Mwenyekiti Tume ya Uchunguzi Uvamizi Clouds TV, ndugu Deodatus Balile atishiwa Maisha

steve_shemej

JF-Expert Member
Nov 26, 2015
1,043
2,000
Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe, ufalme wako ufike, utakalo lifanyike duniani kama mbinguni, utupe leo mkate wetu wa kila siku, utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea, usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe mauvuni... kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu hata milele. Amina.

Juzi mawasiliano ya ofisini kwetu yalidukuliwa. Makala inayopaswa kusomwa kesho, waliojiteua kuwa wasaidizi wa aliyetaka nimwombe radhi kwa kufanya kazi niliyotumwa mchana kweupe, wametamba kuwa wanafuatilia maisha yangu hadi uvunguni mwa kitanda changu.

Nimeona nisali kwa sauti sala hii, ili nikipotea, hawa wasaidie kutoa majibu nilipo. Nimeambatanisha baadhi ya meseji zao za udukuzi kwangu.

Balile

1aff131093ffb1b62e52243f7d0b04f2.jpg


a4b7a1daf3ce7a614e79d0c0cfa4a8c1.jpg
 

Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,832
2,000
Hata Dkt Wilbroad Peter Slaa alikuwa anapata Kick kwa hako kamsemo 'kuna watu wananifuatilia waniteke'

Waliotekwa wote hawajawahi kuhisi watatekwa!


Babile kachagua kuwa Wakala wa Wauza dawa za kulevya!

Hii Tabia ya kujitumia sms za kujitisha na kusema wametishwa ilianza enzi za Slaa Naona Nyumbu ndio urithi pekee waliobaki nao kwa Yule Babu
 

Ngushi

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
9,080
2,000
Hivi hawa washenzi wanaotisha watu kweli imeshindikana kupata mmiliki wa simu iliyotuma SMS!
Hii nchi inavituko sana,Roma eti mpaka siku tatu simu IPO hewani ila haifahamiki uko maeneo gani!
Ama kweli tupo nchi za ulimwengu wa tatu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom