua nafasi ya Korona(covid 19), yaani kuna watu wanataka kuleta madhara kwa wenzao kama ilivyo Korona. Hawa pia tumwachie Mungu awapeperushe kama alivyopeperusha Korona.

Niwashauri wapinzani kama kweli wana nia ya kuliongoza Taifa hili kwa amani ,upendo,haki,umoja,mshikamano, usawa na kupiga vita Rushwa na dhulma zote za kidini kikabila na kikanda basi kila wanapokutana Wasome dua maalum na maombi ya kumkabidhi Mungu siasa za Tanzania ili Mungu apambane na watesaji na walioko nyuma yao.
Ikiwezekana isomwe Albadiri na Zaburi kwa ajili ya waliompiga Tundu Lisu , waliomuua Mawazo, waliomuua ,Azori ,Waliompoteza Saanane. Isomwe Albadiri na Zaburi Maalumu kwa ajili ya wale wanaoteka watu na kulichafua Taifa letu ili damu wanazomwaga ziwe juu yao na vizazi vyao vyote.

Wapinzani Sasa wamuombe Mungu asimame kuwatetea Wale wanaopoteza ndugu,wazazi na watoto wao kwa sababu tu ya watu wanaotumia nafasi zao kulinda madaraka kwenye nchi ya kidemokrasia. Taifa linaongozwa na sheria na Katiba ambayo kila kiongozi anaapa kuilinda akiwa ameshika Msahafu wa dini yake.
Sasa wapinzani wasipuuze Bali wasimame na kumwomba Mungu asimamie vile viapo vya viongozi walivyoapa wakati wa kupewa madaraka.
Kama wanakiuka viapo vyao Mungu awaadhibu hapa hapa duniani walipoapa kutenda haki.

Ni lazima wapinzani wazitizame siasa zinazoendelea kiroho mana sio kawaida kwa Viongozi wa Dini tena ya kikristo kukaa kimya na kuangalia watu wakiwa wanafanyiwa unyama kwa sababu ya ujenzi wa mapiramidi na minara ya babeli inayojengwa kwa kodi ya wote.
Wachache wanatumia kodi ya wote kuwaumiza watu. Watu wanalipa kodi zao kwa machungu halafu zinageuka kuwa mateso kwa ndugu zao kwa sababu tu ya wale waliozoea Raha za madaraka na woga wa kunyimwa kura.
 
These crimes against humanity entail extermination, murder, enslavement, torture, imprisonment, rape, forced abortions and other sexual violence, persecution on political, religious, racial and gender grounds, the forcible transfer of populations, the enforced disappearance of persons and the inhumane act of knowingly ...
 
Kama Mungu aliamua kuwalinda Watanzania dhidi ya Ugonjwa wa Korona na watu wakamshukuru Mungu kwa uwezo wake mkuu na jinsi alivyowapenda Watanzania basi hata hili nalo Mungu atawalinda watu wake kwa kuwafukuzilia mbali wale wote wanaogeuka kuwa wabaya na kuchukua nafasi ya Korona(covid 19), yaani kuna watu wanataka kuleta madhara kwa wenzao kama ilivyo Korona. Hawa pia tumwachie Mungu awapeperushe kama alivyopeperusha Korona.

Niwashauri wapinzani kama kweli wana nia ya kuliongoza Taifa hili kwa amani ,upendo,haki,umoja,mshikamano, usawa na kupiga vita Rushwa na dhulma zote za kidini kikabila na kikanda basi kila wanapokutana Wasome dua maalum na maombi ya kumkabidhi Mungu siasa za Tanzania ili Mungu apambane na watesaji na walioko nyuma yao.
Ikiwezekana isomwe Albadiri na Zaburi kwa ajili ya waliompiga Tundu Lisu , waliomuua Mawazo, waliomuua ,Azori ,Waliompoteza Saanane. Isomwe Albadiri na Zaburi Maalumu kwa ajili ya wale wanaoteka watu na kulichafua Taifa letu ili damu wanazomwaga ziwe juu yao na vizazi vyao vyote.

Wapinzani Sasa wamuombe Mungu asimame kuwatetea Wale wanaopoteza ndugu,wazazi na watoto wao kwa sababu tu ya watu wanaotumia nafasi zao kulinda madaraka kwenye nchi ya kidemokrasia. Taifa linaongozwa na sheria na Katiba ambayo kila kiongozi anaapa kuilinda akiwa ameshika Msahafu wa dini yake.
Sasa wapinzani wasipuuze Bali wasimame na kumwomba Mungu asimamie vile viapo vya viongozi walivyoapa wakati wa kupewa madaraka.
Kama wanakiuka viapo vyao Mungu awaadhibu hapa hapa duniani walipoapa kutenda haki.

Ni lazima wapinzani wazitizame siasa zinazoendelea kiroho mana sio kawaida kwa Viongozi wa Dini tena ya kikristo kukaa kimya na kuangalia watu wakiwa wanafanyiwa unyama kwa sababu ya ujenzi wa mapiramidi na minara ya babeli inayojengwa kwa kodi ya wote.
Wachache wanatumia kodi ya wote kuwaumiza watu. Watu wanalipa kodi zao kwa machungu halafu zinageuka kuwa mateso kwa ndugu zao kwa sababu tu ya wale waliozoea Raha za madaraka na woga wa kunyimwa kura.
albadili ilishasomwa we uoni matokeo
 
Mkuu wa wilaya ya Hai Sambai ametajwa Leo katika mahojiano ya Polisi Moshi kuwa aliratibu vijana wa kufanya fujo Bomang'ombe na kurusha mawe kwa ujira wa Elfu 20 kila mmoja.

Hivi Rais Magufuli, uliwatoa wapi vijana kama hawa na kuwapa madaraka? Kweli mtu anayekuwa mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama wilayani anaweza kuunda kikundi cha kurusha mawe ndani ya kundi la watu wakiwa katika shughuli zao? Huyo ndio mwakilishi wako?

Katika nchi zilizo starabika huyu kesha chafua hadhi yako ya uteuzi na alipaswa kuwekwa pembeni uchunguzi ukiendelea. Lakini sio ajabu akapongezwa na kuheshimiwa zaidi kwani kafanya jambo linalo kupendeza.

Hizi zaweza kuwa sababu za kukunyima kura mheshimiwa Magufuli.
 
Mkuu wa wilaya ya Hai Sambai ametajwa Leo katika mahojiano ya Polisi Moshi kuwa aliratibu vijana wa kufanya fujo Bomang'ombe na kurusha mawe kwa ujira wa Elfu 20 kila mmoja.

Hivi Rais Magufuli, uliwatoa wapi vijana kama hawa na kuwapa madaraka? Kweli mtu anayekuwa mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama wilayani anaweza kuunda kikundi cha kurusha mawe ndani ya kundi la watu wakiwa katika shughuli zao? Huyo ndio mwakilishi wako?

Katika nchi zilizo starabika huyu kesha chafua hadhi yako ya uteuzi na alipaswa kuwekwa pembeni uchunguzi ukiendelea. Lakini sio ajabu akapongezwa na kuheshimiwa zaidi kwani kafanya jambo linalo kupendeza.

Hizi zaweza kuwa sababu za kukunyima kura mheshimiwa Magufuli.
Tunzeni hizi kumbukumbu ili mwezi was kumi nikiingia ikulu nianze nae huyu Pimbi wa kutupa Ole sabaya.
 
Back
Top Bottom